CDM Pelekeni matumaini mapya kwa TZ, nendeni kawaambieni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CDM Pelekeni matumaini mapya kwa TZ, nendeni kawaambieni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Najijua, May 9, 2011.

 1. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  CDM wanaanza ziara ya operesheni sangara nyanda za juu kusuni wosia wangu kwao ni huu hapa

  Nendeni bila woga, nendeni kuwahubiria ukombozi wa taifa lao, nendeni kawaambineni TZ bila CCM amani inawezekana, kawaambieni waamke kutetea taifa na rasilimali zao,nendeni kawapeni ujasiri kuwa mabadiliko hata vijijini yanawezekana na sio mijini tu, nendeni kawaambien kwanini mpaka leo ni maskini wakati taifa lao lina rasilimali za kutoshamfano dhahabu, makaa ya mawe,mbuga za wanyama, na ardhi yenye rutuba ya kutosha

  Nendeni kawaambieni wasikubali kupokea T-Shirts na kofia bila suruali wala sketi tena wanakosewa heshima wanatakiwa kuvaa kwa miaka mitano,nendeni kawaambieni kiongozi kwa CCM ana anza maskini akimaliza muhula wake naye ni biliionea, nendeni kawaambieni watoto wao waliosoma vyuo vikuu kwa tabu, mlo mmoja kwa siku, kupigwa na virungu na bado hawapati ajira walio pata hazina tija wakati watoto wa vigogo wanapewa kazi nono kule BOT,ndani ya chama, ikulu na kwengineko, nendeni kawaambieni watoto wao ni ndoto kuwa viongozi wa taifa hili kwa kuwa tuu wao hawapo katika ukwasi na sio family friends kwa waliopo katika ukwasi.

  Nendeni kawaambien hatima ya nchii hii ipo mikononi mwao na wasihadaike na rusha roho na ngoma za siku moja wakati wanalia ukali wa maisha magumu, nendeni kawaelezeni safari hii wameambiwa ARI ZAIDI, KASI ZAIDI NA NGUVU ZAIDI, chaguzi zijazo ni wao kuamua kupunguza kasi ya kufanywa maskini, kupunguza kasi ya kufanywa madalali wa rasilimali za taifa lao

  Nendeni kawaelezeni wafanye maamuzi magumu na yote yanawezekana, Zambia, Malawi, Ghana, Nigeria na hata Ulaya wameweza na wao wanaweza, waache dhana potofu kuwa vyama vya upinzani ni Vita, waache dhana potofu eti CCM imewalea wakati haiwajali tena, kila siku ni afadhali ya jana na CCM yaom kila siku wanapokonywa ardhi zao na kila siku CCM wanayoipigania inawachangisha michango isiyo na tija wakati vigogo wanajilipa posho nono, kodi zinaongezeka wakati vigogo kila siku wanapanga safari za nje wakati mwingine hata kwenda kubembea Jamaica kwa kuwa fedha zao hazina kazi wakati madawa hakuna hospitalini


  Tupo nyuma ya CDM wakati wanapeleka habari hii, tupo tayari kuchangia kama kawaida yetu ili wapeleke habari njema, tupo tayari kuwalinda na kuwatetea daima, tupo nyuma yao wasikate tamaa
   
 2. O

  Omr JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama wana vitenge na t-shirt za kugawa basi watashabikiwa.
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Watanzania wameshaamka mkuu! Na ndo maana magamba wanagombana wenyewe!
   
 4. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Omr na hakika hawana vitenge na khanga, naamini hawana malori ya kwenda kubeba watu toka vijijini na sehemu nyingine ni watu wenyewe wana guswa na kujitokeza

  Tofauti yao na CCM ni kuwa CCM inawapa watu fedha na CDM inapewa fedha na watu wenyewe wanachanga ili viongozi wao wapate nauli za kwenda kwingine kupeleka habari za ukombozi
   
 5. O

  Omr JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tofauti yao ni CCM ndio chama tawala na CDM ni wapiga kelele. Wape mwaka mmoja tu hawa halafu watarudi kwa wazee wa magamba kujipendekeza, nusu ya wabunge wataingia CCM.....
   
 6. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Peoples' POWER
   
 7. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Omri ndg yangu, Hizo kauli za kukatisha tamaa zilishatoka siku nyingi ila kumbuka hata Nyerer alishatabiri tishio la CCM ni CDM tena mwaka 1995 ambapo wengi wetu tulikuwa hatuifahamu wengi walimwamini Mrema na NCCR yake, uzoefu umeshaonyesha CCM wengi kwenda CDM na sio CDM wengi kwenda CCM
   
 8. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #8
  May 9, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Good staff
   
 9. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  duh ujumbe kama wa Mtume Petro kwa Wakorintho..sura ya...mstari wa...ha wa ....!!hahaaa
   
 10. O

  Okinawa Senior Member

  #10
  May 10, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 174
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ujembe wako ni Mzuri sana ndugu kwa kuamsha waliolala.

  Muda wa UKOMBOZI ni sasa.

  People's Powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
   
 11. O

  Okinawa Senior Member

  #11
  May 10, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 174
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Zamani Mwalimu Nyerere na wazee wenzake akina Kawawa, Kambona, Mtei, Karume, Prof. Ibrahimu Babu, na wengine wengi .... walipigania Uhuru wa Taifa letu.

  Leo hii tuwaunge mkono CHADEMA katika kutafuta UKOMBOZI wa nchi yatu kutoka kwenye Uongozi wa Kifisadi na kidhalimu wa CCM (Chama Cha Mafisadi); ile wasiendelee kuuza raslimali zetu na kuendelea kuiba fedha za wavuja jasho wa Taifa hili (ambao ni wewe na mimi).

  Mkoloni wetu kwa sasa ni CCM na Mafisadi wake wote akiwemo mkuu wa kaya ambao wanatumia uongozi waliopewa ku-FISIDI nchi. Lakini siku zao sasa zinahesabika.

  Nasikia siku hizi anajuta kwa nini aligombea tena Urais bora angestaafu.

  Majuto ni Mjukuu siku zote huja baadaye .........
   
Loading...