CCM Zanzibar sasa washiriki maandamano ya CUF


Kubwajinga

Kubwajinga

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2008
Messages
2,190
Likes
22
Points
135
Kubwajinga

Kubwajinga

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2008
2,190 22 135
CCM Zanzibar sasa washiriki maandamano ya CUF

Maelfu ya wafuasi wa chama cha CUF na CCM Zanzibar wakijumuika katika maandamano ya kuunga mkono kauli ya katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad ya kutaka uchaguzi mkuu visiwani humo usogezwe mbele, Maandamano hayo yalianza katika uwanja wa Maisara na kuishia kiwanja cha Demokrasia Kibanda Maiti jana.


*Seif asema Wazanzibari waachiwe Zanzibar yao

Salma Said, Zanzibar

CHAMA cha Wananchi(CUF) jana kilifanya maandamano makubwa yaliyowashirikisha wanachama wa CCM mjini Zanzibar, kuunga mkono maridhiano yaliyofikiwa kati ya Rais wa Serikali ya Mapindizi (SMZ), Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad Novemba 5, mwaka jana.

Maandamano hayo yalianza saa 2:00 asubuhi katika Viwanja vya Maisara na kuishia Uwanja wa Demokrasia Kibanda Maiti Mkoa wa Mjini Magharibi, yalipambwa na rangi za bendera za vyama vya CCM na CUF pamoja na picha za Maalim Seif na Rais Karume.

Katika maandamano hayo baadhi ya wanachama wa vyama hivyo walibeba mabango yenye ujumbe mbalimbali mengine yakisomeka "Ahsante Rais Karume, ahsante Maalim Seif, tumesamehe na tutasahau, kwa maslahi ya wazanzibari tupo tayari kwa lolote, asiyeitakia mema Zanzibar ni hasidi wa Wazanzibari."

Mengine yalikuwa na ujumbe uliosema: "Kujiamulia sio kuamuliwa, maslahi ya Zanzibar ni makubwa kuliko chama, Zanzibar ni moja ya Waunguja na Wapemba, Zanzibar ipo juu ya CCM na CUF, kuungana sio kutengana, hatima ya Wazanzibari itaamuliwa na Wazanzibari wenyewe zama za giza zimekwisha tukishirikiana, pasipo na mapenzi hakuna maendeleo na viongozi tusipoteze nafasi ya kuwaunganisha Wazanzibari."

Vile vile, ngoma ya mpwaka choka (beni) ya wana CCM kutoka Miembeni na Jang'ombe Mitaa yenye wanachama wengi wa CCM ilichangamsha maandamano hayo. Hii ni mara ya kwanza kwa wana CCM kushiriki maandamano ya CUF tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi nchini.

Kabla ya maridhiano hayo, wafuasi wa vyama hivyo walikuwa wakiishi kwa uhasama na mara nyingi zilitokea vurugu baina yao zilizoambatana na umwagaji damu.

Mbali ya ngoma hiyo, zumari likiongozwa na Kikundi cha Mji Mkongwe ambako ndio ngome kubwa ya CUF, walipita huku wakionesha manjonjo yao kwa Maalim Seif na wimbo wao maarufu wa 'Yaa Habibi Seif'.

Wimbo maalumu wa taarabu uliotungwa hivi karibuni kwa ajili ya maridhiano ulioimbwa na Mzanzibari Abdallah Issa (Super Star) nao uliibua shangwe kubwa kutoka kwa maelfu ya watu waliohudhuria maadamano hayo.

Kufanyika kwa maandamano hayo kumetokana na kongamano lililofanywa juzi la CUF ili kujadili mustakabali wa hali ya kisiasa na kujenga Zanzibar mpya yenye maridhiano.

Nguvu ya mshikamano visiwani humo tangu kufikiwa kwa maridhiano ya viongozi hao wawili, ilionekana pia Ijumaa wiki hii katika sala ya pamoja ambapo mamia ya Wazanzibar walijitokeza kutoka vyama vyote.

Akisoma risala ya mikoa mitatu ya Unguja, katika maandamano hayo, Mohammed Kombo alisema maridhiano yaliyofikiwa yanaweza kutoa suluhisho la viongozi kuliko uchaguzi ambao wanaamini umechafuliwa.

"Aliyeanzisha maridhiano ndio aendelee nayo, asipewe mtu mwingine kwani anaweza kuacha njiani au kuyaharibu kwa makusudi kwa lengo la kuwaacha Wazanzibari katika giza kama miaka ya nyuma," alisema Kombo.

