Erwin Rommel
JF-Expert Member
- Dec 1, 2013
- 429
- 115
Suala la bei ya umeme laweza kuiondoa CCM madarakani mwaka 2015 iwapo CDM itauelezea umma kuhusu uhusiano mkubwa kati ya ufisadi ndani ya serikali ya CCM na bei ya umeme.
Na ni rahisi kabisa. Kwanza kabisa Ewura wanaendeshwa na serikali, na haipo kwa masilahi ya wananchi kwani Mkurugenzi wake ni mteule wa Rais.
Serikali inataka kuwaficha Watz kwa kujaribu kutuaminisha kwamba hasara ya mabilioni ndani ya Tanesco kwa asilimia kubwa ni hasara halali na haitokani na ufisadi, na uzembe/mapungufu ya kiutendaji ndani ya Tanesco.
Wananchi wajiulize, vipi wakati wa Mwalimu Nyerere, kiongozi huyo aliweza kujenga mabwawa matano ya uzalishaji umeme – yote mali ya Tanesco, na kuifanya Tanesco kutolazimishwa kununua umeme kutoka popote?
Lakini katika awamu zilizofuata mitambo yote iliyojengwa ya kuzalisha umeme eg IPTL na ile ya dharura (eg Songas, Richmond/Dowans/Symbion, Aggreko rtc) yote ya watu binafsi na hivyo kulazimisha Tanesco kununua umeme kutoka kwao kwa mikataba kandamizi.
Na hii mitambo lilitokana na wazo (brainchild) ya JK kuanzia awamu ya Mwinnyi wakati yeye (JK) akiiongoza Wizara ya Nishati. Hivyi ikaletwa IPTL ambapo Tanesco ililazimishwa kuingia mkataba nao, mkataba ambao hadi leo unaiumiza Tanesco na kesi kuozea mahakamani.
Mkapa awamu yake hakutaka ufisadi wa aina hii – hakuleta/kujenga mitambo yoyote ya kuzalisha umeme. Lakini alipoingia JK kule Ikulu, basi yeye na EL wake wakafufua mipango wa ki-IPTL – kwa kuanzia Richmond ambapo ufisadi ndani yake ulikuwa dhahiri kabisa pamoja na jitihada nyingi za kufunika.
Ndiyo ikafuata ile mitambo mingine ambapo yote yanailazimisha Tanesco kununua umeme kutoka kwao – mpango ambao umeiua kabisa Tanesco na kuwa katika hali iliyo nayo na sasa serikali kulazimisha mzigo wa hasara ubebeshwe wateja.
Zipo hasara zingine za kawaida kama vile upoteaji umeme wakati wa kuusafirisha kupitia miundo mbinu chakavu, au wizi wa umeme unaofanywa na wateja, ingawa hili la wizi pia unachangiwa na ufisadi wa baadhi ya maafisa wa shirika.
Lakini kuna jingine ambalo linatia hasara sana Tanesco – kuharibika mara kwa mara kwa network yao ya kuuza umeme kupitia mawakala wao eg Maxcom, Selcom etc. hazipiti siku mbili lazima network itakuwa down na kuwafanya wateja walioishiwa umeme majumbani mwao kukaa bila umeme kwa masaa kadha. Fikiria – ni wateja wangapi nchini kote, na kilowatthours milioni ngapi kila siku hazinunuliwi kutokana na sababu hii ya network inapokuwa down.
Kwa kuhitimisha tu naweza kusema hasara iliyo "halali" ya Tanesco ni asilimia 25 tu na iliyobaki – asilimia 75 – ni hasara "isiyo halali" -- yaani inayotokana na ufisadi wa watendaji wa serikali ya CCM wanaosimamia sekta ya nishati.
Ingawa sijaandika kwa mpangilio ulio bora na kutokuwa na ufasaha nawaomba Chadema wawaeleze wananchi ukweli huu kwa nini Watz wanabebeshwa mzigo wa Tanesco.