Elections 2010 CCM yatoa tamko kuhusu kitendo cha wabunge wa CHADEMA

Tusijidanganye. CCM know what they are talking about.
Itakuwa vigumu kwa wabunge wa Chadema kufanya kazi bungeni iwapo chama chao hakiitambui serikali inayotawala.
Cha ajabu ni kwamba walishaapa kuilinda katiba ambayo ndiyo iliyomweka Rais wasiyemtambua madarakani.
Motion inayopelekwa na CCM itapita na wabunge watafukuzwa bungeni. Take my word.

Mnaojiita wasomi, weledi, bla bla ... hamlioni hilo?

Liko wazi hata kwa sisi wa kawaida.

CCM wanajua wazi kuwa 72% ya watanzania wapo nyuma ya Chadema. Kama wanajidanganya wameweza kudhibiti effects za uchakachuaji basi wajaribu kufanya wanayoyafanya maana hapo ndipo hasa CHADEMA wanapataka. Tutarajie mgogoro mkubwa wa kikatiba na kisheria. Siku zote demonstration haiwezi kufanikiwa mpaka pale yule anayefanyiwa demosntration hiyo kuchukua hatua za kikandamizaji badala ya kutatua tatizo.

Ninanchokiona hapa kuhusu huyu Chiligati ni yale tuliyoyazoea kuwa anajaribu kumshawishi bosi wake ili nae awekwe kwenye kundi la waadilifu aliwataja bosi wake kuwa ndiyo watakaounda serikali. Ila amesahau kuwa kwa kufanya hivyo ndiyo anajiharibia kabisa kwani huyu na Tambwe Hiza ndiyo waanzilishi wa propaganda za UDINI ambazo leo hii bosi wake anapigia kelele huku akijua wazi kuwa ni bad boys alio nao kama kina Chiligati ndiyo architectures wake
 
kuna mambo huwa nikikaa chin na kutafakari huwa nayashangaa sana tena sana. kipindi cha nyuma wakati maalim seif ni mpinzani wa kweli wawakilishi wa baraza kwa tiketi ya chama cha cuf walifanya kama CDM walivyofanya sasa mbona hakuna jambo lolote lililotokea? tena sheria iliwalinda mpaka mwisho. sasa hapo ni kusubiri na Mungu yupo pamoja nasi
 
mtatumia maneno yote lakini ukweli utabaki palepale. To the party chadema is right to the public they are wrong. Wananchi wanajua rais yupo. Lakini rais wa Chadema hayupo. Vikao wanahurudhuria vya nini. Wasuse kila kitu mpaka 2015 tutawaelewa kweli hawana serikali. Wabunge wametumwa kuwakilisha wananchi si chama. Tatizo la JF ni kutaka kuona kila mtu anasurpot chadema whis is imposible.

wee !! rudi darasa la ngumbaru... ndo tabu ya elimu ya shule za kata za ccm hizi!!
 
Hivi kwa nini Watanzania hatujifunzi hata walau kwa jirani zetu Kenya Lakini je bunge lina mamlaka ya kumfukuza mbunge ambaye alitoka wakati rais analihutubia bunge? Je kama uliapa kwa katiba iliyopo wakati unaingia bungeni huwezi kuleta hoja ya kubadili katiba wanasheria mtusaidie
 
Tusijidanganye. CCM know what they are talking about.
Itakuwa vigumu kwa wabunge wa Chadema kufanya kazi bungeni iwapo chama chao hakiitambui serikali inayotawala.
Cha ajabu ni kwamba walishaapa kuilinda katiba ambayo ndiyo iliyomweka Rais wasiyemtambua madarakani.
Motion inayopelekwa na CCM itapita na wabunge watafukuzwa bungeni. Take my word.

Mnaojiita wasomi, weledi, bla bla ... hamlioni hilo?



Liko wazi hata kwa sisi wa kawaida.

Unauhakika na unachokisema? Na wewe ni mmoja kati ya mbumbumbu omba kuelimishwa.
 
