Uchaguzi 2020 CCM yazidi kujihakikishia ushindi Uchaguzi Mkuu Kanda ya Ziwa

Wewe acha kukurupuka ishu sio kudai tume huru bali kuchapisha habari za uongo ili kuleta chuki kwa serikali.
Twaweza hawakubanwa kwa ajili ya sheria ya takwimu,bali hawakuwa na kibali toka Costech na walifanya tafiti za kupotosh umma. Kwa ufupi walikuwa wanatumiwa na Chadema wakishiriana na mabeberu.
Mawazo ya kijinga kabisa!!!!
 
Hivyo ndio CCM na utekelezwaji wa Ilani zake chini ya Selikali ya Awamu ya 5 iliokabidhiwa jukumu LA kuitekeleza Ilani
 
Kuingiza habari ya Adolph kwenye hili suala ni upuuzi. Kama michango ilizidi na ikatumika kwa maendeleo tatizo lipo wapi? Au ulitaka wapewe wakanywe lubisi?
Mbona kule ukara michango ilizidi na zilizobaki zilijenga kituo cha afya?
Kwani Hitler akufanya maendeleo ya uchumi na miundombinu apa Ujerumani?
Mbona wapo wengi ambao nyumba zao zilidondoka ,ziliharibika kwasababu ya tetemeko na mpaka leo zipo hivyo?
Kwahiyo bila ajari ya kivuko watu wa Ukara wasingepata kituo cha Afya? Vipi hao wana wa Bukoba kitu gani wamepata baada ya janga la tetemeko?
 
Pesa ilitumika kurekebisha miundo mbinu na kukarabati majengo ya umma. Au ulitaka ndugu zako wapewe cash wakanywe lubisi? Mbona kuna watu walilipiwa pango na kusaidiwa material ya kujengea nyumba.
 
Kwahiyo waliotoa rambi rambi zilikua niza kurekebisha za miundo mbinu ya Serikali nasio kuwasaidia wananchi maskini?Sawa endelea kuwaita watu mbwa koko ila hao ni binadamu kama wewe.
 
Hatimae ile meli maarufu katika ziwa victoria New MV Victoria hapa kazi tu inanza safari zake hapo siku ya jumapili. Na kwa wakazi wa eneo la Kanda ya Ziwa huu ni ukombozi mkubwa kwa uchumi wa eneo hilo. Maana zaidi ya miaka saba usafiri toka Mwanza kwenda mkoani Kagera ulikuwa ni kwa njia ya barabara. Japokuwa barabara ni mkeka wa maana tokea Mwanza mpaka Bukoba mkoani Kagera lakini ulikuwa ni gharama Kubwa.

Wafanyabiashara wa ndizi wao walikuwa wanaumia zaidi sababu tani moja kwenye lori ni zaidi ya laki moja. Ila kwenye meli ni kama elfu ishirini na tano. Na kwao huu usafiri ni faraja kubwa. Pia, hata kwa abiria nauli ya meli ni karibu ya robo ya ile ya mabasi.

Kwa mantiki hii CCM inasubiri shukurani ya kura toka kwa wakazi wa Kagera na eneo zima la kanda ya ziwa victoria. Na projections zinaonyesha 98% ya kura za wananchi wa eneo hili sasa ni zawadi kwa CCM kwa kutekeleza ahadi aliyoitoa JPM ya kukarabati meli hii pamoja na Mv Butiama hapa kazi tu.

CHADEMA na wapinzani uchwara kama Act wazalendo ambao ni vibaraka wa mabeberu wasitarajie kupata hata kiti cha udiwani.
Mpina na genge lake wamefilisi wavuvi halafu Leo waifurahie CCM? Umerogwa wewe!!
 
Wewe acha kukurupuka ishu sio kudai tume huru bali kuchapisha habari za uongo ili kuleta chuki kwa serikali.
Twaweza hawakubanwa kwa ajili ya sheria ya takwimu,bali hawakuwa na kibali toka Costech na walifanya tafiti za kupotosh umma. Kwa ufupi walikuwa wanatumiwa na Chadema wakishiriana na mabeberu.

