CCM yatoka kivingine kampeni za Udiwani Mbagala

MTA1

Member
Jun 1, 2013
89
10
Awali ya yote natanguliza MAPENZI yangu kwa CCM. Nimesikitishwa na mwenendo wa kampeni zinazoendelea katika kata ya Mianzini, Mbagala kutakofanyika uchaguzi wa diwani Juni 16, 2013. Jana ilikuwa ni mara ya kwanza kuhudhuria mkutano wa kampeni tangu kipenga kimefunguliwa cha uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata husika, mkutano jana, Juni 9, 2013 ulifanyika katika kiwanja cha Mbagala Zackhem ambako mambo yafuatayo yalijitokeza:-
1. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa DSM, Ndugu Madabida alikuwa mgeni rasmi
2. Mbunge wa Kigamboni, Dr. Ndugulile alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha kiti cha udiwani kinabaki CCM
3. Mbunge wa Viti Maalum CCM, mama Zarina Madabida alitia timu.
4. Sehemu kubwa ya maneno ya utangulizi ya MC, watoa hotuba kutoa maneno machafu yenye kejeli kwa Chadema na CUF.
5. Watoto chini ya miaka 15, kutumika kutoa burudani wakiwa wamevaa tshirt zenye kutangaza bia ya KILIMANJARO

Dalili zinaonyesha timu ya kampeni ya Chama chetu haina jipya hivyo waliamua kutumia muda mwingi KUTOA BURUDANI KWA WANANCHI KUPITIA BENDI YA SIKINDE.

Jambo lililosikitisha zaidi ni kitendo cha wakereketwa wengi wa CCM kuonekana wakiburudika na bia katika baa za jirani na eneo la mkutano wakiwa na mavazi ya CCM,hiyo haikutosha mara baada ya mkutano kwisha, zoezi la kunywa bia liliendelea katika baa ya Scorpion iliyoko Mbiku ikiwa ni hisani ya mgombea wa udiwani kupitia CCM bwana Mbwana.

CCM inajua inachokifanya???
- Kuwatumia watoto kwa kampeni wakiwa na sare za TBL ni halali??
- WAfuasi wa CCM kuhudhuria mkutanoi wakiwa na sare huku wamelewa chakari wanatoa taswira gani kwa watoto??
- Madabida na Mkewe kupewa kipaumbele katika kampeni huku wakiwa na tuhuma za kuuza ARV feki ni kumjenga ama kumbomoa mgombea??
- Mgombea (Mbwana) kutoa ofa ya bia kwa wapiga kura ni halali??
 
Kaka Ccm ile ya zamani ilishakufa, hii ya sasa ni ya majangili, wezi na wapiga dili tu hayo unayosema kwao ni madogo sana
 
Mkuu jana nilikutana nao hao watoto wamevishwa manguo ya Kilimanjaro Premium Lager hadi sikuamini macho yangu. Hawajaishia hapo tu kwani tulipita pita mitaa ya Kibondemaji na Kilungule tukakutana na baadhi ya wananchi wakatuambia ccm imeshaanza kugawa fedha kwa wapiga kura kuanzia buku mbili hadi tano kadri wanavyomthaminisha mtu, na hilo wanalifanya zaidi kwa akina mama.

Tulifika mahali tukiongea na wananchi wakawa wanatuomba fedha kwani tayari ccm imeshawapa na hivyo wanataka na sisi tuwape fedha. Hii ni hali ya hatari sana kwa ustawi wa jamii. Hata kama tukiwa na taasisi mia mbili za kupambana na rushwa bila kuwadhibiti viongozi wa ccm itakuwa ni kazi bure.
 
mbona huwa sina bahati ya kukutana nao nami nichukue sukari ama 5000/=
 
Kula ccm kura kwa chadema.
Fanyeni kama sisi Arumeru mashariki tulivyowamaliza ccm na walikuja na fedha zakutosha na tukawamaliza katika sanduku la kura.
 
Kilimanjaro Premium Larger ilidhamini kampeni za ccm mbagala?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
mKUU Mungi hilo ni swali la msingi sana ambalo tunapaswa kujiuliza. Mimi nimewashuhudia watoto wadogo wa kadri ya miaka 6-10 wakiwa wamevishwa tshirts za Kilimanjaro Premium Lager katika mkutano wa ccm, watoto hao walikuwa wakitoa burudani katika mkutano huo uliokuwa umedoda sana, na wakati huo huo wanaccm pamoja na wananchi wachache waliohudhuria wakijinywea bia za bure walizokuwa wamepewa offer na mgombea wa ccm.
 
