CECAFA Final, 2017: Harambee Stars (Kenya) 2 - 2 Zanzibar Heroes, Kenya mabingwa kwa penati 3-2

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,444
7,808
Leo ni fainali Kati ya Kenya na Zanzibar kuwania kombe la CECAFA na dakika ya tano Kenya inaandika bao la kwanza kupitia kwa Ochieng Ovella baada ya kupiga mpira wa adhabu ndogo.

18' AbdulAziz Makame anaenda nje baada ya kupata maumivu ya paja. Nafasi yake inachukuliwa na Faisal Salum.

25' Aswan Kefa wa Kenya analamba kadi ya njano baada ya kumchezea ndivyo sivyo mchezaji wa Zanzibar.

41' Mwinyi Haji anakosa fursa ya kusawazisha baada ya kupiga mpira wa adhabu ndogo juu ya goli.

42' Almanusura Zanzibar wasawazishe baada ya beki wa Kenya kufanya makosa, mlinda mlango aliweza kuzuia hatari.

45+1' Kenya wanakosa bao la pili baada ya purukushani kwenye goli la Zanzibar kutokana na mpira wa Kona.

45+2' Mapumziko

45' Mpira umerejea kutoka mapumziko

56' Mlinda mlango wa Kenya analala chini baada ya kuguswa na mchezaji wa Zanzibar, baada ya muda anaendelea na mchezo.

59' Ochieng anagagaa chini baada ya kujaribu kuokoa mpira, anapoa na kuendelea na mchezo.

61' Keifa mchezaji wa Kenya anatolewa nje na machela. Masoud Juma anachukua nafasi yake.

76' Zanzibar wanacheza gonga nzuri langoni mwa Kenya lakini hesabu zao zinatibuliwa na beki wa Kenya.

78' Mfungaji pekee Hadi sasa, Ochieng anaenda benchi na nafasi yake kuchukuliwa na Ernest.

86' Onyango anaingia kuchukua nafasi ya George Odhiambo.

87' Zanzibar wanasawazisha, Hamisi Mussa Makame anaungasha krosi ya chini na kusawazisha. Kenya 1-1 Zanzibar.

90+3' Dakika 90 za mchezo zimemalizika.

Zimeongezwa dakika 30 za ziada. Leo ni lazima bingwa mpya apatikane.

97' Kenya 2 - 1 Zanzibar Heroes
Bao la pili la Kenya likifungwa na Masoud Juma baada ya kipa wa Zanzibar kufanya makosa.

99' Kenya 2 - 2 Zanzibar Heroes
Bao la pili la Zanzibar likifungwa na yuleyule Khamis Mussa Makame.

115' Kenya 2-2 Zanzibar.

120'. FULL TIME (Extra time): Harambee Stars (Kenya) 2 - 2 Zanzibar Heroes

Dakika 30 za nyongeza zimemalizika na mpira unaenda kwenye hatua ya matuta.

Penati ya kwanza ya Zanzibar Heroes inapanguliwa na Kipa wa kwenye

Penati ya Pili ya Zanzibar inapanguliwa tena na Kipa wa Kenya

Kenya wanakosa penati yao ya kwanza hapa

Kenya ndiyo mabingwa wapya wa michuano ya CECAFA kwa ushindi wa penati 3 kwa 2 dhidi ya Zanzibar baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika dakika 120 za mchezo.
 
Back
Top Bottom