johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,840
- 141,766
Jenerali Mabeyo amelitaka jeshi la polisi kuhakikisha linatumia mbinu na weledi wa hali ya juu katika kupambana na uhalifu nchini.
Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Diwani Athuman amewataka askari wa jeshi la polisi kudumisha nidhamu na uadilifu wanapotekeleza majukumu yao.
IGP Sirro ameshangazwa na kitendo cha afisa msomi wa jeshi la polisi aliyevuka mpaka na kuingia nchi ya Makawi kinyume cha sheria akifukuzia mali ya magendo isiyozidi sh 30,000 huku akiwa na silaha na gari ya jeshi la polisi.
Wakuu hao wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wamesema hayo katika sherehe za kuwapandisha vyeo maafisa wa jeshi la polisi 2,030.
Source: ITV habari