CCM Zanzibar yasisitiza wazanzibari wasiokubali muungano uliopo warudishe kadi za chama! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Zanzibar yasisitiza wazanzibari wasiokubali muungano uliopo warudishe kadi za chama!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kupelwa, Aug 9, 2012.

 1. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 874
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 60
  Katika mojawapo ya vikao vya chama cha mapinduzi katika chaguzi zinazoendelea viswani unguja, ameonekana makamu wa pili seif iddi akiwasihi wananchama wa CCM, kuwa,"wale wasiokubali mfumo wa sera ya CCM ya kuendelea na muungano ulipo wa serikali ya muungano na mapinduzi zanzibar, warudishe na kuacha unachama wa ccm.

  Je hii katiba mpya tunayotoa maoni kutafuta na mfumo upi , inamaana wazanzibar wanasemewana CCM? Na je kupinga aina ya muungano huu ni usaliti kwa CCM?

  Na je kiongozi mkubwa kama seif iddi kuwasemea wazanzibar ni ni kuupuuza tume ya kukusanya maoni inayotaka wananchi waache wawe huru kutoa maoni yao? Hii CCM inatupeleka wapi na uahafidhina huu? AU NDO KIFO CHA CCM KIMEFIKA?

  CHANZO: TAARIFA YA HABARI SAA MBILI USIKU
   
 2. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,154
  Likes Received: 10,504
  Trophy Points: 280
  Mpaka 2015 tutaona mengi..
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mbona hilo lina mantiki? Kama mwanaccm hakubali sera ya ccm anakivua yu uanachama.
   
 4. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,347
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona unauweka u greti thinka wako rehani.

  Mimi vile vile nimesikia habari hiyo, Makamu wa Rais Zanzibar alikuwa anawajibu wale wana CCM-Uamsho wanaotaka Muungano wa Mkataba.

  Ni makosa ku quote habari bila kuielewa.
   
 5. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli nisema ukweli kutoka moyoni mwangu ya kwamba Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar ameonyesha utofauti na ubora wa kiongozi kusimamia kile kilichokuweka madarakani. Niwakumbushe wanajamii katika hili la muungano uwe wa namna gani kwa kweli viongozi wa CCM na wananchama wa CCM wana nafasi kidogo sana ya kuchagua vinginevyo. Kama Muungano ni swala la itikadi basi viongozi wa CCM walioomba uongozi na kupewa dhamana na wananchi wa Tanzania au kupewa madaraka ya uongozi kwa kuteuliwa na Rais hawana uchaguzi lazima wausemee Muungano wa sasa vinginevyo ni usaliti kwa wapiga kura au mamlaka iliyowateua.

  Na sijambo jema kutousemea na kuacha kutoa mwelekeo kichama. Kiongozi ni lazima utetee yale ambayo uliapa kuyasimamia hata kama wewe huyapendelei maadam ndio mfumo uliokuweka madarakani na ukaapa kuulinda. Kama hutaki lazima uanzishe mchakato kwa njia ya maoni ili uruhusu kura ya wengi iamue mwelekeo na kwa namna hiyo utakuwa umepewe ridhaa ya wananchi juu ya uelekeo mpya.

  Nadhani kusimamia uchungu ambao ndio msingi wa madaraka yako ni hekima kwa kiongozi yeyote. Kazi ya kiongozi si kufurahisha kikundi na wala si kuudhi bali ni kusimamia utaratibu ulioapa kuulinda. Leo nimeamini Makamu wa pili wa Rais anaweza kuaminiwa hata kwa ofisi kubwa kwa sababu ya ushupavu wa kuwa tayari kuchukiwa kwa kusimamia misingi ya makubaliano mpaka itakapoamliwa vinginevyo. Mnyonge mnyongeni lakini chake mpeni, na zake sifa apewe.
   
 6. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,347
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu, baada ya longo longo ndeefu na vurugu ya wana Uamsho, Wazanzibari wenye uchungu na hali ya wanyonge wameanz kujitokeza wazi wazi kuhesabiwa.

  Hata mimi nimefarijika kwa at least kuna watu wanaoweza kuaminika n kueleweka kiuongozi huko visiwani.

  Tamko hilo la Makamu wa pili wa Rais Zanzibar si tu linaonyesha kuwa kuna watu waliorubuniwa kuasi CCM bli vile vile kuw kuondoka kwao kunatrajiwa badl y kufukuzwa.

