CCM YAWA GOLDEN TEMPLE OF AMRITSAR (Punjab India) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM YAWA GOLDEN TEMPLE OF AMRITSAR (Punjab India)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ebaeban, Jul 30, 2012.

 1. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,834
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Haya tarehe 6 June 1984 siku ya Jumatano majeshi ya serikali chini ya utawala wa Waziri mkuu Bibi Indira Gandhi yalivamia msikiti mtakatifu wa dhahabu wa masingasinga wa AMRITSAR. Kwa mjibu wa imani ya masingasinga pale ni pahala patakatifu ambapo ilikuwa hairuhusiwi kuingia na viatu. Bibi Indira Gandhi aliamrisha wanajeshi kuingia mle kwa kisingizio cha kusaka makalasinga wapinzani ambao inasadikiwa walikuwa wameficha silaha mle, wanajeshi wakaingia na viatu kwenye mskiti wa dhahabu huku wengine wakivuta na sigara, katika patashika ile wanajeshi walikufa na masingasinga wengi waliuwawa, baadae kilichompata Bibi Indira Gandhi nafikiri wana JF home of great thinkers wengi mnakifahamu.

  Turudi kwenye chama chetu cha CCM, Utamaduni uliojengeka katika chama hiki ni kulindana,huyu ni mwenzetu, chama ni chetu, uwenzetu huo ndio uliowavutia wengi wenye ubaya na inchi yetu kuingia mle na hatimae kugombea uongozi kwa nia ya kupata immunity ya kubughuziwa na polisi, kupata passport nyeusi (diplomatic) si kwamba wanakipenda sana chama bali kivutio ni ile hali ya kulindwa na u-wenzetu, walikifanya chama chetu kama kichaka cha kujificha ili maovu yao yasifuatiliwe sana iishie tu huyu ni mwenzetu.

  Waheshimiwa wafuatao waliingia kugombea uongozi CCM kwa falisafa hiyo.


  1. Mh. Rostam Aziz, kumbe fisadi anapaosport ya inchi mbili
  2. Mh. Idd Simba hana hata chembe ya uaminifu
  3. Mh. Getrude Rwakatale na ulokole wote ule kumbe mwizi wa Umeme wa Tanesco
  4. Mh. Mohamed Dewji na kutoa kote misaada Singida kumbe alikuwa anawinda atuibie kiwanja cha iliyokuwa GAPEX
  5. Christopher Ole Sendeka na kupiga kelele kote kule kuwapigia mafisadi kumbe kuwadi wa mafisadi
  6. Mh. Aden Rage hana hata chembe ya kuitwa kiongozi mwaminifu,fuatilia record zake za nyuma.

  Na wengine wengi kama hao.

  Sasa jana wakati wa kupitisha bajeti ya nishati na madini msikiti wa dhahabu wa CCM ulivamiwa,waovu wote wakajulikana na wataendelea kujuliukana, Mather Spika akaamrisha majeshi yake yaufumue msikiti huo ili wote waovu wanaokimbilia humo wakamatwe. Kamati ya bunge ya Nishati na madini, Mh Getrude Rwakatare, Ole Sendeka walikamatwa live,tusubili na wengine watakatwa mda si mrefu. ​


  [​IMG] [​IMG] Ed
   
Loading...