CCM yazoa viti vingi vya udiwani

KIBE

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
943
184
Chaguzi ndogo za udiwani zilizofanyika sehemu mbalimbali ziligubikwa na vurugu wakati hali ilikuwa mbaya zaidi huko Makuyuni mkoani Arusha ambako Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari alipigwa na wafuasia wa CCM na kulazimika kulazwa hospitalini.
Pamoja na vurugu hizo, CCM iliendelea kudhihirisha umwamba wake katika ulingo wa siasa baada ya kujizolea viti vingi vya udiwani wakati wa chaguzi ndogo zilizofanyika sehemu mbalimbali nchini.
Wafuatiliaji wa mambo ya kisiasa walikuwa wanafuatilia kwa kina chaguzi hizo ili kupima joto la kisiasa nchini.
Uchaguzi uliokuwa unasubiriwa kwa hamu ni ule wa Makuyuni wilayani Monduli ambako Mbunge wake ni mwanasiasa maarufu Edward Lowassa.
CCM iliibuka kidedea huko Makuyuni na kufanya maneno ya Rais Jakaya Kikwete kuwa Lowassa ana misuli ya kuifanya CCM ishinde huko Monduli.
Lowassa alikuwa na kibarua cha kukabiliana na Chadema waliokuwa wanataka kujipenyeza Monduli ambako hawajahi kuwa na kata tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe.
Hata hivyo, bado CCM haijapata dawa ya ushindi Pemba kwani kilishindwa vibaya na CUF kwenye uchaguzi wa ubunge wa Chambani.
Chadema kwa upande wake kilitoa changamoto kwa CCM katika chaguzi hizo za kata na hata kujizolea kata mbili za Iyela huko Mbeya na wilayani Hanan’g huko mkoani Manyara.
Nassari apata kichapo Makuyuni
Nassari alivamiwa, kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali mwilini na watu wanaodaiwa kuwa viongozi na wafuasi wa CCM, akiwa katika harakati za uratibu wa shughuli za upigaji kura za udiwani katika Kata ya Makuyuni, wilayani Monduli.
Nassari aliyekuwa wakala mkuu wa Chadema katika kata hiyo alivamiwa na kundi la watu zaidi ya 30 waliomshambulia kwa fimbo na
Tukio hilo lilitokea jana kati ya Saa 3:00 na 4:00 katika kituo cha kupigia kura cha Kwa Zaburi wakati mbunge huyo alipofika kuangalia maendeleo ya zoezi la kura.
Source:mwananchi 17 juni 2013
 
Huyu mwandishi mnazi wa kutipa hivi CDM inanyakua kata mbili tu? Mbona kuna Ifakara, Sengerema Sindiga hajazisema??? Huu ndiyo ukanjanja.
 
[COLOR=#333333 said:
Tukio hilo lilitokea jana kati ya Saa 3:00 na 4:00 katika kituo cha kupigia kura cha Kwa Zaburi wakati mbunge huyo alipofika kuangalia maendeleo ya zoezi la kura.[/COLOR]
Source:mwananchi 17 juni 2013

Am au Pm huo muda ulioandika bado sijatambua ni saa ngapi
 
Ikikuwa ngoma iwe droo ni vile wametupiga na vitu vyenye mlipuko huko arusha......
 
Chaguzi ndogo za udiwani zilizofanyika sehemu mbalimbali ziligubikwa na vurugu wakati hali ilikuwa mbaya zaidi huko Makuyuni mkoani Arusha ambako Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari alipigwa na wafuasia wa CCM na kulazimika kulazwa hospitalini.
Pamoja na vurugu hizo, CCM iliendelea kudhihirisha umwamba wake katika ulingo wa siasa baada ya kujizolea viti vingi vya udiwani wakati wa chaguzi ndogo zilizofanyika sehemu mbalimbali nchini.
Wafuatiliaji wa mambo ya kisiasa walikuwa wanafuatilia kwa kina chaguzi hizo ili kupima joto la kisiasa nchini.
Uchaguzi uliokuwa unasubiriwa kwa hamu ni ule wa Makuyuni wilayani Monduli ambako Mbunge wake ni mwanasiasa maarufu Edward Lowassa.
CCM iliibuka kidedea huko Makuyuni na kufanya maneno ya Rais Jakaya Kikwete kuwa Lowassa ana misuli ya kuifanya CCM ishinde huko Monduli.
Lowassa alikuwa na kibarua cha kukabiliana na Chadema waliokuwa wanataka kujipenyeza Monduli ambako hawajahi kuwa na kata tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe.
Hata hivyo, bado CCM haijapata dawa ya ushindi Pemba kwani kilishindwa vibaya na CUF kwenye uchaguzi wa ubunge wa Chambani.
Chadema kwa upande wake kilitoa changamoto kwa CCM katika chaguzi hizo za kata na hata kujizolea kata mbili za Iyela huko Mbeya na wilayani Hanan’g huko mkoani Manyara.
Nassari apata kichapo Makuyuni
Nassari alivamiwa, kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali mwilini na watu wanaodaiwa kuwa viongozi na wafuasi wa CCM, akiwa katika harakati za uratibu wa shughuli za upigaji kura za udiwani katika Kata ya Makuyuni, wilayani Monduli.
Nassari aliyekuwa wakala mkuu wa Chadema katika kata hiyo alivamiwa na kundi la watu zaidi ya 30 waliomshambulia kwa fimbo na
Tukio hilo lilitokea jana kati ya Saa 3:00 na 4:00 katika kituo cha kupigia kura cha Kwa Zaburi wakati mbunge huyo alipofika kuangalia maendeleo ya zoezi la kura.
Source:mwananchi 17 juni 2013

