CDM: CCM wanavuraga amani makusudi kwanini mkutane nao faragha kuongea? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CDM: CCM wanavuraga amani makusudi kwanini mkutane nao faragha kuongea?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkwawa, Sep 29, 2011.

 1. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Chama kinapokuwa madarakani kina wajibu mkubwa mbele ya jamii, na wajibu mmojawapo ni kuhakikisha ulinzi na usalama wa watu wake na mali zao ndani ya mipika ya nchi siku zote na wakati wote. Vurugu zinazotokea Igunga zinafanywa makusudi na serikali ya CCM ili kuvipaka matope vyama vya upinzani.

  Sielewi kwanini Viongozi wa CDM wameamua kukaa na wana siasa Vijana wa CCM kuzungumzia hizo vurugu zinazofanywa na CCM bila jeshi la polisi kuchukua hatua. Tumeshuhudia polisi wakipewa na maelekezo na viongozi wa juu wa serikali pale makada wa CCM wanapo dhuru maisha ya binadamu hata kuwaumiza.

  Shigela alihusika kupigwa kwa mwanacham,a wa CUF wala hajahojiwa
  Aeshi na mwenzake walihusika kuwafyatulia risasi walinzi wa CDM- haukuhojiwa akashikiliwa Waitara
  Rage kapanda na silaha juu ya jukwaa la hadhara- kaomba msamaha Clouds FM
  Fatuma Kimario kakusanya makada wa CCM kuwandaa kuiba kura - Jela wakalala makamanda wa CDM
  Mwigulu kamwingilia kimapenzi mke wa kada mwenzake CCM ikahonga mume katulia
  CCM wamemwagia kada wao tindikali- wakaambiwa ni CDM
  CCM imemchomea kada wao nyumba kila kitu kikaungua ikabaki eti karatasi inadai CDM
  CCM wametumia lugha za uchochezi na kidini
  CCM imetumia waumini wa dini moja kuchukia vyama vingine.

  Hawa watu mnakaa nao wa nini hasa, sisi wananchi tumeshawachoka hatutaki kuwasikia wala kuendelea kutuongoza, kwanini mnawabembeleza. Siasa zibakie majukwaani. Mnawachnganya hata vijana na walinzi wa CDM wanojitoa kutetea chama na maslahi ya wananchi hata kwa uhai wao. Hawa CCM mnaowatukuza sasa, kesho wanabeba mputa mputa kwenda jela lama ninyi sio binadamu.

  Haijawahi kutokea CCM kutaka kukaa mezani kwenye uchaguzi. Mnajua nia yao ni nini au ni siasa za kujipendekeza. Hubirini na muishi mnayohubiri msituchezee viini macho.

  Mwafaka wowote na CCM ni uhaini.

  Chief Mkwawa wa Kalenga
  Uhuru ni pamoja na kumjua aliyekuweka utumwani.
   
 2. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,180
  Likes Received: 1,182
  Trophy Points: 280
  % 100 nakubaliana na wewe. Ova
   
 3. M

  Maengo JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli mkuu!
   
 4. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Kitendo cha vjana wa ccm kuwafuata viongozi wa cdm kuomba radhi kwa wanayoyafanya vjana wao wa green gard ni kukiri makosa ya vijana wao na kilichokuwa kinatakiwa ni cdm kuwarekodi hao jamaa na kupeleka ushahidi mahakamani. Hapo watakuwa wamefanya jambo la maana sana. Washtakiwe ili wapate hukumu yao.
   
 5. m

  mtolewa Senior Member

  #5
  Sep 29, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ndio mkuu.mimi mwenyewe sipendi kitu kinachoitwa eti tume ya maridhiano na ukweli au muafaka baada ya watu kuumiza wenzao makusudi.Walah naapa chadema siku ikikubali muafaka na hawa makafiri mie nitakuwa wa kwanza kupinga na hata kuihujumu.
   
 6. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni muhimu wakutanae kwa ajili ya amani ya wanaigunga,watanzania wenzetu, siasa safi ni pamoja na marithiano hasa ya kudumisha amani, vijana wa CHADEMA wasife moyo kwani chama si cha vurugu kama inavyohubiriwa,viongozi walio kwenye majadiliano ni makini,tutegemea utulivu wakati wa zoezi la upigaji kura, kutunishiana misuri hakutatui kero za igunga,wanaigunga wenyewe wana akili timamu wataaamua okt 2 na kumaliza ubishi.
   
Loading...