CCM yawasilisha utetezi kwa Tendwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yawasilisha utetezi kwa Tendwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Luteni, Sep 2, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  [​IMG] Mkulo asema Bunge lilibariki mishahara
  [​IMG]
  Kinana naye atoa ufafanuzi kilichojiri
  [​IMG]
  Makamba kama kawa aendelea na kejeli


  Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewasilisha utetezi wake rasmi dhidi ya pingamizi lililowasilishwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikitaka mgombea rais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete aenguliwe kwenye kushiriki Uchaguzi Mkuu.

  Akizungumza na NIPASHE jana, Mwenyekiti wa kampeni za CCM Abdulrahaman Kinana, alisema wamewasilisha utetezi wao kwa msajili kama walivyotakiwa na wamezijibu hoja zote (tuhuma) zilizowasilishwa dhidi ya mgombea wao Rais Kikwete. Kinana alisema utetezi huo uliwasilishwa na viongozi wa CCM kwenye ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa jana.


  Alipoulizwa madai ya mgombea wao kuongeza mishahara ya wafanyakazi kwa kutumia fedha za serikali (OC) tena bila kupitishwa na Bunge, Kinana alisema suala hilo halina ukweli, kwa vile fedha zote zinazotumika zilipitishwa na Bunge wakati wa mkutano wa bajeti.


  Hata hivyo, alisema haelewi ni kwanini kila kitu ambacho kinasemwa na mgombea urais wa Chadema, Dk. Willibroad Slaa, kinaaminiwa na kuonekana kuwa ndicho chenye ukweli.

  Akifafanua alisema suala la fedha za nyongeza ya mishahara ya wafanyakazi kutoka kwenye fungu la OC, ni madai yaliyotolewa na Dk. Slaa, lakini hakuna uthibitisho.

  "Slaa kusema fedha hizo zimetoka OC, sio issue (hoja), hayo ni madai yake isichukuliwe kuwa ndio ukweli, na sisi tumepeleka majibu yetu kwa Tendwa, ambayo yamejaa ukweli na uthibitisho usiokuwa na ushabiki wowote wa kisiasa wala kujitafutia umaarufu," alisema.


  Alipoulizwa wamejibu nini hasa katika madai hayo, alidai hawezi kutaja majibu hayo kwenye vyombo vya habari, kwani kwa kufanya hivyo na yeye atakuwa mtovu wa nidhamu kama Chadema.


  "Msajili ametutaka tupeleke majibu yetu, tutakuwa watu wa ajabu kuyasambaza kwenye vyombo vya habari, tutakuwa tumeingilia kazi yake, ngoja asome mashtaka na utetezi, kisha atatoa hukumu," alisema Kinana huku akisisitiza kwamba kama mwandishi anataka mengine kuhusu majibu hayo awasiliane na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba.


  Akizungumza na NIPASHE, Makamba alisema wamewasilisha utetezi huo, lakini naye akasema utetezi huo ni siri. "Wewe usitake kuuliza juu ya waraka wetu kwa Msajili, ila kile tulichokisema naweza kukueleza na wewe, mimi ndio Katibu Mkuu wa Chama hiki," alisema Makamba.


  Alisema suala la kuongeza mishahara lipo kwenye Ilani ya CCM ya mwaka 2005.

  Vilevile alisema hata ahadi aliyotoa Rais Kikwete ya kununua meli, ni jambo ambalo lipo kwenye ilani hiyo.

  "Tuliahidi kwamba tukichaguliwa tutaimarisha usafiri wa anga, ardhini na ule wa majini. Sasa kununua meli ni sehemu ya kuimarisha usafiri wa majini,"alisema.


  Alisema hata suala la nyongeza ya mishahara licha ya kuwepo kwenye ilani, lakini Rais Kikwete amekuwa akilizungumzia kila mara na kusema wafanyakazi wataboreshewa maslahi kwa kadri ya uwezo unavyopatikana.


  Alisema Rais kutekeleza ahadi alizotoa kwa wafanyakazi sio rushwa, kwa vile hata Dk. Slaa naye ametoa ahadi ya nyongeza ya mshahara mkubwa zaidi kwa wafanyakazi, kuliko wanaolipwa sasa.


