Cd & dvd zinazidi kukosa umuhimu na changamoto kwa wasanii wetu

Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,940
0
Nimesoma articles mbali mbali mbali zinzotabiri kuwa bidhaa inayoitwa CD& DVD storage and Drive zitakosa umuimu kwenye soko. kama ilivyokuwa Diskette. Leo hii Disk drive na diskette zimebaki kama maonyesho tu na story. Haina umuhimu

Makadirio yanaonyesha mauzo ya CD yalishuka 17% mwaka 2007 na kwa % 20 mwaka 2008 ( Refer to Is the CD Becoming Obsolete? — Reviews and News from Audioholics)

Kwa sasa makadirio haya yanaweza yasiwe sahihi kwa nchi zetu za afrika kama Tanzania sababu mara nyingi tuko nyuma ya teknolojia lakini yanaonesha muelekeo wa tuendako

Ukisoma hiyo article imetaja sababu zinazopelekea kupunguza umuhimu wa CD/DVD. kwenda mbali zaidi ni kwamba hata CD au DVD drive zitakuwa hazina maana sana hapo mbeleni kuwa kifaa cha muhimu kwennye laptop / computer.

Baadhi ya sababu zinakazofanya CD/DVD kuzidi kukosa umuhimu.


  • Technolgy ya flash sorage kama USB imechangia kwa kiasi kikubwa

  • Teknolgy ya manufacture kuweza BIOS za kompyuta kuweza ku boot na kuinstall software kutoka kwenye flash drive kama USB

  • Uwezo wa USB kuwa na storage space kubwa kuhifadhi mambo mengi kuliko CD/DVD

  • Binafsi naona Data zinakuwa salama(Security& Safety) zaidi kwenye USB kuliko zikiwa kwenye CD

  • Wakat gharama ya CD ni nafuu kuliko USB gharama ya CD/DVD Drive inaongeza gharama za kompyuta hivyo bei za kompyuta zitashuka sana bila kuwa na CD/DVD drive
  • Teknolojia ya MP3 na MP3 player za kisasa
UKisoma article niliyotaja hapo juu inaonyesha sababu nyingine Kushuka matumizi ya DVD hasa kwa wenzetu


  • Kuazima movie sio lazima mtu aende physicaly library anaweza kudownlod au kuangalia movie kwenye website aliyolipia umember
  • Kuna website mfano Amazon zinauza legal soft copy za movie/miziki/Vitabu
  • Sababu nyingine ni internet imewezesha piracy kuwa rahisi
Changamoto
Wakati wasanii wetu bado wanakazania kuuza CD nawapa changamoto washirikiane na wadau wajaribu kuuza kazi zao online pia.

Mfano watanzania walio nje hawana urahisi wa kuapata CD za wasanii wa kitanzania. kama mtanzania anataka kuchanagia kwa kununua kazi halali ya msanii afanyeje.??!!!!! Hakuna jibu zaidi ya piracy sababu ndio njia iliyo accesible.

Any Idea U have to add ,suggest, advice ,critize about my my observation ?

Karibu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom