CCM yatumia bilioni 3 uchaguzi Igunga....!

Sajenti

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
3,651
412
Chama cha mapinduzi kilitumia shilingi bilioni 3 katika kampeni na mchakato mzima wa uchaguzi katika jimbo la Igunga. Pia helikopta ya chama hicho iliyotumika katika kampeni hizo ililipiwa na Rostam Aziz. Kwa upande mwingie CHADEMA wao walitumia shilingi milioni 400. Source: Gazeti la Mtanzani. My take: Ni hekima gani iliyotumika kwa hawa magamba kutumia 3 bilion kwa uchaguzi wa Igunga tu wakati kuna watanzania wanakosa chakula, akina hospitali hazina dawa, nchi iko gizani eti umeme hakuna?
 
Ukweli ni kwamba ilikuwa ni muhimu kwa CCM kutangazwa washindi katika uchaguzi huu. Dhana ya magamba ingewagawa tena zaidi kama wangeshindwa kushinda katika uchaguzi huu. Sio tu kwamba ingewagawa lakini hata vurugu zingenukia na tungesikia mengi zaidi ya tuliyoyasikia na ambayo tutayasikia hapo mbeleni.
Ilikuwa in kinyang'anyiro cha kufa na kupona lakini jimbo lazima libakie CCM. Bila kutumia fedha walizotumia kugharamia hizo kampeni ingekuwa ni vigumu wao kushinda kirahisi, has ukiangalia kuwa katika Jimbo ambalo upinzani ni kama vile haukuwepo October 2010, Chadema na CCM kuchuana vikali vile. Hakika margin ya ushindi siyo kubwa na inawezekana watu wote 171000 wangejitokeza labda matokeo yangeweza kuwa mabaya zaidi. Vijana wengi hawakupiga kura hasa vijijini. Hata hivyo ushindi ni ushindi uwe mwembamba au mnono ni ushindi ili mradi umetangazwa mshindi. Hongera CCM kwa kulihifadhi Jimbo. Tunaamini kuwa Dr. Kafumu atakuwa liberal na kuyashughulikia maendeleo ya wana igunga wote badala ya kuanza siasa chafu ambazo siyo tunayohitaji wananchi wa Igunga.
 
Ukiona hivyo ujue wananchi wa Igunga wamenufaika..
Kuingiza hizo bilioni tatu kwenye circulation ni neema kubwa sana kwa wana Igunga.
 
MKUU unaongelea circulation ya Igunga ya ya Tz! Ninaamini kama ungekuwepo uwezekano wa kufanya uchambuzi, yumkini campaign managers wametoka na vi-makumi milioni vyao. Wengi wao si wananchi wa Igunga. Igunga yawezekana waliambulia wali...kofia an Tshirt ambazo nazo zinaweza kuwa zilinunuliwa Dar au Dodoma. Pia kwa upande mwingine, kwenye uchumi mdogo kama wa Igunga ukiingiza mihela yote kwa wakati mmoja inamadhara makubwa sana kiuchumi, kwa kuwa almost kila kitu kinapanda bei. Waathirika wakubwa wa janga hili ni kina-Pangu Pakavu Ntilie Nchuzi. Sina hakika kama tunaweza kusema wanaIgunga wamefaidika kwa mihela ya campaignS
Ukiona hivyo ujue wananchi wa Igunga wamenufaika..
Kuingiza hizo bilioni tatu kwenye circulation ni neema kubwa sana kwa wana Igunga.
 
Ukiona hivyo ujue wananchi wa Igunga wamenufaika..
Kuingiza hizo bilioni tatu kwenye circulation ni neema kubwa sana kwa wana Igunga.

naamini kuna watu mnalipwa/kunufaika kwa namna yoyote ile kuitetea ccm hata pale inapokosea
 
Ukweli ni kwamba ilikuwa ni muhimu kwa CCM kutangazwa washindi katika uchaguzi huu. Dhana ya magamba ingewagawa tena zaidi kama wangeshindwa kushinda katika uchaguzi huu. Sio tu kwamba ingewagawa lakini hata vurugu zingenukia na tungesikia mengi zaidi ya tuliyoyasikia na ambayo tutayasikia hapo mbeleni.
Ilikuwa in kinyang'anyiro cha kufa na kupona lakini jimbo lazima libakie CCM. Bila kutumia fedha walizotumia kugharamia hizo kampeni ingekuwa ni vigumu wao kushinda kirahisi, has ukiangalia kuwa katika Jimbo ambalo upinzani ni kama vile haukuwepo October 2010, Chadema na CCM kuchuana vikali vile. Hakika margin ya ushindi siyo kubwa na inawezekana watu wote 171000 wangejitokeza labda matokeo yangeweza kuwa mabaya zaidi. Vijana wengi hawakupiga kura hasa vijijini. Hata hivyo ushindi ni ushindi uwe mwembamba au mnono ni ushindi ili mradi umetangazwa mshindi. Hongera CCM kwa kulihifadhi Jimbo. Tunaamini kuwa Dr. Kafumu atakuwa liberal na kuyashughulikia maendeleo ya wana igunga wote badala ya kuanza siasa chafu ambazo siyo tunayohitaji wananchi wa Igunga.
..Unadhani kuhofia mpasuko wa CCM kama wangeshindwa uchaguzi wa Igunga ni issue? Huenda basi hata hizo 3bn walizitumia kwa hira ili kulazimisha ushindi. Kiukweli mimi kwa maoni yangu hakuna mwana-magamba ambaye anaweza kusimama aka-justify matumizi ya hizo pesa ukizingatia hali halisi ya Tanzania kwa sasa. Lakini kwa kuwa magamba siku zote wako tayari hata kama roho za watu zipotee ili wao washinde hizi chaguzi basi na iwe hivyo. Lakini ole wao litakapowageukia hili vumbi kamwe hawataona tena mwanga machoni mwao!! Siwapendi kabisa Magamba!!
 