  "Vilevile Rais kusema serikali itachukua deni la Nyanza la bilioni tano, pia alikuwa anatekeleza ilani yake, kwa vile ndani ya Ilani hiyo tumeahidi kuimarisha ushirika,"alisema Makamba.


  Awali akizungumza na gazeti hili kabla ya kupeleka majibu kwa Msajili, Makamba alikejeli pingamizi hilo la Chadema na kusema limeandaliwa kwa hoja dhaifu.


  Jumatatu wiki hii Chadema kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, iliwasilisha pingamizi hilo kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa.


  Pingamizi hilo lililenga kumzuia Rais Kikwete, asishiriki Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, kwa madai kuwa amekiuka Sheria za Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010.


  Hata hivyo Makamba alisema baada ya chama chake kupokea na kupitia pingamizi la Chadema, imebainika kuwa hoja zilizowasilishwa na wapinzani hao ni dhaifu na hazina msingi.


  Makamba alisema Rais Kikwete hafanyi kosa lolote kuwaeleza wananchi mambo yaliyofanywa na serikali yake katika kipindi cha miaka mitano iliyopita na matarajio yake kwa miaka mitano ijayo.


  Makamba pia alisema katika ilani ya chama hicho ya mwaka 2005, waliahidi kuboresha usafiri wa anga na majini, hivyo Rais Kikwete alipoahidi ununuzi wa meli haipaswi kutafsiriwa kuwa rushwa.


  "Tuliahidi kuboresha usafiri wa anga na majini sasa ukienda sehemu ukakuta wananchi wana shida ya meli, usiwanunulie kisa ni wakati wa kampeni," alihoji.

  "Sisi tunatekeleza ilani na lazima tuwaeleze wananchi tumewafanyia nini na tutawafanyia nini,"

  Alisema Dk. Slaa amekuwa akiahidi mambo mbalimbali katika mikutano yake ya kampeni, hivyo haoni sababu ya chama hicho kuendelea kumsakama Rais Kikwete.


  Kuhusu hoja nyingine ya Chadema kwamba mgombea wa CCM anatumia wadhifa wake wa urais kutoa ahadi, Makamba alisema kwa mujibu wa Katiba, Kikwete bado ni Rais hadi atakapopatikana mwingine katika Uchaguzi wa Oktoba 31 mwaka huu.


  Katika pingamizi hilo lililowasilishwa na Mnyika, chama hicho kinalalamika kuwa Rais Kikwete amekuwa akitumia madaraka yake ya urais kutoa ahadi kwenye kampeni jambo ambalo linakiuka kabisa sheria hiyo.


  "Sheria inakataza mtu aliyeko madarakani kama Rais au waziri kutoa ahadi yoyote iwe ya mali au fedha taslimu kwa kutumia wadhifa wake kwenye kampeni, lakini tumeshuhudia Rais Kikwete akifanya hivi kila siku ina maana sheria aliisaini bila kuisoma," alihoji Mnyika.


  Alisema nyongeza ya mshahara katikati ya kampeni ni rushwa ya waziwazi kwa mujibu wa kifungu namba 21 (1) (a) na (e) ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi namba 6 ya 2010.
   
 2. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kama kila ahadi inayotolewa na viongozi jibu lake ni utekelezaji wa ilani kulikuwa na haja gani kupitishwa kwa kifungu namba 21 (1) a na e cha sheria ya gharama za uchaguzi. Kifupi ni kwamba hakuna mtu yeyote atakayebanwa na kifungu hicho kwa vile jibu litakuwa ni rahisi tu natekeleza ilani ya chama.

  Mfano ilani zote toka ya 2000 zinasema zitaongeza mishahara, sasa hata kama utaratibu utakiukwa mwaka 2010 bado viongozi wanasema wanatekeleza ilani ya 2000 ni hatari tunakoelekea. Kuyachukua madeni yote ya vyama vya ushirika tunasema ilani ilisema tutaimarisha ushirika just simple like that, nafikiri tumepotea njia tunahitaji mtu wa kutuongoza.

