Cecafa yasitisha mashindano yote kwa mwaka 2020 kutokana na Corona

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
  • Kagame Cup ambayo inashirikisha mabingwa kutoka wanachama 12 wa Cecafa, ni moja ya shindano kongwe barani Afrika ambalo kwa muda mrefu limekuwa likidhaminiwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame.
d78e5a30785944c16a2ff9b45a7f5c6f

Dar es Salaam. Baraza la Vyama Vya Mpira wa Miguu la Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), limefuta mashindano yote mwaka huu kutokana na ugonjwa wa Covid19.

Moja ya mashindano hayo ni klabu bingwa ya Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) ambayo yalipangwa kufanyika mwaka huu hapa nchini.

Kagame Cup ambayo inashirikisha mabingwa kutoka wanachama 12 wa Cecafa, ni moja ya shindano kongwe barani Afrika ambalo kwa muda mrefu limekuwa likidhaminiwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame.

Shindano hilo lilipangwa kufanyika nchini mwezi huu, lakini ratiba ilibadilika kutokana na kuendelea kwa Ligi Kuu Bara na kuondoa uwezekano wa kufanyika hata kwa miezi ya mbele.

Mbali ya kuendelea kwa ligi ya Bara, shindano hilo pamoja na mengine yamefutwa kutokana na zuio la michezo na mikusanyiko kwa baadhi ya nchi wanachama za Cecafa.

Rais wa Cecafa, Wallace Karia alisema ukiondoa Burundi na Tanzania, nchi nyingine bado zipo katika zuio la shughuli za michezo na mikusanyiko mingine jambo ambalo linawapa tabu kufanya mashindano hayo.

Karia alisema kuwa afya ni muhimu kuliko jambo lingine na wanaheshimu uamuzi wa nchi nyingine kuzuia mikusanyiko.

“Kenya wameweka zuio mpaka mwakani, Rwanda na nchi nyingine ukiondoa Burundi na Tanzania kuendelea na shughuli mbalimbali, bado nchi hizo haziwezi kufanya mashindano peke yake,” alisema.

Alisema Cecafa itajipanga mwakani kuona ni mashindano gani yatafanyika kwa kutegemea na hali ya ugonjwa huo

Mbali ya Kombe la Kagame, michuano mingine maarufu ambayo imefutwa ni Kombe la Chalenji ambalo lilipangwa kufanyika nchini Sudan mwezi Novemba na Desemba.

Kwa mujibu wa Cecafa, Burundi ilipewa nafasi ya kuandaa mashindano ya U-17 na U-20 wakati Rwanda ilipewa mashindano ya kufuzu ya Afcon ya U-17 na mashindano ya Chalenji ya wanawake.

Nayo Sudan ilipewa nafasi ya kuandaa mashindano ya U-20 ya kufuzu ya Afcon kwa nchi za Cecafa huku Djibouti ikipewa mashindano ya Cecafa ya U-16 na Uganda ikipewa yale ya U-20
 
Pamoja na kusitisha hilo kombe wangempa Simba tu kwani ukiondoa Burundi ndio timu pekee iliyochukua ubingwa kabla ligi haijaisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom