CCM Zanzibar Yamuogopa Maalim Seif. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Zanzibar Yamuogopa Maalim Seif.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Aug 10, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeitolea wito Serikali zote mbili na jumuiya za kimataifa kuanza kumtazama kwa maakini Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad kama ni tishio jipya la uvurugaji wa ustawi wa amani katika nchi za Maziwa Makuu.

  Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Itikadi na Uenezi CCM Vuai Ali Vuai ametoa tamko hilo leo katika mkutano wake na waandishi wa habari uliuofanyika katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui mjini Unguja.

  Vuai alisema Maalim Seif ndiye anayechochea wafuasi wake wafanye fujo huko Pemba na kuvunja sheria huku akiwalazimisha waandikishwe wakiwa hawana vitambulisho vya ukaazi wa miaka mitatu vinavyotolewa chini ya sheria Namb 7/2005 ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
  Alisema kuwa bila shaka ana agenda ya mpya tete iliyojificha ikiwa dhamira mbaya ya kudumaza misingi ya demokrasia ili isifuate mkondo wake Zanzibar.
  Alisema kiongozi yeyote anayetoa matamshi yasiyo na tahadhari yenye kuchochea ili kuharibu misingi ya amani kunakoambatana na ukiukaji wa katiba na sheria ni tishio kwa usalama na amani ya nchi na mustakabali wake.
  “CCM tunaziomba serikali mbili za SMT na SMZ kuzifuatilia kwa karibu kauli za Maalim Seif,lakini pia tunaitolea wito jumuiya ya kimataifa,mabalozi wanaowakilisha nchi zao Tanzania na Tasisis za kimataifa kumtahadhari kiongozi huyu kama ni tishio jipya”

  Katibu huyo wa Kamati Maalum ya NEC CCM Itikadi na Uenezi Zanzibar alieleza kuwa maraekebisho ya Katiba ya nane na tisa yaliofanywa mwaka 2002 kwa sehemu kubwa yalitokana na mapendekezo ya Tume ya Rais ya Pamoja ya Usimamizi na Uteklezaji wa Muafaka wa Oktoba 10,2001 ambapo sheria yake ndiyo inayotumika sasa chini ya Tume ya Uchaguzi -ZEC- ikiwemo suala zima la Daftari la kudumu la wapiga kura.

  “Chini ya sheria hiyo muda wa ukaazi katika jimbo ulipunguzwa kutoka miaka mitano hadi mitatu ili kuwezesha kila mmoja kupata haki ya kuwa mpiga kura,CUF ndiyo waliokuwa wapiga chapuo ya hoja hiyo lakini leo wao ndiyo walalamishi wakuu”Alisema Vuai.

  Aidha kwa mujibu wa Katiba kifungu cha 7 (2) cha Katiba sehemu (b) kinasema kila mtu awe ameonyesha kitambulisho chake cha ukaazi kilichotolewa chini ya sheria No 7/2005 na sehemu ya (2) inasema hakuna mtu atakayeandikishwa kuwa mpiga kura katika zaidi ya jimbo moja la uchaguzi au katika zaidi ya eneo moja katika jimbo na sehemu (3)(i) kinabainisha kuwa mtu yeyote ambaye ni mkaazi wa kawaida wa jimbo linalohusika ataandikishwa kuwa mpiga kura wa jimbo hilo.

  Hata hivyo Vuai alisema kuwa kinachofanyika sasa ni utekekezaji wa sheria hiyo ambapo masheha na maafisa husika wa ZEC katika majimbo wanasimamia sheria hiyo iliyopitishwa na BLW huku akinukuu sheria ya uchgaguzi ya mwaka 2004 kifungu cha 12(a)(b) kinachosema mtu hawezi kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura bila ya kuwa na kitambulisho cha ukaazi cha mzanzibari......

  SOURCE:ZANZIBAR YETU WEB BLOG.
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Na ndiyo maana(CCM) wakapandikiza mabovu yao ya "kariakoo" kule Pemba wapate la kupayukia, wamevuna mabuwa kwa kumchekea nyani, mbinu zao zimegundulikana, hawana mpya, wamebaki sasa kuomba msaada kwa mabazungu, wakubali tu bila ya hila na ubabe "Mwenye ndevu" hawamuwezi.
   
Loading...