Hizo pesa wangejenga nyumba za walimu,kuboresha madarasa ya shule na madawati, zahanati kila kata, maji safi kila kata nk...kifupi igunga ingekua neema tu tena na chenji ingebaki....maana millioni elfu tatu sio mchezo
 
enyi wana jf mliojaliwa kusoma vizuri; tengenezeni hiyo hesabu tumpe okampo ahaingaike na haya magamba, tunakwisha tukiwa tunaona.
 
doh......ebwana sio mchezo...
Alafu iyo gap ya matumizi ya cdm na cccm haiendani na gap ya matokeo..
Hahahahahahahaha magamba wanatia aibu nyie....
 
nina maashaka na uelewa wako kiakili, umeishia kidato gani mkuu? kama umepita chuo basi ulikuw amdesaji mkubwa na ukaambulia makarai
hatutakaa tuendelee hata mataifa ya nche wanashangaa sana, zingetumika milioni 200 zingetosha hizo nyingine zikakarabati barabara za igunga,kujenga hops,mshule, kuwapa wanafunzi vitabu na madawati. ushabiki wa kijinga huu.wamenufaikaje na hizo hela??? magamba hawana akili

Ukiona hivyo ujue wananchi wa Igunga wamenufaika..
Kuingiza hizo bilioni tatu kwenye circulation ni neema kubwa sana kwa wana Igunga.
 
nina maashaka na uelewa wako kiakili, umeishia kidato gani mkuu? kama umepita chuo basi ulikuw amdesaji mkubwa na ukaambulia makarai
hatutakaa tuendelee hata mataifa ya nche wanashangaa sana, zingetumika milioni 200 zingetosha hizo nyingine zikakarabati barabara za igunga,kujenga hops,mshule, kuwapa wanafunzi vitabu na madawati. ushabiki wa kijinga huu.wamenufaikaje na hizo hela??? magamba hawana akili
Tatizo hujui garama za uchaguzi..
Chadema unaowasapot wenyewe wametumia zaidi ya hiyo 200 uliyotaja.
 
Kama ni kweli kuwa CCM ilitumia 3biln, CHADEMA 400Mln na CUF 150Mln...

CCM wamepata kura 26,484, CHADEMA kura 23,286, CUF kura 2,104....

Using the Mathematics concept, which most run away!

CCM-3,000,000,000/26,484=113,275/=

CDM-400,000,000/23,286=17177/=

CUF-150,000,000/2,104=71,292/=

In summary!! Hehehhehee

CCM imegharamikia kura moja kwa tsh 113,275/=

CDM imegharamikia kura moja kwa tsh 17,177/=

CUF imegharamikia kura moja kwa tsh 71,292/=

Kila mmoja anajionea, Mathematics never lie!!
 
Hivi hizo pesa zilizotumika na vyama vyote ingetumika kutatua matatizo ya Igunga mambo yangekuwa mazuri zaidi..
 
Ukiona hivyo ujue wananchi wa Igunga wamenufaika..
Kuingiza hizo bilioni tatu kwenye circulation ni neema kubwa sana kwa wana Igunga.
Wakati mwingine hata kukujibu haisaidii! ukishakuwa poyoyo ni poyoyo tu!!
 
Wote walioichagua ccm igunga mmewaponza wanaigunga woote, kwa maana hamna haki ya kumdai maendeleo kafumu/ccm chochote maana uongozi wake kaununua kwa pesa! hivyo pesa yake irudi kwanza na faida! Kweli mchuma janga hula na nduguze.
 
Kama ni kweli kuwa CCM ilitumia 3biln, CHADEMA 400Mln na CUF 150Mln...

CCM wamepata kura 26,484, CHADEMA kura 23,286, CUF kura 2,104....

Using the Mathematics concept, which most run away!

CCM-3,000,000,000/26,484=113,275/=

CDM-400,000,000/23,286=17177/=

CUF-150,000,000/2,104=71,292/=

In summary!! Hehehhehee

CCM imegharamikia kura moja kwa tsh 113,275/=

CDM imegharamikia kura moja kwa tsh 17,177/=

CUF imegharamikia kura moja kwa tsh 71,292/=

Kila mmoja anajionea, Mathematics never lie!!
Big says thank you very much for this useful post.
 
Ukiona hivyo ujue wananchi wa Igunga wamenufaika..
Kuingiza hizo bilioni tatu kwenye circulation ni neema kubwa sana kwa wana Igunga.

Nasikitika sana kuona unaongea maneno ya kijinga kama hayo,wana Igunga wamefaidika kwa lipi?fikiria mara 2 zaidi usikurupuke.
 
Ukiona hivyo ujue wananchi wa Igunga wamenufaika..
Kuingiza hizo bilioni tatu kwenye circulation ni neema kubwa sana kwa wana Igunga.

mmmh! tukiwa na watanzania 2 kama wewe kwenye serikali yetu, tumekwisha!.
 
Back
Top Bottom