CECAFA Championship Record: Any Conclusion | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CECAFA Championship Record: Any Conclusion

Discussion in 'Sports' started by Kichuguu, Jun 13, 2010.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Jun 13, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Baada ya uhuru tulikuwa na mashindano yanitwa Gossage Cup. Mashindano haya yalikuwa yanadhaminiwa na kampuni ya madawa ya Gossage; mashinado haya hayakuwa na uhusiano na yale mashati ya Gossage, Shikibo, na Kurabo yaliyokuwa maarfusu sana wakati huo. Gossage Cup ilikuwa inahusiha nchi za Kenya, Uganda, Tanganyika na Zanzibar tu. Kipindi hicho kulikuwa na wachzaji maarufu sana kama Joe Kadenge na Livingstone Madegwa wa Kenya, Joseph Massajage kipa wa Uganda, na Mohamed Msomali na Maulid Dilunga wa Tanzania.


  Mashindano haya yaliendelea hadi mwaka 1973 ambapo nchi za Somalia, Zambia na Ethiopia zilijiunga na mashindano hayo yakabilishwa jina na kuwa Ubingwa Afreika ya Mashariki na ya kati chini ya uongozi wa CECAFA ambao makao yake makuu yalikuwa Somalia kabla hayajahamishiwa Nairobi. Baadaye nchi nyingine kama Sudan, Malawi, Zambia na Zimbabwe zikajiunga na mashindano hayo. Mwaka 1994 baada ya uhuru wa Afrika ya Kusini, nchi za Zimbabwe, Zambia, na Malawi zilijitoa katika mashindano haya wakaanzisha ya kwao huko kusini, hivyo nchi za Rwanda, Burundi, Jibuti na Eritrea zikakaribishwa katika mashindano hayo. Wakati huo Rwanda ilikuwa katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

  Historia ya washindi wa mashindano haya kuanzia mwaka 1974 ni kama ifuatavyo.

  Utaona kuwa timu za Kenya na Tanzania zilikuwa mabingwa wa mashindano haya mara nyingi sana hadi mwaka 2002 ambapo kibao kiligeuka kikawa zaidi kwa Rwanda na Uganda. Kuanzia mwaka 2002, Tanzania imetwaa ubingwa huo mara moja, Kenya mara moja, Uganda mara tatu, na Rwanda mara nne.

  Hii inanirudisha kuwa uongozi wa Kagame, japo ni wa mkono wa upanga, umerudisha nidhamu sana huko Rwanda. Je matatizo yetu michezoni pia yanasababishwa na viongozi wa nchi kwa jumla ambao wamsheindwa kujenga nidhamu za kazi ?
   
 2. Golden Mean

  Golden Mean Member

  #2
  Jun 13, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ni kweli-i- i we, you're righto.
   
Loading...