Cecafa na mashabiki wakibongo

AMARIDONG

JF-Expert Member
Jun 24, 2010
2,502
0
[FONT=ArialMT, sans-serif]Jana, michuano ya soka kwa nchi za Afrika Mashairiki na Kati maarufu kama Kombe la Chalenji ilifikia tamati baada ya kufanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 27 ambapo wenyeji, timu ya taifa ya Tanzania Bara’Kilimanjaro Stars’ ilicheza mechi ya ufunguzi dhidi ya timu ya taifa ya Zambia, ‘Chipolopolo’. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Stars ilibahatika pia kufunga michuano hiyo jana baada ya kuwafunga Rwanda na Uganda katika mechi za robo na fai8nali na nusu fainali na hatimaye kucheza fainali dhidi ya Ivory Coast, timu iliyoalikwa kwenye michuano hiyo ikitokea ukanda wa Afrika Magharibi. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kuna mambo mengi ya kuzungumzia kuhusina na matatizo na mafanikio yaliyojitokeza katika kipindi chote cha michuano hiyo ya Chalenji. Hata hivyo, sisi tunaona kwamba mojawapo kubwa la kulizungumzia, ni ushiriki wa mashabiki katika kufika uwanjani kwa wingi na kuzishangilia timu mbalimbali, hasa wenyeji Kilimanjaro Stars na timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kabla ya kuanza kwa michuano hiyo, kulikuwa na hofu kubwa kwamba hakutakuwa na msisimko unaotazamiwa na wasiwasi ulitokana zaidi na uwezekano wa kuwa na mashabiki wachache uwanjani. Baada ya waandaaji, TFF na CECAFA kushindwa kupata idhini ya kuutumia uwanja mdogo wa Uhuru kutokana na mwingiliano wa ratba yao na ile ya maadalizi ya sherehe za uhuru zilizofikia kilele Desemba 9, woga wa kupooza kwa michuano ukazidi. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Ni kwamba, mechi zote za michuano hiyo kutakiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Taifa ambao ni mkubwa zaidi ya mara nne kulinganisha na ule wa Uhuru, kuliibua shaka kuwa michuano hiyo itakosa kabisa mashabiki. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa kawaida, ili viti vyote vya uwanja wa Taifa vijae na kuleta msisimko unaotarajiwa, idadi ya mashabiki inatakiwa isipungue 60,000 na hilo lilionekana kuwa ni ndoto kwa michuano ya Chalenji, hasa kutokana na uzoefu uliopatikana katika michuano kadhaa ya hapo kabla, ikiwemo miwili iliyopita katika nchi za Uganda na Kenya, ambapo licha ya Uganda kutwaa kombe na Kenya kufika mbali, bado hakukuwa na mashabiki wa kutosha viwanjani. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Katika mech ya ufunguzi ya Stars dhidi ya Zambia, hofu nyingine zaidi ilijitokeza. Mashabiki walijitahidi kufika kwa wingi uwanjani. Hata hivyo, kiwango cha chini kilichoonyeshwa na wenyeji katika mechi hiyo waliyolala 1-0 kilionekana kuwa kitakimbiza zaidi mashabiki na michuano kuweka rekodi ya kuwa na mahudhurio duni. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Baada ya hapo, waandaaji TFF na CECAFA waliketi na kuibuka na mbinu mbadala ya kuongeza hamasa, na ambayo tunaamini ilisaidia sana kuongeza msisimko na hatimaye uwanja kujaa kuliko kawaida. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Katika mechi ya mwisho ya Stars ya hatua za makundi dhidi ya Burundi, askari wa kutuliza ghasia (FFU) walilazimika kutumia virungu, mabomu ya machozi na kumwaga maji yao ya kuwasha ili kuwaondoa mashabiki wengi zaidi waliokosa nafasi baada ya uwanja kujaa mpaka pomoni. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hilo lilkuja baada ya waandaaji kutumia mbinu ya kuruhusu mashabiki waingie bure uwanjani katika mechi za hatua ya makundi isipokuwa wale wanaokalia viti maalum (VIP) na pia kutoa hamasa ya kila mara kupitia magazeti, televisheni na redio. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kama hiyo haitoshi, matokeo mazuri katika mechi zinazofuata za wenyej Stars na pia ndugu zao Zanzibar Heroes yalizidi kuinua hamasa na mwishowe uwanja ukawa ukipendeza kwa namna iliyosisimua. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa ubunifu wa TFF na CECAFA na mafanikio zaidi ya Stars iliyofanya vyema na kufika fainali jana, uwanja uliendelea kujaa hata pale kiingilio cha bure kilipofutwa na mashabiki kutakiwa kulipa kati ya Sh. 1,000 hadi Sh. 5,000. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Baada ya fainali ya jana iliyokuwa pia na mashabiki lukuki, sisi tunaamini bila shaka yoyote kuwa michuano ya mwaka huu itakuwa katika kumbukumbu za kuwa miongoni mwa mashindano ya yaliyovutia zaidi kulinganisha na mingine mingi ya CECAFA ya miaka ya hivi karibuni. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Ni kwa sababu hiyo, ndipo tunapoona kwamba waandaaji TFF na CECAFA wanastahili pongezi, lakini pia tukiamini kwamba watajifunza vilevile kuwa hamasa ya kutosha ikitolewa na viingilio vya mechi kuzingatia hali za kiuchumi za mashabiki wengi wa soka, idadi ya viti visivyokaliwa uwanjani katika kila mechi kubwa itapungua sana kama ilivyothibitika jana na siku Stars walipocheza dhidi ya Burundi na Rwanda [/FONT]
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom