CCM Yatumia ujanja kufanya kampeni kuelekea uchaguzi mdogo mwakani

kilagalila

JF-Expert Member
Nov 8, 2018
320
154
1545832346910.jpeg
Ikiwa kila ifikapo December 25 Waumini wa Dini ya Kikristo Nchini wanaungana na Wakristo Wengine Duniani Kote Kusherehekea Sikuku ya Kuzaliwa kwa Yesu Kristo Ambapo Wananchi Mjini Njombe wametoa Wito kwa Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Humo Kuhakikisha Kuwa wanaendelea Kuisimamia na Kuitetea Serikali ya Awamu ya Tano.

Wananchi hao waliokuwa Wakizungumza na Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe Ndg. Erasto Ngole (Shikamoo Parachichi) Kwa nyakati Tofauti katika Maeneo ya Stendi kuu, Ramadhani, Mjimwema, Na maeneo Mengine Mjini Njombe, Walimweleza Kuwa Wanaimani Kubwa na Serikali yao Inayoongozwa Na Rais Dkt. John Magufuli Chini ya Chama cha mapinduzi CCM Hasa katika Kushughulika na Shida za Wananchi wa kipato cha chini.

Aidha wananchi hao walimpongeza Ndg. Erasto Ngole Ambae ni Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Njombe kwakuwatembelea Wananchi katika Maeneo hayo mjini Njombe nakusikiliza Kero na Maoni yao Juu ya Ushirikiano Mzuri kati ya Chama tawala na Viongozi wa Serikali na kuongeza Kuwa Kiongozi huyo hakujali Msimu wa Sikukuu lakini Aliona ni jambo jema Kukaa na Wananchi na kusikiliza Mawazo yao.

Akiwa katika Uwanja wa Mpira wa Miguu Sabasaba Mjini Njombe Ndg. Erasto Ngole Alishiriki Bonanza la Mpira wa miguu lililowakutanisha Wachezaji wa zamani wa Mchezo Huo Veterans Kutoka Njombe na Makambako Kisha aliwaunga mkono Wachezaji hao kwa kutoa Pesa Kiasi cha Tsh. 100,000/= Kama Zawadi yake kwa wachezaji hao katika Kusheherekea Sikukuu za Christmas na Kuupokea Mwaka mpya 2019.

"Ndg. Wanamichezo Leo Kuanzia Asubuhi nimepita katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wetu wa Njombe lengo nikuzungumza na Wananchi ili kujua namna gani Wanaelewa juu ya Utekelezaji wa Ilani yetu ya Uchaguzi ilani ya CCM Kwa bahati Nzuri watu wetu Wametupongeza Sisi Chama pamoja na Serikali kwa hatua Nzuri tunayoenda nayo ya Kuleta maendeleo Si katika mkoa wa njombe pekee bali katika Nchi yote ya Tanzania,Sasa nikaona nije pia nishiriki Hili bonanza Hapa ambapo kwa leo Ninawachangia Tsh. 100,000/= Kuonesha kuwa Nalitambua hili Tukio lenu". Alisema Ndg. Erasto Ngole katibu Mwenezi CCM Mkoa wa Njombe.

Akiendelea Kuzungumza Na Wadau hao wa Michezo Ndg. Ngole kwaniaba ya Viongozi wengine wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa njombe Alitumia Nafasi hiyo pia Kutoa Salamu za Sikukuu za Christmas na Mwaka mpya kwa Wakazi wote wa Mkoa wa Njombe huku akisema kuwa Mwaka mpya 2019 Ni mwaka wa Uchaguzi Wa Serikali za Mitaa Hivyo wananchi wanatakiwa Kujipanga Kikamilifu ili kutoa Ushindi Mkubwa kwa Chama cha Mapinduzi katika Kila nafasi ya Uongozi.

"Ndugu zangu wananchi na wadau wa Maendeleo katika Mkoa wetu wa Njombe najua Tunausubiri Mwaka mpya kwa Shauku na Shangwe kubwa Nijambo jema sana lakini nivyema tukakumbuka Kuwa mwaka huo mpya 2019 Ndio mwaka Muhimu sana na ndio wakutengeneza Serikali Imara na Madhubuti Kupitia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Hivyo naomba Tujipange ili kupata viongozi Watakao zungumza lugha moja Na Rais Magufuli na Kusikilizwa Kwa Uharaka. Alisisitiza Ndg. Ngole.
 

Attachments

  • IMG-20181225-WA0045.jpg
    IMG-20181225-WA0045.jpg
    94.9 KB · Views: 16
  • IMG-20181225-WA0110.jpg
    IMG-20181225-WA0110.jpg
    87.5 KB · Views: 16
Legally wanatambulika kama wapinzani. Sijui kazi yao iwe nini kama si kupinga!

Ikiwa kiongozi au mwanachama wa CCM (asiye na ajira serikalini) ana haki ya kuitetea serikali basi mpinzani awe kiongozi ama mshabiki anayo haki ya kuponda!
 
CCM haina haja ya kufanya kampeni kwa Tanzania kwa sasa ni nchi ya chama kimoja wananchi karibu wote wanaipenda ccm
Jidanganyeni wenyewe kwa wenyewe hakuna shida! Yaani ccm inajitekenya ma kucheka yenyewe kiundawazimu! Na bado mtaweweseka sana tu! Laiti mioyo ya mnaodhani wapo upande wenu ingefunguka kama gazeti hakika mngeanguka na kufariki baada ya kuisoma kilichoandikwa humo! Ajira hakuna, kiwanda hata kimoja tu hakuna na pesa hakuna pia na leo mtambe mnapendwa! Labda mnapendwa na marehemu!
 
Back
Top Bottom