Nimekuambia leta sababu za Tanzania daima kufungiwa, ukasema wamechapisha kuhusu kudai tume huru ya uchaguzi. Ndio nataka kujua kudai tume huru ya uchaguzi kunaletaje chuki kwa serikali, wakati ni madai halali?

Hizo sheria za costech ni bad law, hizo ni baadhi ya sheria zenye nia ovu kwa utawala bora. Watawala pekee ndio waliokuwa wanaitaka hiyo sheria ili wapate nafasi ya kuwalisha wananchi watakacho, lakini wananchi wasijue lolote la upande wa pili. Ni wendawazimu kushabikia sheria mbovu.
 
Kuwa muelewa sijasema wamechapisha habari kudai tume huru ya uchaguzi. Bali wamechapisha habari za uongo kuhusu askofu Bagonza kuhamasisha maandamano kudai tume huru.
Costech ipo kwa mujibu wa sheria lazima ukitaka kufanya utafiti upate kibali. Kama Twaweza wanatumiwa na Chadema na mabeberu kwa nini wasishughulikiwe? Habari ya bad law hayo ni yako. Maana hata kifungu kinachopinga ushoga nyie Chadema mnasema ni bad law.
 
Wanasema Tanzania daima limefungwa baada ya kuonywa mara 10, ww unaandika hilo moja. Inawezekana Bagonza hakuitisha maandamano, lakini amehamasisha wananchi kuvaa nguo nyeupe siku ya 7/7 kuonyesha kudai tume huru ya uchaguzi. Hilo gazeti inawezekana limeleta tafsiri yake kwenye huo uhamasishaji. Ila sikuona kosa kubwa hivyo la kuifungia, labda hofu ni hiyo kusema maandamano kudai tume huru ya uchaguzi isiyotakiwa na rais na ccm yake. Lakini kuna magazeti yanayoisifu serikali, wanafanya makosa ya wazi bila kuchukuliwa hatua yoyote.

Costech kuwepo kwa mujibu wa sheria, sio mwanya wa kutekeleza sheria zenye nia ovu. Sheria mbaya hazipati uhalali kwakuwa kuna chombo kilichopo kisheria. Nionyeshe ni wapi cdm kama chama wanaunga mkono ushoga, ama ww ni wale bendera fuata upepo, ukisikia neno unalibeba kama lilivyo na kuanza kulirudiarudia, ili uonekane na ww unaenda na wakati.
 
Hatimae ile meli maarufu katika ziwa victoria New MV Victoria hapa kazi tu inanza safari zake hapo siku ya jumapili. Na kwa wakazi wa eneo la Kanda ya Ziwa huu ni ukombozi mkubwa kwa uchumi wa eneo hilo. Maana zaidi ya miaka saba usafiri toka Mwanza kwenda mkoani Kagera ulikuwa ni kwa njia ya barabara. Japokuwa barabara ni mkeka wa maana tokea Mwanza mpaka Bukoba mkoani Kagera lakini ulikuwa ni gharama Kubwa.

Wafanyabiashara wa ndizi wao walikuwa wanaumia zaidi sababu tani moja kwenye lori ni zaidi ya laki moja. Ila kwenye meli ni kama elfu ishirini na tano. Na kwao huu usafiri ni faraja kubwa. Pia, hata kwa abiria nauli ya meli ni karibu ya robo ya ile ya mabasi.

Kwa mantiki hii CCM inasubiri shukurani ya kura toka kwa wakazi wa Kagera na eneo zima la kanda ya ziwa victoria. Na projections zinaonyesha 98% ya kura za wananchi wa eneo hili sasa ni zawadi kwa CCM kwa kutekeleza ahadi aliyoitoa JPM ya kukarabati meli hii pamoja na Mv Butiama hapa kazi tu.

CHADEMA na wapinzani uchwara kama Act wazalendo ambao ni vibaraka wa mabeberu wasitarajie kupata hata kiti cha udiwani.
Ulikuwa unaelezea vzr mpaka ulipoamua kufunguka kwenye aya ya mwisho.
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom