MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,975
Mgombea Uenyekiti wa CHADEMA Taifa, Cecil David Mwambe ameahidi kujenga jengo jipya la Ofisi ya Makao Makuu ya CHADEMA pindi atakapochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na kuachana na jingo la sasa ambalo halina hadhi ya CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani.
Hayo ameyasema baada ya kufanya mahojiano na mwandishi wa habari na mtandao wa DarMpya nchini.
Mgombea huyo amedai mpaka sasa CHADEMA kimepokea kutoka serikalini kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 13 kama ruzuku lakini pesa hizo hazikupangiwa mipango mizuri ya kukiendeleza chama.
Mgombea huyo amedai kama atachaguliwa atahakikisha Makatibu wa Majimbo, Mikoa na Wilaya wanapata posho zitakazowawezesha kutimiza majukumu yao tofauti na sasa ambapo hawalipwi.
Amemaliza kwa kusema, atahakikisha mapato na matumizi ya pesa za chama yanakuwa wazi tofauti na sasa ambapo ni siri ya viongozi wachache.