  Kwa hiyo tusiwe tunapoteza muda na mali kuanzisha sheria ambazo tunajuwa hazina misingi wala uzito wowote linapokuja swala la utekelezaji, ndiyo naanza kuona usahihi wa watu waliokuwa wanapinga na kusema sheria hizi hazina maana yeyote.

  Mwisho nakishukuru chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kwa pingamizi hili, hata kabla ya kutolewa uamuzi na Msajili na NEC tayari limesaidia jamii ya watanzania kuonyesha ubutu wa sheria hizi mpya zilizosainiwa kwa mbwembwe.
   
 3. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  Mbona kikwete alisaini kwa mbwembwe sana ile kitu gharama za uchaguzi?????
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180

  hapo kwenye BOLD siyo TUSI hilo?
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,205
  Trophy Points: 280
  The problem CCM huwa wanajifanya wao ni smart wanafikiri watu hatuwaoni, lakini siku huwa hazigandi kuna siku na wao watakuwa wapinzani halafu naomba wakati huo hasa Makamba awepo.
   
 6. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  atakuwa keshakufa maana kabisha chini ya miaka mitano, kutokana na kauli yake na CCM haiwi upinzani pengine hadi uchaguzi ujao kwa maana huu weshashinda
   
 7. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2010
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Nilishasema humu, "THE BUCK STOP WITH WASAIDIZI" according to MAKAMBA. Hili ZIGO ameshatupiwa MKULO kama MASHA alivyotupiwa la BASHE.

  Pia sisiemu wanasahau kuwa kutoa ahadi sio kosa, bali kutoa ahadi na kutekeleza wakati huu tena bila BARAKA za BUNGE kwa matumizi yanayohitaji baraka zake ni kosa.

  Hawana jipya, serikali ya GUNDI GUNDI tu.
   
 8. Epason

  Epason JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2010
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 427
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Makamba ni sawa na gunia tupu, sawa na puto lenye hewa za kueleaelea, ubabe wa dhamana, lakini uongozi wake hauna nguvu za hoja bali ni za ubabe," alisema Shibuda.

  Jawabu zuri kwa mtu kama makamba ni kumnyamazia..... ila ningependa akutanishwe na Shibuda kwenye huo mdahalo.
   
 9. Epason

  Epason JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2010
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 427
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Makamba ni sawa na gunia tupu, sawa na puto lenye hewa za kueleaelea, ubabe wa dhamana, lakini uongozi wake hauna nguvu za hoja bali ni za ubabe,” alisema Shibuda.

  Jawabu zuri kwa mtu kama makamba ni kumnyamazia..... ila ningependa akutanishwe na Shibuda kwenye huo mdahalo.
   
 10. c

  chach JF-Expert Member

  #10
  Sep 2, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 439
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Hii nchi bwana eti mwizi wa kuku sharti akutwe na kipande cha mnofu au mchuzi.Akikutwa na kuku mzima siyo Mwizi.Hivi mashairi ya Mpoto yameishia wapi au ameishaajiriwa na CCM?
   
 11. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #11
  Sep 2, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35

  My take:
  1. Hii sheria ilitungwa ili kuwabana vyama vya upinzani zaidi na sio CCM.
  2. Hiyo sheria ni "too vague" … inaweza kupewa tafsiri yoyote kutegemea na nani analalamikiwa.
  3. Inaonesha CCM hawajajiandaa kwa utawala wa sheria… ushahidi mwingine ni vita ya ufisadi, sheria imekiukwa mchana kweupe kwa wahusika waliokwapua pesa za EPA kusamehewa kwa tamko la rais.
  4. Body language ya Kinana na Makamba inaonesha jibu la Tendwa atakalotoa next week. Kikwete hataenguliwa.
  Kilichobaki hapo ni ku-appeal kwenye mahakama kuu, potelea mbali hata kama huko nako bado itakuwa kesi ya nyani kuipeleka kwa ngedere. Lakini ukweli utakuwa amplified zaidi na jitihada zitakuwa sio haba.
   
 12. K

  Keil JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hoja nyingine zote watazikwepa kwa kusingizia kwamba wanatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya 2005 - 2010. Lakini swala la mishahara ya wafanyakazi wa sekta ya umma sioni kama wataweza kulikwepa.

  Kwanza, kuongeza kima cha chini kutoka Sh. 135,000 mpaka Sh. 260,000, ni ongezeko la karibu asilimia 75. Nyongeza hiyo ya mishahara haiwezi kuingizwa kwenye fungu la OC, lazima iwe reflected kwenye bajeti ya wizara husika. Swala siyo kwamba Bunge lilipitisha bajeti, swala ni kwamba je, Bunge lilipitisha hiyo nyongeza ya mishahara? Nadhani huo ndio utaratibu unatakiwa kufuatwa.

  Kitu kingine, Kikwete alitamka kwa kinywa chake mwezi Mei kwamba hata kama wafanyakazi watagoma kwa miaka 8, serikali yake haiwezi kuongeza mishahara mpaka kima cha chini kifike Sh. 315,000. Lakini within three months mishahara ilipanda kinyemela (kimya kimya) na tena kwa kiwango kikubwa, kinyume na claim ya Kikwete ya mwezi May. Hapa lazima kunakuwa na mshaka zaidi.

  CHADEMA wanaweza ku-drop hoja nyingine zote, lakini hoja ya nyongeza ya mishahara siyo ya kuachiwa, wanatakiwa kukaa na wana sheria waliobobea na pia wapitie Bajeti yote kwa makini ikiwa pamoja na Hansard maana serikali ya CCM ni mafia, wanaweza kutoka na version nyingine ya Bajeti wakadai ile ya mwanzo ilikosewa.
   
 13. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #13
  Sep 2, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Huyu hapa chini ni mwanachama wa Chadema... Je hapa katusi au kasifia?
   
 14. t

  tumaini yarumba Member

  #14
  Sep 2, 2010
  Joined: Dec 29, 2009
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kinana na makamba waongo si jk mwenyewe alisema hata wafanyakazi wagome miaka nane hapandishi mishahara?mkulo atuletee bajeti tuone kama kweli hawajaedit mana hawa watu wajaja halafu nyongeza mpaka leo haijawekwa eti hiyo ni nrushwa ccm hawatajinasua wote wameoza yani watanzania wanatakiwa kumfanya jk rais wa kwanza kukaa miaka mitano madarakani kweli bwagamoyo wametubwaga mbona
   
 15. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #15
  Sep 2, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Huu mjadala unaoendelea hapa ni extra extra extra large kwa ubongo wako. Waachie watu wenye busara zao. Wewe rudi kwenye simple iisues zinazokufaa...
   
 16. A

  African Member

  #16
  Sep 3, 2010
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM has submitted its defence to the objections filed by Chadema to the Registrar of Political Parties John Tendwa. Kikwete’s campaign manager Abdulrahman Kinana told reporters that CCM has done so as required by Tendwa. He said it is not true that presidential candidate Kikwete raised minimum wages of public employees without approval of Parliament. When asked for details, Kinana said it would be improper to disclose the contents of letter sent to Tendwa. On Monday Chadema submitted their objection to Tendwa, saying Kikwete violated the Election Expenses Act and misused his office by giving pledges during his campaign trail. Chadema therefore wants Kikwete to be disqualified from running for the presidential race. (Nipashe)
   
 17. t

  tumaini yarumba Member

  #17
  Sep 3, 2010
  Joined: Dec 29, 2009
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mi nadhani wewe macho unafaidika na sera butu za ccm may be you are that much bright but you can not tel or read the signs
   
 18. e

  emalau JF-Expert Member

  #18
  Sep 3, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Dr Slaa ni smart sana lazima anayo original, wakija na za kupika wataumbuka
   
 19. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #19
  Sep 6, 2010
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hii issue imekwisha,sasa kilichobaki ni kukata rufaa na kuhangaika na mahakama wee..hadi uchaguzi huoooooo.Nendeni kwa majukawaa mfanye kampeni,haya memgine manapoteza muda.Huu ni ushauri wa bure.:becky:
   
Loading...