  Big up, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.
   
 7. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Yetu macho na masikio, bora salama.
   
 8. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 874
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 60

  Nimechagiza thread, na kuonyesha ccm imesema nini, sual la mfumo wa serikali zipi tufuate si la kichama bali ni la matakwa ya umma.hakuna katiba ya nchi ikawa ya cha cha ccm, bali ni watanzania wote bila kujali chama, nasaba, elimu, mali, dini n.k Nimechagiza kushuhudia yale ambayo jaji warioba ameelalamikia kuhusu vyama kuingilia na kutoa mitazamo yao kuhusu maoni yao.Kimsingi si vyema kutunga katiba ya chama cha mapinduzi, bali katiba ya watanzania bila kujali chama.Kuwatisha, si jambo jema na hasa kwa viongozi wakuu wa serikali.waachwe watanzania watoe maoni yao kwa uhuru tupate katiba ya watanzania.Kufanya hivyo tutatunga katiba ya kundi na haitawakislisha maoni , na matakwa ya wailo wengi.swali je kama watanzania wakapinga maoni ya ccm, ccm iko tayari kuakataa maoni ya watanzania kwenye katiba yao?je rasimali zinazotumika kupata maoni ,a kutunga katiba mpya ni za ccm au taifa kwa ujumla?jibu , zinazotokana na kodi ya walipa kodi mabo ni watanzania kwa ujumla wao bila itikadi ya ccm .kivipi kama ni hivyo kutokee kundi lianze au kiongozi wa serikali , kisa ni mwa ccm aanze kutisha watanzania kuhusu maoni yao?katiba ni watanzania wote na si yawana ccm.Kufanya hivyo, ni kumomonyoa mshikamano , umoja, na amani ya watanzania, ambayo haina itikadi, bali ni utamaduni wetu kwa ujumla
   
 9. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Kuna mwenzie alijutia kauli yake kwa kusema kuwa Hataki Kura za Wafanyakazi
   
 10. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,347
  Trophy Points: 280
  Mkuu nakubaliana kabisa na wewe katika maudhui ya mchakato mzima wa kutoa maoni ya katiba mpya.
  Hata hivyo maoni ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar s hould be read between the lines.
  Siyo siri kwa siasa za Zanzibar suala si katiba mpya tu- CCM Zanzibar kwa muda sasa imekosa msemaji mwenye nguvu.
  Kwa wanaoielewa siasa ya Zanzibar tazama sura za wanapinga Muungano na ulinganishe na wale wanaoupigania.
  Conclusions utazi draw mwenyewe.
  Kinachoongelewa hapo ni kikubwa zaidi ndani ya blanketi la maoni ya katiba mpya.
   
 11. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,946
  Likes Received: 1,505
  Trophy Points: 280
  Wakifukuzwa watamfuata Ahamed Rajabu London
   
 12. s

  saliha Member

  #12
  Aug 9, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  namie na pita kidogo kwani nimeguswa na mada hii .pongezi kwa Bw balozi Seif Iddi Makamo wa pili wa rais huo ndio ukweli kwani ingawa wananchi wakiwemo wana CCm wanauhuru wa kuchangia lakini ukiwa kiongozi uliotokana na chama CCM chenye msimamo wa kuendelea na mfumo huu na baadhi yao walikuwmo kwenye semina elekezi sijui za CCM karibuni hivi dodoma na walikuwepo na walichangia bila ya kutoa indhari kwamba wao hawamo pamoja na msimamo wa chama.

  Kwa ushujaa na kwa taratibu za siasa za vyama ni budi wenyewe bila ya kungoja kufukuzwa wa rudishe kadi na waende upande wa uamsho na wana weza pia kuwapa sura ya chama cha siasa ili wapeleke mbele agenda yao.haitokuwa vibaya wakiomba uongozi kwenye jumuia ya Uamsho kwani kila ngoma ina sheria zake za kucheza ,kuvaa sare nk .

