Awali ya yote natanguliza MAPENZI yangu kwa CCM. Nimesikitishwa na mwenendo wa kampeni zinazoendelea katika kata ya Mianzini, Mbagala kutakofanyika uchaguzi wa diwani Juni 16, 2013. Jana ilikuwa ni mara ya kwanza kuhudhuria mkutano wa kampeni tangu kipenga kimefunguliwa cha uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata husika, mkutano jana, Juni 9, 2013 ulifanyika katika kiwanja cha Mbagala Zackhem ambako mambo yafuatayo yalijitokeza:-
1. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa DSM, Ndugu Madabida alikuwa mgeni rasmi
2. Mbunge wa Kigamboni, Dr. Ndugulile alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha kiti cha udiwani kinabaki CCM
3. Mbunge wa Viti Maalum CCM, mama Zarina Madabida alitia timu.
4. Sehemu kubwa ya maneno ya utangulizi ya MC, watoa hotuba kutoa maneno machafu yenye kejeli kwa Chadema na CUF.
5. Watoto chini ya miaka 15, kutumika kutoa burudani wakiwa wamevaa tshirt zenye kutangaza bia ya KILIMANJARO
Dalili zinaonyesha timu ya kampeni ya Chama chetu haina jipya hivyo waliamua kutumia muda mwingi KUTOA BURUDANI KWA WANANCHI KUPITIA BENDI YA SIKINDE.
Jambo lililosikitisha zaidi ni kitendo cha wakereketwa wengi wa CCM kuonekana wakiburudika na bia katika baa za jirani na eneo la mkutano wakiwa na mavazi ya CCM,hiyo haikutosha mara baada ya mkutano kwisha, zoezi la kunywa bia liliendelea katika baa ya Scorpion iliyoko Mbiku ikiwa ni hisani ya mgombea wa udiwani kupitia CCM bwana Mbwana.
CCM inajua inachokifanya???
- Kuwatumia watoto kwa kampeni wakiwa na sare za TBL ni halali??
- WAfuasi wa CCM kuhudhuria mkutanoi wakiwa na sare huku wamelewa chakari wanatoa taswira gani kwa watoto??
- Madabida na Mkewe kupewa kipaumbele katika kampeni huku wakiwa na tuhuma za kuuza ARV feki ni kumjenga ama kumbomoa mgombea??
- Mgombea (Mbwana) kutoa ofa ya bia kwa wapiga kura ni halali??