Akizungumza katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif alisema yeye na Rais Karume hawatarudi nyuma katika kuwaangusha Wazanzibari kwa kuwa wana nia safi juu ya suala hilo na kwamba, Wazanzibari wamejenga matumaini makubwa kwao.

"Mimi ni CUF kindakindaki na mheshimiwa Karume ni CCM kindakindaki; lakini tumeamua kufanya maridhiano kwa maslahi ya Wazanzibari na haturudi nyuma," alisema Maalim Seif. Alisema kutokana na maridhiano hayo kumekuwepo na mbinu za watu fulani aliowaita wasioitakia mema Zanzibar ambao wanataka kutumia nafasi ya kuwagawa Wazanzibari kwa vyama vyao vya siasa, jambo ambalo alisema halitawezakana na kuwataka wananchi hao wakatae kugawanywa kwa kuwa wametoka mbali katika misukosuko ya kisiasa.

Alisema kwa kuwa Rais Karume ndiye muasisi wa maridhiano anapaswa kuendelea nayo kwa hali yoyote na asijaribu kumuachia mtu mwengine ambaye anaweza kuyaharibu njiani kwa maslahi yake na kuongeza kwamba, Rais Karume akubali maombi ya Wazanzibari.

"Rais Karume ndiye uliyeanzisha maridhiano haya, tena unataka tumpe mtoto nani? Tumpe mwanga? Atamuua…sisi wenyewe tunapaswa kumlea mtoto huyu, hatuwezi kuwapa hawa watu wenye kutia tia maneno; eti wanataka urais.

Hapana ni sawa na wanga watamuua…rekebisha katiba tupate kumlea mtoto wetu," alisema Maalim.

Seif alisema kutokana na maridhiano hayo Watanzania wote kwa ujumla wangefurahi na kuunga mkono kama alivyoonyesha Rais Kikwete.

Alisema ameshangazwa na watu wenye kutilia shaka na kuanza kuleta chokochoko za kutaka kuwagawa Wazanzibari.

"Namshukuru Rais Kikwete, amefahamu na ametuunga mkono na ameahidi kuwa atatumia njia zote kutusaidia katika kuyaunga mkono maridhiano haya.

Mimi nawashangaa hawa wengine ambao wameanza maneno, mimi nilidhani watu wenye akili wote watayaunga mkono; lakini bahati mbaya wanatumia vyama kutaka kutugawa tena, tusikubali kurudi huko tulipotoka jamani," alisisitiza Maalim Seif.

Baadhi ya wanasiasa wakiwamo wasomi kutoka Tanzania bara wameibuka kupinga mapendekezo ya Rais Karume kuongezewa muda yaliyotolewa wiki hii na Maalim Seif.

Juzi Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alionyesha wasiwasi kuhusu mshikamano unaozidi kukua kati ya Maalim Seif na Rais Karume na akayaponda mapendekezo kumwongezea muda rais wa Zanzibar.

Pia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati alipinga mapendekezo hayo na kusema rais anayekuja ataendeleza maridhiano yao.

Maalim Seif aliwaomba wananchi kuunga mkono kusogezwa mbele uchaguzi wa Zanzibar ili kuweka mazingira mazuri ya kuingia katika uchaguzi katika hali ya amani na maridhiano hasa kwa kuzingatia chaguzi zote zinazofanyika huwa zinakumbwa na malalamiko na misuguano isiyo ya lazima ambayo matokeo yake husababisha chuki, uhasama na mauaji. "Uchaguzi ni sumu ya umoja wa Wazanzibari, uchaguzi ni farka ya kutufarakanisha na yeyote anayetaka uchaguzi sasa hatutakii mema anataka kutuua tunakwenda katika uchaguzi tunapigana, tunauana hiyo ni kwa faida ya nani? Hapana tunataka tukifanya uchaguzi uwe safi" alisema Maalim.
 
PJ

PJ

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Messages
297
Likes
2
Points
35
PJ

PJ

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2007
297 2 35
Sasa hivi wanachotaka wazanzibari sio siasa za chama bali utaifa wao.

Kwa mtaji huu kama ccm watalala watajikuta wanachama wao wanaungana na wa cuf kudai haki ya utaifa wao na kuingoa ccm kirahisi tu
 
Mr. Zero

Mr. Zero

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2007
Messages
10,620
Likes
4,012
Points
280
Mr. Zero

Mr. Zero

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2007
10,620 4,012 280
Sasa hivi wanachotaka wazanzibari sio siasa za chama bali utaifa wao.