Hivyo viti vingi ni vipi mbona hujaorodhesha? Na tukio la kupigwa na Nasari wakati alikuwa wakala na sio mpita njia hamuoni kama ndio linazidi kujenga hisia mbaya kwa CCM. Hapo nani mwenye fujo Nasari au ni hao vijana wa CCM. Ilikuwaje mpaka tukio hilo liokatokea. Sasa CCM mkiusishwa na mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa Chadema uliotokea juzi Jmosi mtakataa. Kwa uhuni huu mnaliweka Taifa pabaya.
 
Matokeo Jimbo la Chambani:

CUF: 2,751
CCM: 399
ADC: 112
CHADEMA: 12
Zimeharibika: 16
 
Tulimshauri "KAMANDA" wa mabua Nasary, asikimbie JKT hakutusikia, sasa ameona madhara yake KAKOFI kamoja tu damu kibaao puani hadi kulazwa........ huu sasa ndo ukamanda legelege....

Anyway taarifa njema ni kuwa ADC imeanza kupata umaarufu kupitia matokea yaliyotolewa jana,
 
Mwananchi wamekurupuka na haya ndiyo matokeo ya kutokwenda field kukusanya habari badala yake wanakaa ofisini na kuvizia updates za JF, habari gani haina maelezo ya kwanini vurugu zitokea, zilitokea wapi,ziliathiri vipi uchaguzi, CCM wameshinda kata ngapi, CHADEMA na CUF wamejitwalia kata ngapi? Mwamko wa wapiga kura ulikuwaje katika maeneo mbalimbali? Changamoto kubwa zilikuwa ni zipi kuelekea kwenye uchaguzi wa mwakani ili zifanyiwe marekebisho mapema? Uandishi wa aina hiyo haulisaidii taifa kukuza demokrasia na uwazi!
 
viti vingi vipi hapo! kwa nguvu za allah na damu ya ndugu zetu wa arusha mlioimwaga mtaanguka anguko baya 2015
 
hv kwa akili zako ndogo unasema ccm ni mwamba? Umefuatilia sehemu zote za uchaguzi umesikia wapenzi na viongozi wa chadema walivyo teswa na kupigwa na vitu vyenye incha kali?
 
CCM ni chama cha Wanyonge hakina wasiwasi kwenye Chaguzi zinazoshirikisha Wanyonge, pamoja na Propaganda nyingi lakin wananchi wakikaribia sanduku la kura wanakumbuka kuwa bila ya Ccm nchi itayumba
 
Nipo Minepa, gari la M4C limefika na kuchukua majeruhi na kuwawahisha Ifakara hospital. Wananchi wanawashangilia na kuwaambia wamewanyima kura CCM. Vipi Ifakara​

Pin ya bomu na maganda ya risasi yaliyookotwa katika uwanja wa soweto Arusha na wanajeshi yamegundulika kuwa ni toleo la kisasa mno na pia ni bidhaa za kiwanda cha China na zimezalishwa mwaka huu ktk kiwanda husika.
Bidhaa hizi zimekutwa zote zimetengenezwa katika kiwanda kimoja na ni bidhaa zilizowekwa serial numbers za mwaka huu na zinafuatana kwa kupishana degits chache sana, jambo ambalo linadhihirisha kuwa mtupaji/watupaji wa bomu na mpigaji/wapigaji wa risasi za moto ni kundi moja au ni mtu moja.

Mwanajeshi mmoja aliyekuwepo kwenye operation husika ametonya kuwa uchunguzi huu ulifanyika kwa maamuzi yao binafsi baada ya kushangazwa na aina ya Pin inayodhaniwa kuwa imesalia baada ya bomu husika kulipuka kuonekana kuwa ni unique sana tofauti na aina za mabomu waliyoyazoea na wanayoyamiliki kama jeshi. Wamegundua mabaki ya silaha hizi ni bidhaa mpya ambazo bado hazijawahi kutumika katika majeshi ya TZ(hasa bomu husika).

Waliamua kukagua maganda ya risasi za moto na pin husika na kuchukua serial numbers wakaingia kwenye search engines na ndipo wakagundua kuwa bidhaa hizo ni za mwaka huu na zimezalishwa ktk kiwanda kimoja cha serikali ya China.
 
Viti jumla vilikuwa 20 unaposema vingi unamaana havihesabiki

kiarabu wingi ni kuanzia tatu, kiswahili, kiingereza wingi ni kuanzia mbili viti ishirini kwa lugha zote ni vingi. Kuchukia CCM ni kuchukia Taifa, kuchukia CCM ni kuchukia mustakbal wako mwenyewe na kizazi chako.
 
hivi pamoja na tulipofikia kumbe kunawatu bado wanaipigania ccm kiasi hicho kweli!? Naanza kupata wasiwasi na 2015
 
Back
Top Bottom