CCM yazidi kumuandama Dkt. Slaa kuacha kukipigia ramli chama chao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yazidi kumuandama Dkt. Slaa kuacha kukipigia ramli chama chao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 4, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  03 OCTOBER 2012

  Na Mwanajuma Juma, Zanzibar

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimemtaka Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa, kuacha kukipigia ramli chama chao.

  Katibu wa Kamati Maalumu ya NEC, Itikadi na Uenezi Zanzibar, Bw. Issa Haji Usi Gavu, aliyasema hayo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui.

  Alimtaka afanye utafiti zaidi ili kujua nguvu ya chama hicho kisiasa ndio maana wananchi wanakipa ushindi katika chaguzi mbalimbali.

  Bw. Gavu alisaema Dkt. Slaa hana kigezo kinachothibitisha CCM imekufa au itakufa na kumtaka atambue kuwa, nguvu ya chama hicho kisiasa ni kubwa na haizuiliki kwa maneno ya kujifariji.

  "Apite kuanzia Ileje hadi Kisiwapanza, aanzie Kamachumu hadi
  mkokotoni, ataona joto la CCM lilivyotanda, huu ni uhai sio kifo kama anavyosema ili kuwadanganya Watanzani," alisema.

  Akizungumzi sakata la kudondoka kwa baadhi ya vigogo wa chama hicho wakiwemo wabunge, wawakilishi na makada maarufu kwenye chaguzi za chama hicho, Bw. Gavu alisema hali hiyo si sehemu ya utekelezaji mpango wa kujivua gamba.


  "Matokeo ya chaguzi zinazoendelea hayana uhusiano wowote na kuanguka kwa baadhi ya vigogo katika chaguzi zinazoendelea bali
  ni matokeo ya kawaida yanayotoa tafsiri ya demokrasia kuchukua mkondo wake," alisema.

  Bw. Gavu aliongeza kuwa, matokeo ya chaguzi za CCM yatasaidia kuimarisha uhai wa chama hicho na wanafurahi kupata viongozi wapya wenye upeo, ufahamu na wanataaluma.

  "Chama chetu kimepiga hatua katika suala zima la demokrasia kwa kuwa na mtazamo mpya, wanachama wetu ni wakomavu, tumepata safu ya viongozi ambao wataheshimu, kufuata maadili na wazalendo watakaojitenga na vitendo vya rushwa na ufisadi," alisema.

  Aliongeza kuwa, chaguzi hizo ni muhimu kwa uhai na maendeleo ya chama hicho na umeonesha dira ya mabadiliko na ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

  Akizungumza kwa kujiamini, Bw. Gavu alisema chaguzi hizo zimezingatia kanuni na taratibu hivyo wagombea ambao wataambulia patupu, wanayo nafasi ya kushiriki tena katika uchaguzi ujao ifikapo 2017.


   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  Sasa kwanini CCM iwe na Wasiwasi ? Ilikuwa inalalamika kuwa CHADEMA ni CHAMA cha kifamilia...

  Haya Mr. Presidaa hakwenda kwenye UN; akahakikisha CCM-NEC pia Imejaza CULT Ndugu na MARAFIKI kibao

  Yaani Rais ana Mdogo wake wa kike; wa kiume; mtoto wake best the Prince; Mkewe Mama Wama na Pia Mtoto

  wake
  Ambaye yuko kwenye Chipukizi ni Ka-Kiongozi ka Chipukizi TAIFA... woote waka CCM-NEC

  Bado wengine wengi hadi Mtoto wa Hassan Nassor Moyo; Baba yuko Upinzani alianzisha CCM; Mwanae yuko

  CCM-NEC...

  *** SASA wamefuata Mipango yote ya Dr. Slaa kwanini wanagombana nae???
   
 3. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hivi nyie wazenji lile wimbi la kuchoma makanisa limekwisha? au limeahirishwa tu?
   
 4. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Huyu Issa Haji Gofu Uzi anajidanganya. Ana mawazo ya mwaka 47 akidhani watanzania wa sasa ni wale wa 77. Endeleeni kujihadaa. Wenzenu KANU kule Kenya walijidanganya kama nyinyi sasa waulize wakao wapi kama siyo kunyea debe tena kwa aibu. Heri ya KANU waliiba na kujenga Kenya kuliko nyinyi mnaoiba kama panya na kuficha Uswisi na kuwekeza kwenye nyumba ndogo kama vile CUF.
   
 5. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi ccm wamefanya hata utafiti mdogo kweli? Spidi ya ccm kuporomoka ni kama barafu, waje huku mtaani waƶne kama kweli ccm inapendwa saana kama zamanh! Watanzania wana hamu na mabadiliko!
   
 6. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  Slaa hapigi ramli, amesoma alama za nyakati
   
 7. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Dr Wilbroad Peter Slaa
   
 8. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #8
  Oct 4, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kuna jamaa moja mwendawazimu alikuwa na uchafu mwingi usoni akapewa kioo cha kujitazama na ndugu zake ili kumshawishi aoge halafu yeye akakasirika na kukipiga chini kioo kile kikapasuka na akabaki na uchafu wake.

  Alipoulizwa akasema kioo kijinga kimeharibu uso wake. Nahusianisha kwa karibu hii story na huo mpambano wa Dr Slaa vs CCM.
   
 9. m

  malaka JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ndio kazi yake analipwa kwa matamko kama hayo. Msijali 2015 sio mbali tuombe mungu leo imetimia October 2012.
   
 10. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #10
  Oct 4, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hata mi sielewagi wanavosema cdm ni chama cha familia bora hata cdm wana familia ya watu mbali mbali... ccm ni chama cha kikwete maana ndg zake wote wamo humo..hata mkapa na mwinyi hawakuaga hivyo
   
Loading...