CCM yaweweseka: Mwenyekiti UVCCM asimamishwa kazi kwa kufanana na Mlinzi wa Mbowe... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yaweweseka: Mwenyekiti UVCCM asimamishwa kazi kwa kufanana na Mlinzi wa Mbowe...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mpotevu, Oct 8, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  Oct 8, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni. CCM imemsimamisha kazi Mwenyekiti wake wa UVCCM Arumeru kwa sababu eti amefanana na Mlinzi binafsi wa mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe. Soma habari hii.

  MLINZI binafsi wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amezua balaa kubwa kwa Chama cha Mapinduzi mkoani Arusha kutokana na sura yake kufafanishwa na ile ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) wilayani Arumeru, Boniface Mangaya Laizer, na hivyo kusimamishwa uongozi.

  Laizer ambaye ni rafiki mkubwa wa kada wa CHADEMA mkoani Arusha, Ally Bananga, aliyejiengua CCM mapema mwaka huu, amedaiwa kuonekana kwenye picha gazetini akiwa na viongozi wa CHADEMA wakati wa operesheni ya chama hicho katika mikoa ya kusini hivi karibuni.

  Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu, Boniface alisema kuwa ameshangazwa na tuhuma hizo alizoziita kuwa ni mizengwe akidai kwamba hata huyo mlinzi wa Mbowe, Zakaria Swai, anayefafanishwa naye hamfahamu.

  “Mimi sijawahi kuhudhuria mkutano wowote wa CHADEMA katika mikoa ya kusini na tuhuma hizo zilipoibuliwa nikalazimika kumtafuta huyo mlinzi ili nimfahamu. Katika picha iliyochapwa na gazeti moja la kila siku la Juni mosi mwaka huu, anaonekana Bananga akiwa na Mbowe na viongozi wengine na mlinzi huyo akiwa nyuma amevalia mawani meusi, sasa huyo watamfananishaje na mimi na kunisimamisha?” alisema.

  Katika barua ya kujulishwa kusimamishwa kwake yenye kumb. Na. CM/AR/S/K. 13/3/Vol. V/233 ya Oktoba mosi, mwaka huu, ikiwa imeandikwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda, mwenyekiti huyo anajulishwa kuwa anasimamishwa kutokana na tuhuma za usaliti.

  “ Tuhuma zinazokukabili za kiitikadi na usaliti ni nzito ambazo zinakuondolea sifa za kuwa kiongozi. Kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya Mkoa iliyokutana kuanzia Septemba 27-29, mwaka huu, ilitafakari kwa kina tuhuma zinazokukabili na kwa Mamlaka iliyonayo kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya 1977 Toleo la 2007- Ibara ya 96 (7) iliazimia kukusimamisha uongozi,” ilisomeka barua hiyo.

  Chatanda katika barua hiyo anaongeza kuwa Boniface anajulishwa rasmi kwamba kuanzia sasa amesimamishwa uongozi hadi hapo mamlaka yenye uwezo juu yake ya kikatiba itakapoamua vinginevyo.

  Hata hivyo, Boniface ambaye ameibuka na ushindi mkubwa katika uchaguzi uliomalizika hivi karibuni, alisema kuwa amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa UVCCM wilayani humo kwa taratibu zote za chama na hivyo akashangaa uamuzi huo umetoka wapi.

  Alisema kuwa wapiga kura wake pia wameshangazwa na uamuzi huo aliodai kuwa ni mkakati wa viongozi wa mkoa kupandikiza kiongozi wanayemtaka wao awe mwenyekiti wa UVCCM wilayani Arumeru.

  Naye rafiki yake wa karibu, Bananga, alizungumzia sakata hilo akisema huo ni ushuhuda tosha kuwa Chatanda baada ya kumaliza kutimiza azma yake ya kuvuruga vyama vya upinzani mkoani humo sasa dhambi hiyo imemrudia na kuanza kukibomoa chama chake.

  “Mimi Boniface ni rafiki yangu wa karibu tangu nikiwa CCM hadi sasa, ila kutokana na CCM kutapatapa na makundi yao Arusha wanadhani ninamtumia kama pandikizi kuwabomoa. Anayeonekana kwenye ile picha si Boniface bali ni Swai mlinzi wa Mbowe,” alisema.

  Bananga ambaye alikuwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Arusha na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa kupitia mkoa huo, aliongeza kuwa Chatanda ni janga la kitaifa kwani amevuruga upinzani Arusha na sasa amegeukia chama chake
   
 2. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Siku ya kufa nyani......
   
 3. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #3
  Oct 8, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Hizi kweli ni dalili za kufa nyani, ni kuweweseka kupita kiasi
   
 4. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Bado kidogo watageukana wao kwa wao
  Itakuwa gamba Vs gamba
   
 5. S

  SHEMGUNGA JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 653
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  karibu gamba huko hukuwezi!
   
 6. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #6
  Oct 8, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  ndio wameanza tayari namna hiyo
   
 7. s

  sony wega JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 234
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hehehe hii inanikumbusha wale watoto wa kaka yake tyson mzee wasira alivyowakana watoto wa ndugu yake
   
 8. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,108
  Likes Received: 7,364
  Trophy Points: 280
  Mfano ikitokea labda JK anafanana na Mbowe??, ha ha ha!!
   
 9. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Siku mlinzi wa Dr Slaa akionekana kufanana na Kikwete au Nape watamfanyaje? Siasa na namna hii ni za kizamani na kipuuzi. Kwani huyo jamaa alijiumba au wanaweza kumuumba tofauti na alivyo ili asifanane na mlinzi wa Mbowe?
   
 10. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,696
  Trophy Points: 280
  Sosi: Tanzania daima
   
 11. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #11
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  sio kila kitu source.....usikariri....waweza ambiwa na mamayako uyu ndo baba yako then uakaanza kuhoji source....?
   
 12. m

  malaka JF-Expert Member

  #12
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Du hii kali. Yaani inafikia mary anakimbia kivyli chake yeye mwenyewe? KAma ni kweli hii ni kali ya mwaka.
   
 13. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Hebu wekeni picha za wote wawili tuangalie na sisi wataalamu wa mambo ya sura
   
 14. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #14
  Oct 8, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Na watapoteana sana tu mwaka huu.....
   
 15. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #15
  Oct 8, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,635
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 16. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #16
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Acha wafu wazike wafu wao!
   
 17. m

  mamajack JF-Expert Member

  #17
  Oct 8, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  tobah!!!!!wehu kweli hawa.
   
 18. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #18
  Oct 8, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,148
  Likes Received: 2,109
  Trophy Points: 280
  na picha yake iko wapi sasa tulinganishe
   
 19. KirilOriginal

  KirilOriginal JF-Expert Member

  #19
  Oct 8, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 1,930
  Likes Received: 451
  Trophy Points: 180
  Yale yale ya Kombe, mnanikumbusha mbaaali na machungu mengi, haya mambo ya kufananisha watu ni hatari, Luteni Generali Imran Husein Kombe aliuawa na vijana wa usalama wa taifa eti wakimfananisha na jambazi aitwaye White, je ni kweli kuna polisi asiyeifahamu sura ya bosi wake? Napata tabu na roho inauma
   
 20. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #20
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  R.i.p sisiem
   
Loading...