Last edited by a moderator:

Duh hili nilikutana nalo jana kwenye mkutano wa kampeni kata ya kimandolu arusha wahudhuriaji wengi wakiwa wamevaa t-shirt za kilimanjaro nikadhani ni zile promotion za kili nami nikapaki nicheki wanenguaji mh nilikuwa disapointed kweli kukuta ni watoto
 
Last edited by a moderator:
ILI SISIM IPATE WATU KWENYE MIKUTANO YAKE LAZIMA YAFUATAYO YAWEPO AMA YOTE AU BADHI YAKE:
1. Vikundi vya burudani,kama TOT,Diamond,Marlow,ZE COMEDY.....Msondo etch
2. Lazima watu watajichana mapilau na makuku + Mabia mengi na mavileo mengine
3. Lazima Watu wataondoka mkutanoni na buku kadhaa wa kadhaa...mf buku 5,000,7,000 na hata 10,000
4.Tshirts,kanga kofia,n.k zitagawiwa kama njugu...si unajua kuna watanzania wanavaa ngu moja mwezi mzima sasa wakipata tshirt,gauni,kanga ya bure awanaona wamefikaaaa
5. Ahadi kibao zitatolewa.......anaweza kuja hata waziri kuthibitisha kuwa ahadi hizo ni za kweli...lakini mwisho wa siku hushia hewani
6. Matusi kwa wapinzani..........( Mnamkumbuka Mzee wa Mtera...Lusihinde! kama haamjui kutukana shule ipo pale!)
 
Awali ya yote natanguliza MAPENZI yangu kwa CCM. Nimesikitishwa na mwenendo wa kampeni zinazoendelea katika kata ya Mianzini, Mbagala kutakofanyika uchaguzi wa diwani Juni 16, 2013. Jana ilikuwa ni mara ya kwanza kuhudhuria mkutano wa kampeni tangu kipenga kimefunguliwa cha uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata husika, mkutano jana, Juni 9, 2013 ulifanyika katika kiwanja cha Mbagala Zackhem ambako mambo yafuatayo yalijitokeza:-
1. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa DSM, Ndugu Madabida alikuwa mgeni rasmi
2. Mbunge wa Kigamboni, Dr. Ndugulile alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha kiti cha udiwani kinabaki CCM
3. Mbunge wa Viti Maalum CCM, mama Zarina Madabida alitia timu.
4. Sehemu kubwa ya maneno ya utangulizi ya MC, watoa hotuba kutoa maneno machafu yenye kejeli kwa Chadema na CUF.
5. Watoto chini ya miaka 15, kutumika kutoa burudani wakiwa wamevaa tshirt zenye kutangaza bia ya KILIMANJARO

Dalili zinaonyesha timu ya kampeni ya Chama chetu haina jipya hivyo waliamua kutumia muda mwingi KUTOA BURUDANI KWA WANANCHI KUPITIA BENDI YA SIKINDE.

Jambo lililosikitisha zaidi ni kitendo cha wakereketwa wengi wa CCM kuonekana wakiburudika na bia katika baa za jirani na eneo la mkutano wakiwa na mavazi ya CCM,hiyo haikutosha mara baada ya mkutano kwisha, zoezi la kunywa bia liliendelea katika baa ya Scorpion iliyoko Mbiku ikiwa ni hisani ya mgombea wa udiwani kupitia CCM bwana Mbwana.

CCM inajua inachokifanya???
- Kuwatumia watoto kwa kampeni wakiwa na sare za TBL ni halali??
- WAfuasi wa CCM kuhudhuria mkutanoi wakiwa na sare huku wamelewa chakari wanatoa taswira gani kwa watoto??
- Madabida na Mkewe kupewa kipaumbele katika kampeni huku wakiwa na tuhuma za kuuza ARV feki ni kumjenga ama kumbomoa mgombea??
- Mgombea (Mbwana) kutoa ofa ya bia kwa wapiga kura ni halali??

huu nao ni ugaidi.weka picha acha uzushi na uongo uliotukuka
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom