CCM yawasuta Sitta, Lembeli,Nape asema kauli zao haziwezi kusikilizwa kwani hawajiamini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yawasuta Sitta, Lembeli,Nape asema kauli zao haziwezi kusikilizwa kwani hawajiamini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ndiyomkuusana, Sep 24, 2012.

 1. ndiyomkuusana

  ndiyomkuusana JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 627
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]na Waandishi wetu


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][​IMG] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakitishwi na baadhi ya viongozi wake ambao wamekuwa wakitoa kauli zao barabarani kwa ajili ya kulalamika na kukikosoa chama badala ya kupeleka malalamiko yao katika vikao husika.
  Kitendo cha viongozi hao kuendelea kutoa taarifa zao za malalamiko barabarani ni dalili za kutojiamini na kuonyesha udhaifu wa kuhimili mikiki ya uchaguzi ndani ya chama hicho na inawezekana wana agenda zao za siri.
  Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) Taifa ya chama hicho, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya vikao vya chama ambavyo vinaendelea mjini hapa.
  Licha ya Nape kutowataja vigogo hao kwa majina, lakini ni wazi kuwa walengwa ni pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye kwa siku za karibuni amenukuliwa akilalamikia vitendo vya ufisadi kwenye mchakato wa uchaguzi ndani ya CCM na hivyo kuibua mjadala mzito kwa baadhi ya makada akiwemo Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja, wakimtaka awataje kwa majina anaowatuhumu.
  Wengine waliosikika hivi karibuni wakilalamikia mchakato huo wa uchaguzi unaoendelea ni Mbunge wa Kahama, James Lembeli na Nimrod Mkono wa Musoma Vijijini ambao inasemekena majina yao yamekatwa kwenye orodha ya wagombea, huku wakisema hapatatosha iwapo wataenguliwa kweli kimizengwe.
  Nape alisema kuwa CCM inashangazwa na baadhi ya wanachama wake ambao wanaonyesha woga wa kushindwa kuhimili mikiki ndani ya chama, hususan katika kipindi hiki cha uchaguzi na badala yake wamekuwa wakitishia kujitoa kama majina yao hayatarudishwa kwa ajili ya kuchaguliwa katika nafasi zao walizoomba.
  Alisema kuwa chama hakiwezi kuwasikiliza viongozi ambao wamekuwa na tabia ya kutoa matamshi yao barabarani na kwamba kama wanataka kutoa kauli hizo, watumie fursa ya kuwasilisha hoja zao katika vikao.
  “Chama hakiwezi kusikiliza kauli za barabarani ambazo zinatolewa na viongozi hao, kama wana hoja wazilete katika vikao kwa maana nao ni viongozi, wasipofanya hivyo basi huenda wana agenda zao za siri, ambazo wanazijua wao,” alisema.
  Kuhusu baadhi ya wagombea ambao walisikika wakidai kuwa majina yao yasiporudishwa patachimbika, alisema kuwa inaonyesha ni jinsi gani hawajiamini kwani kiongozi ni lazima awe mvumilivu na mwenye kuhimili mikiki ya siasa za sasa ambazo zina ushindani mkubwa.
  “Kama kiongozi anaanza kusikia tetesi kuwa jina lake halitarudishwa halafu anaanza kusimama barabarani na kudai kuwa hapatatosha, ni wazi kuwa ni mwoga wa kuhimili ushindani, lakini nataka kusema kuwa haki itatendeka na busara zitatumika.
  “Hakuna mtu ambaye jina lake litakatwa kwa ajili ya mizengwe, bali vigezo vitazingatiwa ili kila mmoja apate haki yake, na lazima wagombea watambue kuwa kwa vyovyote vile lazima apatikane kiongozi ambaye ataweza kuongoza jumuiya husika,” alisisitiza Nape.
  Aliongeza kuwa kutokana na kuwepo kwa wingi wa wagombea katika nafasi mbalimbali, kuna uwezekano wa kutokea msuguano mkubwa kwa wanachama kutokana na kila mmoja kutamani kushika nafasi aliyoiomba.
  “Kimsingi wanachama waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali ni wengi zaidi ya mahitaji, hii ni ishara kuwa chama bado kinapendwa… kunawezekana kukatokea msuguano wa ndani kutokana na wingi wa wagombea, lakini chama kina utaratibu wa kumaliza mambo kama hayo,” alisema.
  Kuhusu vikao kwenda kinyume na ratiba, Nape alisema kuwa kutokana na wingi wa wagombea wa nafasi mbalimbali, imelazimika sekretalieti kukaa siku tatu badala ya moja na kamati ya maadili ilitakiwa ikae siku moja, lakini imekaa mbili tofauti na matarajio.
  Nape alisema kutokana na wingi wa wagombea, imewalazimu vikao kuchukua muda mwingi kujadili kwa makini ili kuhakikisha haki inatendeka na kuongeza kuwa, kwa nafasi ya wenyeviti wa mikoa zinazotakiwa ni nafasi 31 ila walioomba ni 187, katibu siasa na uenezi mkoa zinatakiwa nafsi 31 walioomba pia ni 187.
  Alisema kuwa makatibu wa uchumi/fedha wa mkoa nafasi zinazohitajika ni 31 ila walioomba ni 170, wenyeviti wa wilaya nafasi ni 31 walioomba 148, wenyeviti wa wilaya wanahitajika 161 walioomba ni 965, wajumbe wa NEC taifa wanahitajika 221, lakini walioomba ni 1,380 na wajumbe wa NEC taifa wanahitajika 20 bali walioomba ni 89.
