msumeno
JF-Expert Member
- Aug 3, 2009
- 2,827
- 1,729
Wakati mchakato ukiendelea kule Dodoma jamaa zangu hapa DRC hawakua nyuma kuufuatilia, kuna jamaa yangu mmoja alinitembelea kwangu na kukuta nafuatilia recorded video ya mchakato wa CCM wa kumpata mgombe wa urais ,,, tuliangalia mwanzo mpaka mwisho. Mcongoman huyu kwa masikikitiko akasema ''natamani na sisi tungekuwa kama ninyi watanzania''. Alifurahia kila tukio na kusema hii ndio democrasia ya kweli na nchi zote Africa zinapashwa kujifunza toka kwenu. Huyu bwana aliniuliza pia kama kuna vyama vya upinzani vingi na kama wana uhuru wa kufanya shuguli za kiasa.. kwa kweli nilimjibu ndio na wako huru kisiasa na nikamwambia na wao viongozi wao wanapatikana kwa kura.
Leo wakati nikichungulia FB, nimekutana na post ya jamaa yangu mmoja wa Burundi, huyu jamaa kasema mengi sana akisifia democrasia ya CCM, nikiweza nitaipost hiyo post ya huyu jamaa, iko kwa kifaransa na kiigereza. mchakato wa CCM ulifuatiliwa sana hasa hapa DRC.
Nilichotaka kusema ni kwamba Democrasia yetu inasifika sana nchi zingine.