Kwa mtaji huu kama ccm watalala watajikuta wanachama wao wanaungana na wa cuf kudai haki ya utaifa wao na kuingoa ccm kirahisi tu
Imetoka hiyo!! I think ni too late kwa CCM kufanya lolote na ukichukulia udhaifu wa serikali ya sasa hakuna kitu kitafanyika. Cha kuombea mambo yabaki kuwa under control ili yasije yakaharibu muungano. Kama CCM bara wataleta ubabe wao nafikiri itakuwa mwanzo wa mwisho wa muungano!!!
 
MrFroasty

MrFroasty

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2009
Messages
741
Likes
47
Points
45
MrFroasty

MrFroasty

JF-Expert Member
Joined Jun 23, 2009
741 47 45
Everything has an end, so is the union :rolleyes:
 
Lekanjobe Kubinika

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2006
Messages
3,065
Likes
31
Points
135
Lekanjobe Kubinika

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Joined Dec 6, 2006
3,065 31 135
Sasa hivi wanachotaka wazanzibari sio siasa za chama bali utaifa wao.

Kwa mtaji huu kama ccm watalala watajikuta wanachama wao wanaungana na wa cuf kudai haki ya utaifa wao na kuingoa ccm kirahisi tu
Ofcourse inaeleweka hata na CCM wenyewe kwamba siku zote CUF walikuwa wanashinda ila ubabe ndio pekee uliowabakisha madarakani siku zote. Sasa unadhani maalim ni mjinga kushabikia kitu kisichokuwa na tija? Hawajasema wazi walikubaliana nini, Karume anacheza karata ya mtaji wa ziada na hesabu imetick. Wenye kulalama na walalame waachwe solemba.

Hilo suala la muungano kama mtu wa bara bado sijaona nanufaika vipi, watu wa visiwani ndio wananufaika zaidi ingawa wanapiga kelele za maudhi.Wanakuja huku na kutwaa hekari maelfu hatuwasemi Mbara ukienda kisiwani hata hatua mbili kupata utangulie kufa kwanza. Wanasiasa wa bara labda ndio waanufaikana sio mwananchi wa kawaida. Tunacholilia hapa ni kwamba vurugu zao zinaharibu jina zima la Tanzania. Kama sivyo tungewaacha na mambo yao kama tulivyowaacha Rwanda na Burundi tuwapokee kama wakimbizi tu.

Zanzibar wanahitaji kuonyesha seriousness yao kupatana kama ndugu. JK hawezi kuwalazimisha kupatana kama wao wenyewe hawaqtaki. Hata kule nako wanaoumia ni watu wa kawaida tu, wanasiasa wana njia za kuwa salama. Familia zao wengi ziko bara kwenye mashamba na majumba ya kifahari lakini wanakataa muafaka.

Tujifunze uungwana ni kukosa na kupata kwa wakati wake na tusilazimishe mambo.


Leka
 
Kubwajinga

Kubwajinga

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2008
Messages
2,190
Likes
22
Points
135
Kubwajinga

Kubwajinga

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2008
2,190 22 135
Sasa hivi wanachotaka wazanzibari sio siasa za chama bali utaifa wao.

Kwa mtaji huu kama ccm watalala watajikuta wanachama wao wanaungana na wa cuf kudai haki ya utaifa wao na kuingoa ccm kirahisi tu
Hili la Maalim Seif kutaka Karume aendelee linashangaza na kuleta maswali mengi.
  1. Kwani walichokuwa wanapigania CUF ni Demokrasia au maelewano na CCM?
  2. Karume akibadilisha katiba kama Maalim Seif anavyotaka, je atabaki kwenye uraisi bila kupigiwa kura?
    [*]Ni nini hicho anachotakiwa Karume kukilinda kwa kuendelea kutawala?
  3. Kwa nini Maalim Seif anawaburuza Wazanzibari kuvunja katiba yao kwa makubaliano aliyofikia yeye Maalim Seif chumbani na Karume peke yao?
  4. Maalim Seif anajua kabisa kuwa baada ya kushindwa mara kibao, iwe ni kihalali au la, Wazanzibari tayari wameshachoshwa na siasa zake. Sasa hii move ya kujipendekeza kwa Karume ni kwa maslahi yake binafsi au ya Demokrasia?
 
Joss

Joss

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2009
Messages
729
Likes
1
Points
35
Joss

Joss

JF-Expert Member
Joined May 28, 2009
729 1 35
Wazanzibari walipigana vita ya mapinduzi wakiwa wamoja,walimuamini Karume Senior,Imefikia wakati wa Karume Jr. Kusimama upande wa Wazanzibari bila kujali itikadi yake ya chama,huko kutakuwa ni kumuuenzi baba yake.Kuna haja gani ya kukimbilia uchaguzi kama hali ya mambo si shwari?
Na kama ccm watang'ang'ania hivyo basi wanachama wao wengi wa Zanz. watachagua cuf..,na wakijaribu kuiba kura,yatatokea machafuko ambayo hayajawahi kutokea katika chaguzi yoyote iliyopita.
By the way huku bara viongozi wamekalia ufisadi,wawaache wenzao waliofunguka macho wachanje mbuga...,Hata wa zenji wamechoshwa kuwa chini ya viongozi mafisadi,hata wakitaka kujitenga sawa tu,muungano umewanyima nafasi nyingi za kimataifa.
Kama viongozi wa muungano,hususani bara wanaona zanz. ni muhimu kwa usalama wa Taifa,basi waheshimu mawazo yao na kufanya mambo kwa majadiliano na si kutumia mabavu.ndo njia pekee ya kusevu.....
 
Mdau

Mdau

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2008
Messages
1,781
Likes
267
Points
180
Mdau

Mdau

JF-Expert Member
Joined Mar 29, 2008
1,781 267 180
politicians are Devils..........maskini Wazanzibari,hawajui washangilialo!!
 
Pundamilia07

Pundamilia07

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2007
Messages
1,433
Likes
12
Points
135
Pundamilia07

Pundamilia07

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2007
1,433 12 135
Zanzibar ni zaidi ya Karume na Seif Hamad.
Kitendo cha Seif kung'ang'ania kuendelea urasi wa Karume ilhali Karume ametamka kuwa hataki kuendelea na kipindi kingine ni kitendo kinacho waacha wengi wakiwa na maswali machanganyiko. Seif kama kiongozi wa mhimili mkubwa wa siasa za Zanzibar anaonekana kuhubiri maslahi ya Zanzibar nje ya utawala wa sheria. Anahubiri maslahi ya Zanzibar kwa kigezo cha ubinafsi wake yeye mwenyewe na Karume kwa upande mwingine.
Ni vema basi Rais Karume aendelee kutoa msisitizo kwenye jambo hili kabka halijaoteshwa mizizi na kupata tafsiri mbaya.
 
MwanaFalsafa1

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
5,566
Likes
39
Points
135
MwanaFalsafa1

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
5,566 39 135
"CHAMA cha Wananchi(CUF) jana kilifanya maandamano makubwa yaliyowashirikisha wanachama wa CCM mjini Zanzibar, kuunga mkono maridhiano yaliyofikiwa kati ya Rais wa Serikali ya Mapindizi (SMZ), Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad Novemba 5, mwaka jana."

Mimi nina swali kadogo kwa hawa wafwasi wa CUF na CCM Z'bar. Wanaunga maridhiano yapi na wakati hayaja wekwa wazi? Mh wasije kushangazwa na baadhi ya vipengele pindi vitakapo kuja kuwekwa wazi. Anyway good luck to the people of Zanzibar.
 
N

Nyauba

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2008
Messages
1,098
Likes
12
Points
135
N

Nyauba

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2008
1,098 12 135
safi Seif na Karumee..nawaunga mkono na msirudi nyuma katika nia yenu hiyoo NJEMA.

Zanzibar ni zaidi ya CCM na CUF na pia ni zaidi ya Seif na Karume..

Good move...go go
 
MrFroasty

MrFroasty

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2009
Messages
741
Likes
47
Points
45
MrFroasty

MrFroasty

JF-Expert Member
Joined Jun 23, 2009
741 47 45
politicians are Devils..........maskini Wazanzibari,hawajui washangilialo!!
Sisi wazanzibari wenyewe tumekaa tulii....hatuna haraka ya kujua yaliyoko jikoni, tunasubiri hadi chakula kije mezani.

Sasa hii ngoma haswa itaanza kuchezwa vizuri mwaka huu hadi ijulikane kama jikoni kutatoka ubwabwa mweupe au mseto.