  Nape alisema kuwa nafasi nyingine ni wenyeviti wa Jumuiya Taifa ya UVCCM ambayo inahitajika nafasi moja ila imeombwa na wagombea 47, UWT nafasi moja nayo inagombewa na watu 9, Jumuiya ya Wazazi nafasi moja imeombwa na watu 22 na makamu mwenyekiti UVCCM inahitajika nafasi moja, lakini walioomba ni 27, UWT nafasi ya makamu imeombwa na watu watatu huku ile ya wazazi ikiombwa na watu 10.
  Hata hivyo, Nape alisema kuwa hatua ya mwisho ya kupitisha majina ya wagombea hao ni NEC na kwamba vikao vingine vinapitisha na kutoa alama za sifa ya wagombea.
  Kinana ang’atuka
  Mwanasiasa nguli na kada maarufu wa CCM, Abdulrahman Kinana, ametangaza kung’atuka kuwania nafasi yoyote ndani ya chama hicho tawala.
  Kinana ambaye amekuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) na Kamati Kuu (CC) kwa miaka 25 sasa, ametoa kauli hiyo jana alipoulizwa sababu za kutogombea nafasi yoyote ya uongozi katika uchaguzi unaoendelea ndani ya CCM.
  Kada huyo maarufu ambaye amepata kuwa Meneja Kampeni wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa na Rais Jakaya Kikwete, alisema miaka 25 ya kushiriki katika vikao vya juu inatosha na ni vizuri kung’atuka.
  “Naamini kuna wana-CCM wengi wazuri wenye sifa na uwezo wa kuongoza chama. Uongozi ni kupokezana vijiti na ni wakati wangu kukabidhi wengine kijiti hiki,” alisema Kinana.
  Hata hivyo hakuwa tayari kueleza kama mwenyekiti wa chama hicho, Rais Kikwete atamteua kuwa mjumbe wa NEC atakubali au la.
  Kinana amekuwa kada anayeheshimika sana ndani ya CCM, mwenye ushawishi mkubwa hasa wakati wa vikao vya juu vya chama.
  Wakati Kinana aking’atuka, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema kada huyo amekuwa msaada mkubwa kwa chama.
  Hata hivyo alisema licha ya kung’atuka, Rais Kikwete anaweza kumteua akitaka kupitia nafasi kumi alizonazo kwa mujibu wa Katiba ya CCM.
  “Kinana ameng’atuka wakati bado chama kinahitaji mchango wake. Hata hivyo mwenyekiti wetu wa taifa, Rais Kikwete hazuiwi akitaka kumteua,” alisema Nape.
  Katika hatua nyingine, Nape amesema kuwa yeye hajagombea nafasi yoyote ya uongozi ili kujipa nafasi ya kusimamia vizuri uchaguzi huo.
  “CCM ina watu wengi sana wenye sifa na uchaguzi umekuwa na changamoto kubwa. Hivyo nimejipa nafasi kuweza kusimamia uchaguzi huo kwa karibu zaidi,” alisema Nape.
  Katika hatua nyingine, kikao cha Kamati Kuu (CC), kilichotarajiwa kuanza jana na kumalizika leo, huenda kikamalizika kesho baada ya kuchelewa kuanza.
  Kikao hicho chini ya Rais Kikwete, kilitarajiwa kuanza jana saa tatu asubuhi, lakini kilikwama na kuanza saa 11 jioni.
  Habari kutoka ndani ya CCM zilisema kuwa hali hiyo ilitokana na kikao cha Kamati ya Maadili kuchelewa kumalizika kutokana na mvutano mkubwa wa kupitia majina ya wagombea.
  Wazee wamvaa Sitta
  Wazee wa CCM mkoani Shinyanga, wametishia kufanya maandamano ya amani kuhusiana na kauli tata zinazoendelea kutolewa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta.
  Katika tamko lao, wazee hao walisema wakati umefika sasa Sitta awaeleze Watanzania juu ya kauli zake hizo, ikiwemo ile ya kuwepo kwa mafisadi ndani ya chama na aliyoitoa hivi karibuni akiwa Karagwe, ya maisha bora kwa kila Mtanzania hayatawezekana.
  Kwa niaba yao, Shomvi Ibrahimu Saidi, alisema kuwa waziri huyo ambaye pia ni mjumbe wa NEC na mbunge wa Urambo Mashariki, amekuwa akikaririwa akitoa tuhuma nzito ndani ya serikali na chama, hivyo ni vema akaweka wazi majina ya watuhumiwa wa ufisadi.
  Pia walikumbushia jinsi kiongozi huyo alivyowahi kuitolea maneno makali Kamati Kuu ya CCM katika kipindi cha ‘Dakika 45’ kinachurushwa na Televisheni ya ITV, akisema kwamba ilihongwa na mafisadi ikabadili utaratibu wa kuchagua Spika wa Bunge.
  Wazee hao wamemuomba Waziri Sitta kama hana ushahidi wa kutosha wa kuupeleka kwenye vikao vya chama na vyombo vya dola kama TAKUKURU, polisi na mahakama, ni afadhali akae kimya kuliko kuendelea kuwachanganya watu.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. K

  Kibagata JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 773
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Six hachanganyi watu ila anawambia ukweli nyie CCM. Ubaya wenu mambo ambayo mi kwa masilahi ya Taifa mnataka mtu aje asemehe kwenye vikao vyenu vya kifisadi ili mbane humo. Lakini kumbukeni usiri huu wa masirai ya kitaifa ndo yametufikisha hapa tulipo. Kiongozi anaiba Mali za umma anajua watasema kwenye NEC then yy anakuwa ameandaa fungu kwa wajumbe then mtoa mada anaonekana muongo. Ndo maana Mzee sita anasemea nje maake anawajua wenzake kwa kula Rushwa.
   
Loading...