CCM yawaomba radhi Watanzania tatizo la ununuzi wa LUKU

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Katibu wa itikadi na Uenezi CCM amewaomba radhi watanzania wote kutokana na tatizo la ununuzi wa umeme kwa njia za kielektroniki lililo jitokeza nchini kote kwa siku tatu mfululizo,

Baada ya kupokea taarifa za tatizo hilo Shaka Hamdu Shaka alifanya ziara usiku kwa kuzunguka katika vituo vyote vilivyoelekezwa kupatikana huduma ya LUKU na kujionea kadhia walioipata watanzania walio wengi.

Leo Katika Mkutano wa Katibu Mkuu na waandishi wa habari Katika ofisi za CCM DODOMA , Shaka H Shaka alipata wasaa wa kumueleza katibu Mkuu wa CCM Ndg Daniel Chongolo kadhia yote waliyoipata watanzania na kisha kumuomba aseme neno Pindi anapoongea na waandishi wa habari, nae alisema,

"Nionye wale wenye nia ovu na Nchi yetu ambao walitaka kutuweka gizani, niipongeze Serikali kwa hatua za awali walizochukua katika kuhakikisha wananchi wanaepukana na changamoto ya manunuzi ya Umeme....."

akaongeza, wale wote watakaodhibitika kuwa walihusika na kadhia hii kwa wananchi, wachukuliwe hatua stahiki za kisheria

Kupitia sakata hilo Shaka Hamdu Shaka alimpongeza Sana Mh Waziri Mkuu wa jamuhuri ya muungano wa TanzaniaMh Kassim Majaliwa kwa kuchukua hatua za haraka sana Katika kukabiliana na tatizo hilo ndani ya muda Mfupi Sana na Kutoa maagizo ya uchunguzi wa kina juu ya tatizo hilo.

Lakini pia Ndg Shaka Hamdu Shaka alitoa pongezi za dhati kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN kwa umakini wake wa kusimamia serikali na watendaji wake wote.

Leo 20/05/2021 kwa mara ya kwanza katibu Mkuu wa CCM alikuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu mustakabili mzima wa chama cha Mapinduzi na serikali yake.

SEKTETARIATE MPYA
#kazi Iendelee

IMG-20210520-WA0030.jpg
IMG-20210520-WA0028.jpg
IMG-20210520-WA0025.jpg
IMG-20210520-WA0024.jpg
 
Hapa ndio unaona tatizo la Tanzania. Yaani anaweza akatoka mtu ndani ya CCM akiwa hana cheo chochote ndani ya Serikali akatoa amri au akaisemea serikali.

TANESCO ndio waombe radhi sio chama cha siasa!
 
Hizi ni hoja za shirika na serikali,hazitakiwi kujibiwa au kuombewa radhi na vyama vya siasa, tukae kwenye mstari wa professionalism
 
CCM watuombe radhi kwa "KUTUIBIA KURA" kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa na uchaguzi mkuu kwanza, halafu watuombe radhi kutupa viongozi "MODEL YA KINA OLE SABAAYA" ambao walituletea waje kudhulumu na kuteka wananchi badala ya kuongoza wananchi.

Ndio mengine yafuatie.
 
Picha bila utambulisho wa nani ni nani haileti maana, si watu wote wanawajua hao
 
CCM watuombe radhi kwa "KUTUIBIA KURA" kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa na uchaguzi mkuu kwanza, halafu watuombe radhi kutupa viongozi "MODEL YA KINA OLE SABAAYA" ambao walituletea waje kudhulumu na kuteka wananchi badala ya kuongoza wananchi.

Ndio mengine yafuatie.
Hapo upo sahihi kabisa waache unafiki wa kiwango Cha rami
 
CCM wasiingilie mambo yaliyo mbali nao. Ni kukosa uelewa na mwelekeo. Waziri wa sekta husika na Waziri mkuu, wametoa kauki, inatosha.

Kwa mtindo huu, kesho utasikia mwenyekiti wa wacheza bao amewaomba radhi Watanzania kwa kukosekana huduma za Luku kwa njia ya mtandao.

CCM kama cha cha siasa inatakiwa ijue majukumu, wajibu na mipaka yake kama chama, wasijiingize na wenyewe kujifanya ni serikali au taasisi za kiutendaji.
 
Wangeomba radhi kwa wizi wa kura ningewaelewa na kuwasamehe kama imani yangu inavyotaka.Kusamehee na kusahau.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom