CCM yaweza kujirekebisha iking`olewa

Mganga wa Jadi

JF-Expert Member
Mar 12, 2008
280
51
Mhadhiri wa Chuo Kikuu na mmoja wa wachambuzi wa masuala la kisiasa hapa nchini, Dk. Azaveli Lwaitama, amesema ingekuwa vema kama serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ikawekwa nje ya madaraka ili kujifunza makosa.

Aidha, aliwataka wananchi kuondokana na dhana kwamba, dola ni lazima iwe CCM na kutaka wavichague vyama vingine kwa madai kwamba CCM ya sasa si ile ya viongozi wa kinabii kama ilivyokuwa enzi za hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere bali ni ya mabaperi.

Akihitimisha kipindi cha Kipimajoto kilichorushwa juzi kupitia kituo cha ITV, Dk. Lwaitama alisema ili kuweza kukirekebisha chama tawala juu ya mambo yanayofanyika kwa sasa serikalini, ni kukiweka pembeni.

``CCM inaweza kujirekebisha ikiondolewa madarakani, kiwekwe pembeni ya serikali ili ijifunze kwa makosa iliyotenda,`` Dk Lwaitama alisema.

Aliongeza kuwa japo si kweli kama dola na serikali ya CCM kwa ujumla wake inahusika na matukio ya kifisadi na rushwa iliyotikisa nchi, lakini baadhi ya watendaji wake wasio waaminifu wanapaswa kuwajibika.

Mhadhiri huyo alisema ni lazima wananchi na jamii ikaondokana na dhana kwamba dola ni lazima iwe CCM na kutaka kuvichagua vyama vingine ili CCM ije kujifunza kuwa inapaswa kuwa ya wajenga nchi na sio wabomoaji.

Kipindi hicho cha juzi kilikuwa kinajadili na kutathmini matukio yaliyojiri kwa mwaka mzima wa 2008, ambapo waligusia pia mauaji ya maalbino, sakata la EPA na Richmond, migomo ya walimu na wanafunzi na suala la mafuta.

SOURCE: Nipashe
 
Back
Top Bottom