CCM yatoa mapendekezo 17 yawekwe kwenye katiba mpya

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
CCM wameamua kuchukua hoja za wapinzani na kuzifanya zao hasa ambazo zilikuwa zinapigiwa kelele na upinzani. Baadhi ya hoja hizo ni

1: mgombea binafsi hoja ya mch.Mtikila

2: madaraka ya rais. Hoja ya CUF & CHADEMA

3: uteuzi wa mawaziri na madaraka ya waziri mkuu. Hoja ya CHADEMA

4..........

5..........

My concern

CCM wanaona jahazi linazama na wanachukua hoja za upinzani na kufanya zao ikiwemo hoja ya katiba mpya
 
Sasa hivi ni kwamba Wapinzani ndio wanaoongoza hii nchi kwa remote control baada ya Magamba kushindwa. Ukiangalia hata kubadilisha baraza la Mawaziri ni baada ya tishio la kupiga kura ya kutyokuwa na imani na Waziri mkuu.
 
Waziri wao wa sheria na AG si walisema katiba ya sasa ni bora sana na CCM haikuwapinga sasa haya yanatoka wapi tena? Kweli maajabu ndani ya CCM hayaishi.
 
Kwani tuko kwenye kushindania umiliki wa hoja au kujenga nchi? Kama hoja ina manufaa basi itekelezwe tusukume gurudumu la maendeleo mbele.
 
Kwani tuko kwenye kushindania umiliki wa hoja au kujenga nchi? Kama hoja ina manufaa basi itekelezwe tusukume gurudumu la maendeleo mbele.

Shida si ya nani shida ya CCM wanatukana mamba kabla ya kuvuka mto. Sera za wapinzani kikiletwa wanatabia ya kuziponda na kusifia chao kibovu cha ajabu wanakuja kutekeleza ya upinzani
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Chama Cha Mapinduzi kama mdau miongoni mwa wenye haki kisheria kutoa maoni kuhusu mabadiliko ya Katiba, leo kimetangaza msimamo wake kuhusu mambo ambayo kinaona kwamba yanafaa kuwemo kwenye mdajala wa katiba mpya.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dar es Salaam, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (CCM), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema mapendekezo ya CCM yapo katika sehemu mbili. Nape alisema moja ya mambo ambayo haihofii kujadiliwa ni uwepo wa mgombea binafsi, akisema ikiwa hilo litapita katika katiba mpya, itakuwa pigo zaidi kwa wapinzani kuliko CCM.

"Sisi CCM hatuhofii hili la mgombea binafsi, kwanza likikubalika wapinzani ndio watakaoumia.. Unadhani kama ingekuwa na mgombea binafsi nani angehamia upinzani?" Nape alisema na kuhoji,
Ifuatayo ni Taarifa Kamili kuhusu tamko hilo la CCM;

Kwakuwa sheria inayosimamia mchakato wa mabadiliko ya Katiba nchini imevipa uhuru vyama vya siasa kushiriki kwenye mchakato wa Mabadiliko hayo ya Katiba. Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Dk Jakaya Mrisho Kikwete, Mei 13, 2012, walifanya semina kuhusu Mwongozo wa CCM katika kushiriki katika mjadala wa Katiba Mpya.

Katika semina hiyo, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa walijadili maeneo ya Misingi Mikuu ya Taifa ambayo yanatakiwa kubaki ndani ya Katiba mpya; na Mambo ambayo hayagusi Misingi Mikuu ya Taifa lakini ni muhimu kwa nchi, mambo ambayo yako wazi kwa mjadala mpana.

Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ilijadili na kukubaliana kuwa wanachama na wananchi kwa ujumla wahakikishe kuwa Misingi Mikuu ya Taifa letu inabaki katika Katiba Mpya itayoandikwa. Misingi mikuu iliyojadiliwa na kukubalika ibaki au iingie katika Katiba Mpya ni pamoja na:

1. Kuwapo kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

2. Muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuwa wa Serikali mbili; Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. Kuendelea kuwapo kwa mihimili mitatu ya Dola (Serikali, Bunge na Mahakama).

4. Kuendelea kuwapo kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

5. Kuendelea kuwapo kwa Umoja wa Kitaifa, Amani, Utulivu, Usawa na Haki.

6. Kufanyika kwa uchaguzi wa mara kwa mara katika vipindi maalumu na kuzingatia haki ya kupiga kura kwa kila mtu mwenye sifa zinazohitajika kwa mujibu wa sheria.

7. Kuendeleza uhifadhi na ukuzaji wa Haki za Binadamu na kuheshimu usawa mbele ya sheria.

8. Kuendeleza sera ya dola kutokuwa na dini rasmi, bali inaruhusu kila mtu awe na uhuru wa kufuata dini anayoitaka mwenyewe.

9. Kuendeleza sera ya serikali kuwa ndiye mmiliki wa raslimali kuu za nchi, hususan Ardhi.

10. Kuendeleza sera ya kuwapo kwa usimamizi madhubuti wa maadili ya viongozi. Kwa kuupa nguvu za kikatiba.

11. Kuimarisha madaraka ya umma.

12. Kuhamasisha Sera ya msingi ya kujitegemea.

13. Kusimamia Usawa wa jinsia na haki za wanawake, watoto na makundi mengine maalumu katika jamii.

14. Kusimamia Hifadhi ya mazingira.

15. Na kuendelea kuwapo kwa Rais mtendaji.

Mambo mengine mengine yaliyobaki, ambayo yanahusu masuala ya uendeshaji wa serikali, wananchi wapewe fursa ya kuchangia
maoni yao kwa kadri kila mmoja anavyoona inafaa kwa kuzingatia maslahi ya Taifa letu.

Mambo hayo ambayo yapo wazi kwa mjadala mpana ni pamoja na haya yafuatayo;-

1. Mambo yanayosababisha kuwapo kwa kero za Muungano zilizopo hususani Orodha ya mambo ya Muungano.

2. Utaratibu wa uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

3. Madaraka ya Rais.

4. Taratibu za uteuzi wa Mawaziri/ Waziri mkuu.

5. Utaratibu wa Uteuzi wa Tume huru ya uchaguzi.

6. Swala la mgombea binafsi katika uchaguzi wa dola.

7. Kuhusu muundo wa bunge/ baraza la wawakilishi na aina ya wabunge/ wawakilishi.

8. Kuhoji mahakamani matokeo ya Uchaguzi wa Rais.

9. Uwepo wa baraza la pili la kutunga sheria.

10. Ukomo wa Idadi ya Wabunge.

11. Mfumo wa mahakama.

12. Nafasi ya Rais wa Zanzibar katika Uongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

NAPE NNAUYE
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi.

Maoni yangu:
Kwenye red: Sababu moja kubwa ya wananchi kutaka katiba iandikwe upya ni ili kupata fursa ya kusema aina ya Taifa wanalotaka kulijenga na mahusiano kati ya wananchi na dola. Katiba ya sasa iliandikwa na watu wachache na ubovu wake tumeona. Sasa kwa nini hawa viongozi wa CCM wanarudia makosa yale yale? Kwa nini wanataka kuwaamulia wananchi aina ya taifa?

Mfano, 'kuwepo kwa muungano" wa aina gani? Au, "kuwepo na serikali mbili" Wapekele hizi porojo Zanzibar.

Kwenye blue: Wanasema hivi "Mambo mengine mengine yaliyobaki, ambayo yanahusu masuala ya uendeshaji wa serikali, wananchi wapewe fursa ya kuchangia"
Maana yake wananchi hawarusi kuchangia kuhusu Muungano au muundo wa serikali?

Kwa kifupi wakubwa wa CCM hawaonekani kujua wananchi wanataka nini!
 
CCM(Chama Cha Mateja) kimetoa mapendekezo 27 ati!!
.
"KUNA MTU AJIFANYAYE NI TAJIRI HUKU HANA KITU, KUNA MTU AJIFANYAYE MASKINI HUKU NI TAJIRI".
 
Katika gazeti la majira leo kuna habari yenye kichwa CCM yaanza Zengwe. Katika habari hiyo CCM kupitia katibu wake mwenezi imeainisha mambo ambayo haitaki wananchi wajadili. Mathalani swala la Aina ya Muungano. Mimi Siungi mkono Sera ya kuvunja muungano ila napingana na CCM kunyima watu uhuru wa kujadili na kuamua. Kama hili jambo litakubalika itamaanisha kuw atume haina Demokrasia. Nazani tume ipokee maoni haya ila wananchi ndo wataamua kama wayakubali ama la!
 
Katika hali ya kuastaajabisha ccm inaonekana dhahiri inataka katiba mpya iwe ya aina inayotaka yenyewe. Kutoa maoni hatukai kabisa lakini kuanza kuweka na wigo wa serilaki ni kosa kubwa sana. Bora wananchi wapewe uhuru wa kuamua kuwa na serikali moja, mbili , tatu au kutokuwa na muungano kabisa
 
Katika hali ya kuastaajabisha ccm inaonekana dhahiri inataka katiba mpya iwe ya aina inayotaka yenyewe. Kutoa maoni hatukai kabisa lakini kuanza kuweka na wigo wa serilaki ni kosa kubwa sana. Bora wananchi wapewe uhuru wa kuamua kuwa na serikali moja, mbili , tatu au kutokuwa na muungano kabisa

Ccm haipaswi kutoa maoni kabisaaa!!! kwa sababu wamekuwa na serikali maisha yao yote, wangekuwa wamefanya marekebisho ya katiba kukidhi matakwa haya wanayoyapendekeza. wana ccm watoe maoni kama raia wa kawaida.
 
Haya wajameni ni mapmbano, kati ya walalahoi na walalaheri. Hivyo bila kusimama kidete tutaburuzwa na hawa mafisadi. Kila mtu alipo atoe elimu kwa umma. Ili watu waweze kuwa na hoja. CCM ni hatari kama nuklia bomu katika huu mchakato.
 
Back
Top Bottom