Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 725
- 473
CCM YATAKA WAWAKILISHI WAKE KUWA KARIBU NA WANANCHI
Songea, Ruvuma
19 Septemba, 2021
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amewataka viongozi wa chama hicho kushughulikia matatizo ya wananchi badala ya kufanya vikao vya mara kwa mara kwa ajili ya kutafuta madaraka.
Shaka amewataka wawakilishi wa wananchi kupitia CCM wakiwemo wenyeviti wa vitongoji, vijiji, mitaa, madiwani na wabunge watekeleze wajibu waliouomba kikamilifu ikiwemo kufanya mikutano ya wananchi, kuhamasisha maendeleo na kushughulikia kero za wananchi pamoja na kuzitafutia ufumbuzi kwa wakati.
"Ili CCM iendelee kukubalika na kuaminiwa na wananchi na kuendelea kupewa ridhaa ya kuunda serikali na kuongoza Nchi yetu, ni lazima wawakilishi wetu na viongozi serikalini kuwa karibu na wananchi. Hivyo natoa maelekezo kwa wawakilishi wetu hawa nchi nzima wafanye mikutano ya wananchi ili kuhamasisha maendeleo, kusikiliza kero zao na kushirikiana nao kuzipatia ufumbuzi. Pamoja na kuendelea kuwa wasemaji na watetezi wa wananchi wote. Haya ni maelekezo ya ilani yetu ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 ibara ya 255 ambayo ni lazima chama tuyasimamie ili kuendelea kuaminiwa." Alisema Shaka.
Alilazimika kutoa maelekezo hayo kufuatia malalamiko yaliyotolewa kwake na wananchi wa mtaa wa Mlelewa kata ya Mletele ambao walidai tangu wamchague diwani wao Ndg Maurisi Lungu hajawahi kufanya mkutano katika mtaa wao.
Akiwa katika Ziara yake Manispaa ya Songea aliweza kukagua mradi wa machinjio ya kisasa uliogharimu shilingi bilioni 5.523 mpaka ulipofikia huku ukihitaji kiasi cha shilingi bilioni 3.798 kukamilika ili kutoa huduma kama ilivyokusudiwa. Machinjio hayo yanachinja ng'ombe 300 kwa siku ikiwa imetoa ajira za kudumu 35 na vibarua 40.
Shaka alisema "Mradi huu ni sehemu ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati kiuchumi yenye kulenga kuzalisha ajira, kuongeza thamani ya mazao ya mifugo kwa uchakataji nyama kwa ajili ya mahitaji ya ndani na usafirishaji nje ya nchi hivyo kuipatia nchi yetu fedha za kigeni. Ujenzi wa machinjio haya ya kisasa ni utekelezaji wa ilani yetu ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 ibara ya 40(x). Nawapongeza wote waliohusika katika utekelezaji wa mradi huu kwani wamemuunga mkono kwa vitendo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anamedhamiria kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi."
Aidha Shaka aliongeza kuwa mwakani kutafanyika uchaguzi ndani ya CCM hivyo wale wenye sifa za kuwania nafasi mbalimbali waachwe wawanie nafasi hizo ili kuendelea kukijenga na kukiimarisha pamoja na kukipatia chama ushindi katika chaguzi za 2024/2025.
Katika kuhitimisha hotuba yake kwa wananchi wa shina namba tatu, tawi la Mlelewa aliwahamasisha wananchi wananchi kujitokeza kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwaka 2022 kwani kushiriki kwao kutaiwezesha serikali kupata taarifa sahihi kwa ajili ya mipango ya maendeleo ya Nchi yetu.
Shaka yupo wilaya ya Songea Mjini mkoani Ruvuma alipowasili leo akitokea mkoani Mtwara na kuanza ziara ya uhamasishaji uhai wa chama mashinani, kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi, kuhamasisha sensa na kusikiliza kero za wananchi ikiwa ni muendelezo wa ziara ya Sekretarieti ya CCM Taifa inayoongozwa na Katibu Mkuu Ndg Daniel Chongolo katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Njombe.