Ole wao!
Basi wakubali kwamba walichakachua matokeo then tufanye yafuatayo;
1.marekebisho ya katiba kikiwemo kifungu kile kitakocho tengua matokeo potofu ya uchaguzi.
2. Tuchague (sio kuteua) Tume huru ya uchaguzi ambayo itakuwa independent na iongozwe na watu watakaokuwa wazuri na wazoefu wa kufafanua vifungu vya sheria na katiba ya Nchi.
3.wasimamizi wa uchaguzi majimboni wasiwe Wakurugenzi wa wilaya kama ilivyosasa.
4. Tuchague kiongozi mkuu wa TAKUKURU na aape kuwajibika kwa masrahi ya taifa na ikithibitika kama ameenda kinyume na utendaji wa ofisi kwa kumpendelea mtu yeyote yule basi anyongwe mpaka kufa.
Eventually the NEC will declare a call for the General Election.

Hapo kwenye nyekudu UMEWAZA KAMA Captain CHILIGATI (captain wa mtumbwe uliotoboka MV CCM), kwa kuwa ni kitenmgo kinachohitaji mtu kwa misingi ya professionals & expiriences, then WATU WAOMBE KAZI KWA KUTUMA CV ZAO na zipitiwe, na ateuliwe na bunge ILI AWAJIBIKE KWENYE BUNGE KWA KUWA PALE KUNA MITAZAMO TOFAUTI ndo atatia akili. Sasa wewe unataka UMCHAGUE wewe na nani? Kivipi? uitishwe uchaguzi??
 
Tusijidanganye. CCM know what they are talking about.
Itakuwa vigumu kwa wabunge wa Chadema kufanya kazi bungeni iwapo chama chao hakiitambui serikali inayotawala.
Cha ajabu ni kwamba walishaapa kuilinda katiba ambayo ndiyo iliyomweka Rais wasiyemtambua madarakani.
Motion inayopelekwa na CCM itapita na wabunge watafukuzwa bungeni. Take my word.

Mnaojiita wasomi, weledi, bla bla ... hamlioni hilo?

Liko wazi hata kwa sisi wa kawaida.

Kishongo, your word on this issue is not worth a pinch of salt.

Wabunge wa CCM hawawezi, narudia HAWAWEZI, kuwafukuza wabunge wo wote hata wa kwao wao CCM kutoka Bungeni.

Chama kinaweza kumfukuza uanachama mbunge wake na kumfanya apoteze sifa za kuwa mbunge na hivyo kupoteza ubunge wake.

Mahakama inaweza kutengua, kama kuna valid petition kuhusu uchaguzi wake, ushindi wa mbunge yo yote CCM, CHADEMA, CUF na kumfanya apoteze sifa ya kuwa mbunge.

Bunge halina nguvu, utaratibu wala kanuni ya kuweza kumfukuza ubunge, mbunge yoyote. Kikubwa sana Bunge linaweza kufanya ni 'kumsimamisha' kuhudhuria kikao cha bunge mbunge au wabunge waliokiuka kanuni za bunge.


Na hakuna kanuni inayosema kuwa kila mbunge ni lazima awe bungeni wakati Rais au kiongozi yeyote anahutubia.

Ila kuna kanuni inayowaruhusu wabunge aidha wa chama kimoja au vyama mbali mbali kutoka nje ya ukumbi wa bunge kama wanataka kujadiliana jambo miongoni mwao, bila kuwahusisha wengine. CCM imeitumia sana hii kanuni kuwakutanisha wabunge wake wote wa CCM kama wanakabaliwa na mjadala mgumu (nadhani ushawahi kusikia kuwa wabunge wa CCM wakikaa kama kamati ya wabunge).

Hii ndiyo inaweza kuwapa kiburi na jeuri wabunge wa Chadema, kwani hakuna mipaka wala nafasi ya wakati gani wa kukutana. Wanaweza hata kukutana nje ya bunge wakati Kikwete anahutubia.......and that's what happened.
 
mtanukuu vingi tu. Mkuwa walokole wanaochukua verse moja na kuwa sera ya dini. To go out means there is no goverment to chadema. Wakienda bungeni ni kufuata posho tu. chadema wanaojua na kutokutaka aibu hiyo hakuwafuata posho namely Ndesa, zitto, shibuda, mdee, lucy etc.

Hivi kweli na wewe huwa unaenda mbele za watu na unajiona ni binadamu aliyepewa ubongo na Mwenyezi mungu !!??

Dogo, grow up ! you are plain stupid !!
 