Na wewe utasikia harufu tuu, hupati kitu :D
 
Kubwajinga

Kubwajinga

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2008
Messages
2,190
Likes
22
Points
135
Kubwajinga

Kubwajinga

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2008
2,190 22 135
Kitendo cha Seif kung'ang'ania kuendelea urasi wa Karume ilhali Karume ametamka kuwa hataki kuendelea na kipindi kingine ni kitendo kinacho waacha wengi wakiwa na maswali machanganyiko.
Inashangaza kuona Maalim Seif ndie anayeandaa maandamano kushangilia waliyokubaliana kisirisiri.

What is he gaining out of this?
 
S

Stone Town

Senior Member
Joined
May 28, 2007
Messages
108
Likes
2
Points
35
S

Stone Town

Senior Member
Joined May 28, 2007
108 2 35
Asalamau alaykum.

Habari za siku nyingi naona maneno mengi yanasemwa kuhusiana na suala la karume kuongezewa muda kila mmoja anasema vyake mimi nadhani watu kama wamemsikia katika hutuba yake ambayo imerushwa live na baadhi ya vyombo vya habari vya televisheni na radio na mimi binafsi nilikuwepo pale katika uwanja wa gombani karume hajasema kama hataki alichosema kwamba ameanza katika kipindi chake cha uongozi na ameingia katika kipindi cha pili na sasa anamalizia na katiba haimruhusu kuingia kipindi cha tatu. na hilo ndilo walilolisema watu ambao wanataka aendelee wanasema kwamba muda wake unamalizika na hakuna kipindi cha tatu lakini wanamuomba aongezewe muda ili aingie katika kipindi cha tatu suala la yeye kutaka au wazanzibari kutaka hilo ndio suali lakini yeye hakuna sehemu hata moja katika hutuba aliposema mimi sitaki kama ilivyoandikwa katika magazeti.

kuingia katika uchaguzi kwa zanzibar sasa ni hatari kubwa sana kama alivyoeleza mmoja wa wachangiaji, ikiwa andikishaji hali ilikuwa ya kuchomeana nyuma kupigana na mambo kama hayo jee uchaguzi ambao asilimia kubwa ya CUF hawajaandikishwa katika daftari?

wala watu wasiwe na fikra za kuwa wazanzibari wakiungana kuna hatari katika muungano no hiyo sio sahihi suala la muungano lipo na litaendele kuwepo maana hakuna mwenye ndoto hiyo ya kuvunja muungano ila mambo makubwa ni kutafutiwa ufumbuzi wa kero za muungano.

wazanzibari kwa miaka kadhaa walikuwa wanatafuta suala la kuunganishwa kuwa wamoja hivi sasa njia imepatikana nadhani ni fursa nzuri ya kuendelea na maridhiano masuala mengine yote ni madogo sana kwani hakuna kisichowezekana ikiwa dhamira ya kweli ipo suala la katiba watu wanavyolizungumza kama kwamba n kufuru kubwa lakini wanasahau kuwa tanzania inatajwa vibaya kutokana na machafuko yanayotokea zanzibar jee tuendelee kuuwana kwa kisingizio cha kulinda katiba? katiba ni nini mbele ya uhai wa watu? katiba ni nini mbele ya umoja? katiba ni nini mbele ya heshima na utu wa binaadamu? nadhani tufikiri kwanza kabla ya kuzungumza.

katiba imetengenezwa na mtu kwa maslahi ya watu na ikiwa katiba iliyopo kuna vifungu ambavyo ni kikwazo vinaweza kufanyika marekebisho ili kukidhi haja ya wakati husika katiba sio msahafu kuwa hauwezi kuchezewa.

hatupendi kubadilisha katiba lakini kama kuna haja ya kufnaya hivyo wacha ibadilishwe ili hali ya amani iwepo na tuishi kwa amani atutaki uchaguzi wenye gharama ambao utasababisha vifo, majeruhi na mali kupotea bora kubadilisha katiba kuliko kuingia katika gharama hizo.

usiku mwema

ndio mimi mzanzibari wa stone town
 
255Texter

255Texter

Senior Member
Joined
Aug 31, 2007
Messages
150
Likes
1
Points
33
255Texter

255Texter

Senior Member
Joined Aug 31, 2007
150 1 33
Mimi kama mTanganyika, m-bara halisia, ninawaunga mkono hawa wanasiasa waliofilisika wa Zanzibar na ningependa kuona wanatimiza lengo lao la kuuvunja muungano. Kwa hakika mimi M-bara wa Tabora sioni manufaa yoyote ya huu muungano. Sababu ztulizoambiwa siku zote na wanasiasa wetu kwamba WaZanzibar ni ndugu zetu na kwamba muungano ni kwa ajili ya usalama, nadhani sababu hizo sasa zimefulia. Kama ni undugu, basi Tanzania ingeungana na Malawi kwa sababu watu wa kusini(Ruvuma, Mbeya) wana-undugu pia na watu wa Malawi. Au kuungana na Uganda na Rwanda kwa sababu Wahaya wanaujamaa na Baganda na Watutsi wa Rwanda na Burundi.

