CDA Mnatupa mateso ujenzi Dodoma

msemakweli2

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
1,627
1,879
Jamani naomba nitoe dukuduku langu ni mwezi karibia wa tano huu nafuatilia kibali cha ujenzi hapa CDA dodoma,ila sijafanikiwa,kiwanja changu kimepimwa,michoro imekamilika,kila documents inayotakiwa nimeambatanisha,kiwanja hakidaiwi,nimelipia na malipo kwaajili ya kibali cha ujenzi Tshs.49,500 lakini mpaka leo file halitoki,ukienda wanakwambia lipo kwa huyu,mara kwa yule mara halionekani,ni kwanini wanakuwa hivi?nawaza mimi kiwanja changu kimepimwa na kina documents zote,vp wale ambao viwanja havijapimwa?

Hivi mwenye nchi akigundua utumbo wanaoufanya hawa wataendelea kuwepo kweli? System yao ya uhifadhi wa documents ni mbaya kabisa na hawana coordination katika kazi,huyu anapitisha file,linafika kwa mwingine anaweka marekebisho,mnachelesha maendeleo ya DODOMA bila sababu ya msingi.
 
Yawezekana kweli unasumbuliwa kwa kuwa unaenda CDA ambayo kwa sasa haipo kabisa ilishafutwa, fanya mpango uende kwa Mkurugenzi wa Mji wa Dodoma.
 
Pole.mi nimefuatilia file langu miaka 2 sasa nilipie kodi ya ardhi halipatikani hivyo ninashindwa kulipia
 
sheria inaruhusu kuanza ujenzi baada ya siku 60 kama
kibali hakijatoka na umekidhi vigezo vyote. nafkiri kama nna taarifa sahihi, ndo namna jengo la tanesco ubungo lilivyojengwa kipindi icho!
 
Mshawazoesha mashati ya mikono mirefu.

Halafu hii nchi haina mwenyewe, wenyewe ndio sisi.
 
Jamani naomba nitoe dukuduku langu ni mwezi karibia wa tano huu nafuatilia kibali cha ujenzi hapa CDA dodoma,ila sijafanikiwa,kiwanja changu kimepimwa,michoro imekamilika,kila documents inayotakiwa nimeambatanisha,kiwanja hakidaiwi,nimelipia na malipo kwaajili ya kibali cha ujenzi Tshs.49,500 lakini mpaka leo file halitoki,ukienda wanakwambia lipo kwa huyu,mara kwa yule mara halionekani,ni kwanini wanakuwa hivi?nawaza mimi kiwanja changu kimepimwa na kina documents zote,vp wale ambao viwanja havijapimwa?

Hivi mwenye nchi akigundua utumbo wanaoufanya hawa wataendelea kuwepo kweli? System yao ya uhifadhi wa documents ni mbaya kabisa na hawana coordination katika kazi,huyu anapitisha file,linafika kwa mwingine anaweka marekebisho,mnachelesha maendeleo ya DODOMA bila sababu ya msingi.
Unaota wewe CDA ya wapi tena..??
 
CDA imeshafutwa,majukumu yake yanafanywa na Manispaa ya Jiji la Dodoma. Lakini nikubaliane na mtoa mada kuwa enzi za CDA niliwahi kuhangaikia kibali cha ujenzi kwa muda mrefu mpaka nikataka kutumia fedha ya ujenzi kwa mambo mengine. kuna ujasiri nilipewa na mtu kuwa nianze ujenzi kwa kuwa tayari nimekwisha wasilisha maombi yangu na malipo yote. huwezi kuamini kibali kilitoka wakati tayari nimekwisha kupaua nyumba na bahati nzuri hakukuwa na ukaguzi wowote. Siku CDA inafutwa nilifanya sherehe.
 
sheria inaruhusu kuanza ujenzi baada ya siku 60 kama
kibali hakijatoka na umekidhi vigezo vyote. nafkiri kama nna taarifa sahihi, ndo namna jengo la tanesco ubungo lilivyojengwa kipindi icho!
Bad reference, jengo hilo lilipata msukosuko sana kwa kujengwa kinyume na sheria, na hatimaye lilibomolewa bila fidia. Asifuate mkondo huo
 
Kama unaishi nyumba ya kupanga huwezi kuelewa huu uzi
yawezekana wewe ndio kwanza umetoka kupanga na ulinunua kiwanja enzi za CDA ndio maana unateseka, sie wenzio wa kongwe Dodoma kuna majumba sio kiwanja chako unachopigia kelele hapa ambapo hujiu pa kuelekea , unakuja huku unapewa ushauri una leta maneno ya kwenye kanga. basi endelea na CDA yako.
 
sawa mke nimekuelewa wife materials
 
Hiyo ofisi ya manispaa/Jiji kuna tatizo sana kwenye kuhifadhi nyaraka. Kuna mtu alinituma dodoma kufuatilia document zake, nilifuatilia miezi 6 na karibu kila wiki mbili nilikuwa nafungua faili upya kwa sababu yanapotea mara kwa mara
 
Back
Top Bottom