Unajua wabunge wa CCM ni wa chache sana wanaozijua sheria na kanuni za bunge, ukimuondoa Sitta, Harrison Mwakyembe na wengine wachache sana ndiyo wanakubalika kuwa wanazisoma sheria hizo wengine ni wauza sura, ni watu wa vijiweni wanaongea lolote litokalo kinywani wakidhani watanzania wa leo ni wale wa 1995.Chiligati ni mmoja wa vilaza ndani ya CCM press conference yake kapotezea muda waandishi hana jipya.Nahisi kina mwakyembe watamuambia baadae kuwa ametokota hakuna adhabu hapo Chiligati ni mmoja ya wabunge waliogawiwa masanduku ya kura za wizi kama Mahanga lazima alopoke kutetea ujambazi wao.HANA MPYA .Chadema haina kipimo bungeni hakuna wa kupammbana na figures zile.CHILIGATI ARUDI CHUONI AKANOE UBONGO KWANZA
Mwenye elimu yake atuwekee hapa tumpime. Yawezekana alisomea kwenye zile ofisi za Lumumba
 
Source; TBC newz

Chama Cha Mapinduzi,
CCM, kinaandaa tamko
na mkakati rasmi
kuhusiana na kitendo
cha Wabunge wa Chama
Cha Demokrasia na
Maendeleo, CHADEMA,
kuondoka katika ukumbi
wa Bunge hapo jana
wakati Rais alipokuwa
akilifungua bunge hilo
rasmi kwa ajili ya vikao
vya awamu ya 2010 -
2015.
Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa CCM, Kapteni
mstaafu John Chiligati
amekutana na waandishi
wa Habari leo huko
Dodoma na kusema CCM
inapingana na hatua ya
Wabunge wa CHADEMA
kuondoka Bungeni.
Amesema kwamba
chama chake kitapeleka
tamko rami Bungeni ili
ikiwezekana kwa mujibu
wa Sheria, Kanuni na
Taraibu za Bunge, basi
Wabunge wa CHADEMA
waondoshwe katika
ushiriki wa shughuli na
vikao vyote vya Bunge
hadi hapo
watakapotambua kuwa
aliyechaguliwa kwa
asilimia nyingi zaidi
katika uchaguzi uliopita
ni Jakaya Mrisho Kikwete
na ndiye Rais halali wa
Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
 
Nchi hiI sijui ujinga WETU utapungua lini? Suala la Wabunge wa CHADEMA kutoka bungeni mimi nalitazama kama jambo ambalo lipo katika madaraka ya spika wa bunge. Hivyo ninashangaa watu wanaotaka kuwalaumu walichofanya wabunge wa CHADEMA kama lina tatizo bila kumhoji spika. Kwa mantiki hiyo spika kama anajua kuwa anahusika katika jambo hilo alitakiwa kufanya yafuatayo:
1. Wakati wabunge wa CHADEMA wanatoka nje spika alitakiwa kutumia kanuni husika (kama ipo) ili kutoa maelezo kama suala hilo lilistahili adhabu.
2. Mbunge yeyote angeinuka na kuomba mwongozo wa spika juu ya jambo hilo.
3. Hata kama wakati wabunge wanatoka nje spika hakupata nafasi ya kutoa ufafanuzi, basi angetoa ufafanuzi kabla ya kuahirisha kikao cha siku ile.
3. Suala lilihusu madaraka ya spika, hivyo kati wote wanaotoa maelezo na shutuma bila kumhusisha spika ni kukosa dira na ndiyo maana huko mbele ya safari tutashangaa mambo mengi yakitokea.

Hivyo, Chiligati kama mtu wa propaganda wa CCM kutolea maelezo suala la wabunge wa CHADEMA kutoka nje haitatusaidia kitu zaidi ya kusikiliza propaganda. Chiligati kama anafahamu kanuni za bunge anapozunzia suala hilo nje ya bunge wakati muda muafaka ulikuwa pale bungeni kwanini hakufanya hivyo.

Kwa Tanzania watu kuingilia madaraka ya watu wengine imekuwa kitu cha kawaida. Tukirudi nyuma wakati wa kampeni, kuliibuka malalamiko toka CHADEMA kuwa mgombea wa urais wa CCM kufanya kampeni hadi saa moja usiku. Msajili wa vyama aliliingilia hilo na kutoa maelezo kuwa kwa hali ya jiografia ya nchi hii wakati mwingine saa moja bado ni mchana. Akahitimisha kuwa vyama walishakubaliana kuongeza muda wa kampeni hadi saa moja jioni. Baada ya siku chache Tume ya uchaguzi ikakana kuwa muda kuongezwa na wakadai kuwa masuala ya uchaguzi hayapo chini ya mamlaka ya Msajili wa vyama. Hata hivyo mgombea wa CCM wala hakuonywa wala msajili hakuwajibishwa kwa kazi hiyo ya kuingilia wajibu wa vyombo vingine.

