CDM itangaze kwa kuweka tarehe ya mwisho kwa kiongozi wake yoyote anayetaka kwenda CCM aende | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CDM itangaze kwa kuweka tarehe ya mwisho kwa kiongozi wake yoyote anayetaka kwenda CCM aende

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Aug 12, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wanajamvi:

  Nawashauri uongozi mkuu wa CDM utangaze wazi hivi sasa kwa kuwapa muda kwamba hadi tarehe fulani viongozi wote wanaotaka kwenda/kurudi CCM wafanye hivyo wao wenyewe, na baada ya hapo kiongozi yoyote wa CDM atakayehama basi itahesabiwa kahongwa tu na CCM. Hii nadhani ni namna bora ya kukisafisha chama.

  Ushauri wangu unatokana na swali ambalo huwa najiuliza: Kwani inakuwaje kwamba kwa CDM maandamano/mikutano yake huwa inatisha kwa nyomi?

  Na si kitu cha kubishana kwamba CCM sasa hivi haiwezi kuhamasisha maandamano na mikutano mikubwa kama ilivyokuwa zamani – hasa kwa watu kwenda kwa hiari yao bila ya vishawishi vyovyote (malori, kofia, fulana, pesa etc) ambazo chama hicho hutoa kutokana na fedha nyingi inazomiliki, au kuweza kupata kwa njia mbali mbali.

  Na katika kutaka kuonekana kujibu/kupiku hilo, CCM nao huja tu na kile kinachoripotiwa kukomba viongozi wa CDM katika maeneo fulani fulani hapa nchini, kama vile tumeshaona ripoti za Singida na Igunga.

  Kwa haraka haraka hii inaonyesha wazi kwamba katika propaganda zake za kuhimiza ufuasi, CCM hulenga zaidi watu (individuals) wachache ambao bila shaka ni rahisi zaidi kuwashawishi kwa kuwapa hongo.

  Hebu fikiria kwa mfano: Mimi naamini kabisa CDM ina uwezo wa kuhamasisha maandamano na mkutano mkubwa ambao haujapata kutokea katika historia ya sehemu hiyo huko Singida.

  Inakuaje basi viongozi wake wanakihama chama kama siyo hongo? Na kwa hapo Singida, ni rahisi kuhisi ni kigogo yupi wa CCM mwenye ushawishiu mkubwa wa kifedha anayeweza kutumia pesa kununua viongozi wa vyama vingine.


  Katika hali kama hii, yumkini mbele ya safari CCM itakuwa inajidanganya tu kwamba ina ufuasi, kwani wanachokifanya ni kuonekana wana ahueni ya muda mchache katika wimbi la hoja nzito za CDM dhidi ya chama hicho.


  Nawasilisha.

   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nakubalina nawe moja kwa moja, kwani hilo litawaput off CCM na kampeni zake za kununua wafuasi kwa pesa. Na huyo kigogo hapo Singida si mwingine bali na yule dogo mdosi Mohamed Dewji na tuliona jinsi katika uchaguzi uliopita alivyotembeza mapesa kwa yule returning officer ili amtoe mpinzani wake wa CDM katika kuwania ubunge.
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hee, hivi Lissu wet yuko salama hapo? Lakini mie namuamini sana kuwa mtu upright, asiyeyumbishwa na vijisenti vya hao wezi wa magamba.
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ni mkakati mzuri wa kukisafisha chama na kuwaziba midomo CCM. Viongozi wa CDM weafanye haraka kutangaza hivyo.

  Nakubaliana kabisa baada ya tarehe ya mwisho atakayehama basi kahongwa, kwani alishapewa chance.
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huyu dogo ni kama RA kwa kununua wapinzani. No wonder ni kwa sababu ni mahela ya chee tu.
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ni lazima CDM watangaze hivyo, la sivyo hawa CCM watakuwa wanatamba kununuwa viongozi wake kama kampeni ya propaganda. Si unaona wanavyozidiwa kete katika hoja?
   
 7. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kamchezo haka katakwisha msiwe na shaka na tanzania tunayoitaka itapatikana,hawezi mwaga pesa nchi nzima.time will tell.
   
Loading...