  Ngoma hii tayari CCm imekwisha toa msimamo wake hivyo kwa wale ambao wamepata uamsho wa roho zao na uzalendo wao basi wajiunge rasmi na uamsho au jumuiya yoyote .huu ndio utaratibu wa ulimwengu ulioendelea kwa kiongozi kusimamia msimamo wake
  Sasa nataka kuzungumzia juu ya muungano wa mkataba ambao wahusika wanajaribu kuipeleka mbele sijui wanaelewa ki,lle wanachokisema.kwasababu kudai kiti cha umoja wa mataifa ni kwa nchi kamili tu wanakuwa wajumbe ila kuna mifano ya nchi ambazo bado zinatawaliwa na aidha malkia wa uingereza au serikali zengine za ulaya km uholanzi na hizo ni nchi nyingi za visiwa vya carribean na bahari ya pacific wanawakilishwa na wengine wako kama observer.pia suala la kwamba zanzibar ni nchi dogo pia hilo sio sawa kwani udogo wa nchi hauwezi kuwazuia wasiwe wanachama wa Umoja wa mataifa.

  kwa hiyo katika utaratibu uliopo kuomba kiti cha Zanzibar huko umoja wa mataifa maana yake uvunjwe muungano na Zanzibar iwe nchi kamili kwani sidhani itawezekana kuwa na uhusiano kama wa australia na malkia au canada na malkia au pia Aruba na ufalme wa uholanzi .Sasa nafikiri ndugu zetu wa uamsho walijue hilo
   
 13. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #13
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,109
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  alichosema balozi Seifu ni sahihi.Muundo wa muungano tulionao nisera ya CCm Chadema wao wanataka serikali tatu pamoja na cuf sasa kama kuna wanachama au viongozi hawaridhiki na sera ya ccm kuhusu muundo wa muungano kitu gani kinawaweka na hasa ukichukulia wengine wanashiriki vikao vya maamuzi wale wote wanaccm wanaopinga hadharani muundo wa muungano ni wanafiki kwani inawalekea walipojiunga CCM hawakujiunga kwa kupenda chama ila maslahi binafsi
  tunapozungumzia chama tunazungumzia sera na itikadi zake na wala sio mtu kama makamba alivyosema mtaji wa ccm ni kikwete matokeo yake chama chao kinapoteza umaarufu kila siku
   
 14. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #14
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,376
  Likes Received: 8,524
  Trophy Points: 280
  Makamu wa pili wa rais Zanzibar bwana Seif Iddi katoa msimamo mkali wa chama cha mapinduzi kuwa kwa mwanachama yoyote wa CCM asiyetaka muundo wa serikali mbili arudishe kadi ya cham
   
 15. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #15
  Aug 10, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Nasubiri kuwaona Masheikh wa Zanzibar wakipanga foleni kurudisha kadi
   
 16. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #16
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  kwan ni wana CCM???
   
 17. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #17
  Aug 10, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  kwa mantiki hii CCM ni chama cha kidikteta. nijuavyo mimi chama ni cha watu wote bila kubagu makundi ya aina yoyote yale. Hivyo wanachama wanaweza kubadili sera, mtazamo, itikadi nk kulingana na mapenzi ya watu wote kwa wakati husika

  walicho paswa kufanya ni kuwaita wanachama wao kisha wasikilize maoni yao. lakini si shangai ktk hili kwani mabadiliko mengi wanayafanya pasipo kuwahusisha wanachama wao

  na hili wataonekana wapo sawa tu
   
 18. M

  Mzenji73 JF-Expert Member

  #18
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  " vipi kwa wanachama wa CDM, wale wanaotaka serikali mbili ama moja warejeshe chama vile vile, kwa mantiki hiyo uisemayo?"

   
 19. d

  dandabo JF-Expert Member

  #19
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 303
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Watu kama Seif Idd ndio wanatakiwa kuiongoza Zanzibar. Hana chembe ya unafiki!
   
 20. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #20
  Aug 10, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hakika naunga mkono kauli ya makamu wa pili Seif Iddi. Hii ni kwa kuwa naamini "ndege wanao fanana ndio huruka pamoja" Kama hufanani nao, acha kusumbua, rudisha kadi yao kwa heshima zote, kajiunge na wale unaofanana nao, basi!!. Siasa za leo, sio za kubembelezana, na wala sio za unafiki. bora kubaki na wanachama wachache wenye nia moja, kuliko wanachama rundo wasio na tija. "NAPENDA KUTUMIA FURSA HII KUWASIHI WALE WOTE WENYE FIKRA PEVU, WATOKE KWA HESHIMA, WAENDE KWA WENYE FIKRA PEVU, WANAO FANANA NAO. WAKIENDELEA KUKAA HUKO, WAKUBALI KUTOTOA MAONI KWA KUWA HAWARUHUSIWI KUWA NA MAONI YAO, BALI YA CHAMA"
   
Loading...