Swali langu ni kuwa Chiligati alipoongelea suala lililotokea bungeni aliongea ili kumsaidia spika? hizo kanuni anazodai kuzitumia kuwaadhibu wabunge wa CHADEMA watazitumia kama CCM kwa maana ya chama au kama mbunge? Na kama zipo ni zipi?
 
Haya yalitarajiwa na nina imani kabisa kwamba Chadema watanyang'anywa hadhi ya kuongoza upinzani Bungeni.

Kwanza hali itakuwa mbaya sana kwa Chadema Bunge litakapoanza kujadili Hotuba ya JK.
Watajikuta katika wakati mgumu wa kuwepo Bungeni wakati wa majadiliano ya hotuba waliyoisusia.

Wakisusa kuwepo wakati wa mjadala huo ni sawa na kujipalia makaa zaidi.

Tulishauri tukapuuzwa. 'Negative implications' tulizokuwa tunazitolea angalizo ndio hizi sasa.
Umesahau kwamba hali itakuwa mbaya kwa Kikwete na serikali yake maana nchi nzima itawaka moto. Amini usiamini atakuwa katupa njiti ya kiberiti kwenye petrol na hakuna..... I repeat hakuna wa kuuzima! Na this might be the end of your dominance of this country's politics
 
Ninachofurahi tu ni kwamba jiwe limegonga penyewe Chadema cool down waacheni wasambaze habari wenyewe wamesahau asubuhi walikuwa wanasema hakuna media coverage sasa wao ndio wamekuwa coverage yenyewe kweli akili ni nywele.
 
hahahahaha uwiii I love my country hivi tutafika kwa mpango huu!.....how is the participatory democracy applied kwenye vyama vingi in Tanzania
 
Tusijidanganye. CCM know what they are talking about.
Itakuwa vigumu kwa wabunge wa Chadema kufanya kazi bungeni iwapo chama chao hakiitambui serikali inayotawala.
Cha ajabu ni kwamba walishaapa kuilinda katiba ambayo ndiyo iliyomweka Rais wasiyemtambua madarakani.
Motion inayopelekwa na CCM itapita na wabunge watafukuzwa bungeni. Take my word.

Mnaojiita wasomi, weledi, bla bla ... hamlioni hilo?

Liko wazi hata kwa sisi wa kawaida.

kwa iyo kishongo unaona hamna haja yoyote ya kuwa na mabadiliko na kuwa na katiba mpya? Pia hamna haja ya kuwa na tume huru? Unasema ccm inawezapost motion kuwaondoa chadema bungeni,ni kwa kipengele kipi au kanuni ipi ktk bunge ambako chama tawala kinapewa mamlaka ya kuleta motion kama iyo? Au ni kwa kutumia mamlaka ya spika? Hata ivo spika anatoa hadhabu hamfukuzi mtu bungeni. Usikebei tuelezane ukweli wala hatuna ugomvi!
 
Chama Cha Mapinduzi, CCM, kinaandaa tamko na mkakati rasmi kuhusiana na kitendo cha Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, kuondoka katika ukumbi wa Bunge hapo jana wakati Rais alipokuwa akilifungua bunge hilo rasmi kwa ajili ya vikao vya awamu ya 2010 - 2015.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Kapteni mstaafu John Chiligati amekutana na waandishi wa Habari leo huko Dodoma na kusema CCM inapindana na hatua ya Wabunge wa CHADEMA kuondoka Bungeni.

Amesema kwamba chama chake kitapeleka tamko rami Bungeni ili ikiwezekana kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taraibu za Bunge, basi Wabunge wa CHADEMA waondoshwe katika ushiriki wa shughuli na vikao vyote vya Bunge hadi hapo watakapotambua kuwa aliyechaguliwa kwa asilimia nyingi zaidi katika uchaguzi uliopita ni Jakaya Mrisho Kikwete na ndiye Rais halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nimeshindwa kuelewa....
Ina maana Chiligati ameitisha press conference ili kutangaza maandalizi ya tamko?
 
Back
Top Bottom