Kuhusu usalama, hivi kweli kama tukiwa serious na kuimarisha Navy ya Bongo, hawa wapemba watatusumbua vipi? How can we as WaTanganyika, be scared of 600,000 lazy-to-the-bones and ngoma obsessed people of Zanzibar?

Tuvunje huu Muungano na Tuuvunje sasa! Rev. Mtikila yupo wapi?
 
MrFroasty

MrFroasty

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2009
Messages
741
Likes
47
Points
45
MrFroasty

MrFroasty

JF-Expert Member
Joined Jun 23, 2009
741 47 45
Mimi kama mTanganyika, m-bara halisia, ninawaunga mkono hawa wanasiasa waliofilisika wa Zanzibar na ningependa kuona wanatimiza lengo lao la kuuvunja muungano. Kwa hakika mimi M-bara wa Tabora sioni manufaa yoyote ya huu muungano. Sababu ztulizoambiwa siku zote na wanasiasa wetu kwamba WaZanzibar ni ndugu zetu na kwamba muungano ni kwa ajili ya usalama, nadhani sababu hizo sasa zimefulia. Kama ni undugu, basi Tanzania ingeungana na Malawi kwa sababu watu wa kusini(Ruvuma, Mbeya) wana-undugu pia na watu wa Malawi. Au kuungana na Uganda na Rwanda kwa sababu Wahaya wanaujamaa na Baganda na Watutsi wa Rwanda na Burundi.

Kuhusu usalama, hivi kweli kama tukiwa serious na kuimarisha Navy ya Bongo, hawa wapemba watatusumbua vipi? How can we as WaTanganyika, be scared of 600,000 lazy-to-the-bones and ngoma obsessed people of Zanzibar?

Tuvunje huu Muungano na Tuuvunje sasa! Rev. Mtikila yupo wapi?
Kwanza shukurani kwa kututukana sie wazanzibari.
Pili, jiulize ni mara ngapi wazanzibari wakiongozwa na viongozi wao wameshajaribu kuvunja, halafu ndio uje na hoja zako za kimizengwe.

Kwa ufupi mimi pia kama mzanzibari naomba dua kila ninaposali manaake X5 a day muungano uvunjike!Sitaki hata kusikia kuwa ati mimi uraia wangu umekuwa sasa na mmasai au mmakonde wa huko Tabora.

Kwa hiyo be my guess tieni pressure huko kwenu muvunje, halafu musikie kama SMZ itapinga wazo la kuvunja muungano.

Huu muungano ni mawazo ya Nyerere ambae ndie alikuwa kiongozi wenu, sasa sioni sababu ya kututukana.Bwana huyo ambae munamuenzi kwa mawazo yake yaliyochoka na yenye ujamaa mwingi, alitumia kila rasili mali yenu kuhakikisha kuwa Zanzibar inalazimishwa kuwa chini ya muungano wa Tanzania.

Sasa lawama zote tupa huko Butiama, sijuwi hata kama hahusiki babu huyu na kifo cha Karume hapo 1972.

Go ahead na vunja, sisi huku visiwani hatutaki miungano na wamasai :D
 
J

JUZAMO

Member
Joined
Apr 12, 2009
Messages
41
Likes
0
Points
0
J

JUZAMO

Member
Joined Apr 12, 2009
41 0 0
politicians are Devils..........maskini Wazanzibari,hawajui washangilialo!!
Nakusikitikia sana mpaka leo unamawazo finyu na mafupi kiasi hichi Wazanzibari ni waelewa kuliko yoyote Africa kumbuka ndio ambao wamekufungua macho wewe na wazee wako mafika sehemu angalau mnaweza kutamka neno fisadi bila ya kuogopa vitisho POLE SAMAKI WEWE!@
 

Forum statistics

Threads 1,250,853
Members 481,494
Posts 29,747,788