CCM yatoa ratiba mchakato wa Uteuzi wa wagombea. Vikao kuanza 18 - 23 Mei, 2015

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Chama Cha Mapinduzi kupitia Katibu wake wa Uenezi Ndugu Nape Nnauye kimetangaza ratiba za Vikao vya juu vya Chama hicho kuanzia tarehe 18 mpaka 23 Mjini Dodoma.

Tarehe 18 mpaka 19 Mei Kikao Cha Sekretarieti ya CCM chini ya Katibu Mkuu Ndugu Kinana

Tarehe 20 Mei kutakuwa na Kikao cha Kamati Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti Ndg Jakaya Kikwete.

Tarehe 21 mpaka 22 kutakuwa na Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Ndg Jakaya Kikwete.

Vikao hivyo ambavyo vitafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Makao Makuu Dodoma maarufu kama "whitehouse" vinategemea kujadili ajenda zifuatazo.

1. Kuwasilisha na kujadili ripoti ya hali ya siasa nchini.

2. Ratiba ya mchakato wa uteuzi wa wagombea wa nafasi za udiwani, uwakilishi, ubunge, urais wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

3. Kupitia Rasimu ya Kwanza ya maboresho ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015/2020.

4. Mapendekezo ya uboreshaji wa mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM.

5. Namna ya Ushiriki na Mkakati wa Ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba Mwaka huu.
 
Hahahaa wamechelewa sana japo walikuwa wanatazama upepo, mungu awatangulie japo uzalendo ccm hakuna tena nasi twataka mtu mwenye uzalendo na mwenye uchungu na taifa hili, mwaka huu nimwaka wa wazalendo kushika njia kuu kuliokoa taifa. MUNGU WALINDE WAZALENDO WOOTE
 
5. Namna ya Ushiriki na Mkakati wa Ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba Mwaka huu.[/QUOTE said:
hapa ni mkakati wa kuiba fedha ya umma kwa ajili ya kutoa rushwa/takrima kwenye uchanguzi
 
Natamani nilale niamke tayari uchaguzi umefanyika na tuna rais mpya kwa jinsi ninavyochukia hekaheka za kampeni
 
Naona huu ndo muda wa EL kwenda ujerumani kuchomwa sindano ya kuongeza siku ili awe fit kwa sababu anahitaji concentration ya 100%
 
CCM ni debe tupu kwa sasa haliachj kuvuma! UKAWA mambo yote tunasuka serikali mpya
 
Back
Top Bottom