CCM yatoa maelekezo matatu kwa Serikali, ahueni kwa wakulima wa mahindi nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,890
939
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHATOA MAELEKEZO MATATU KWA SERIKALI, AHUENI KWA WAKULIMA WA MAHINDI NCHINI.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa maelekezo matatu kwa Serikali kuhusu ununuzi wa mahindi ya wakulima, vituo vya kununulia mahindi pamoja na bei ya mbolea nchini.

Maelekezo hayo yametolewa leo tarehe 06 Septemba, 2021 na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Daniel Chongolo Makao Makuu ya Chama Dodoma.

Katibu Mkuu ametoa maelekezo hayo, baada ya Chama kusikia malalamiko ya wakulima kuhusu uhaba wa masoko ya mahindi, ambapo Chama kimeilekeza Serikali kutafuta fedha kwa ajili ya kununua mahindi katika mikoa yenye uzalishaji mkubwa.

"Baada ya maagizo ya Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa katika ziara ya mwezi Julai mwaka huu kwenye mikoa ya Rukwa, Songwe na Mbeya, kuhusu utafutaji wa masoko ya mahindi, NFRA na Bodi ya Mazao Mchanganyiko ilitenga fedha kununua mahindi, na taarifa zilizopo ununuzi unasua sua kutokakana na fedha kuisha, sasa hatuwezi kukaa namna hii wakulima wetu hawana pa kuuza mahindi yao, hivyo maagizo ya chama kwa serikali, watafute fedha popote wanapojua na suala la kununua mahindi liendelee kwenye maeneo yote ya uzalishaji." Ameelekeza Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo.

Aidha, katika Hatua nyingine, baada ya kuwepo kwa malalamiko ya wakulima kuhusu uchache wa vituo vya ununuzi wa mahindi, Chama kimeilekeza serikali kupitia Wizara ya Kilimo, kuongeza vituo vya ununuzi na gharama za usafiri wasibebeshwe wakulima kama inavyofanyika sasa kwa wakulima waliopo pembezoni mwa vituo vya ununuzi.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu ameitaka Wizara ya Kilimo na Wizara ya Fedha na Mipango kukutana haraka kwa ajili ya kuangalia namna ya kupunguza mzigo kwa wakulima baada ya ongezeka kubwa la bei ya mbolea kutoka shilingi elfu 50 kwa mfuko wa kilogram 50 na sasa kupanda mpaka shilingi elfu 80-85 katika nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania kutokana na athari za janga la Uviko 19.

#ChamaImara
#KaziIendelee

AIDHA.......

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeiagiza Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kununua tani 100,000 za mahindi katika Mikoa ya Nyanda za juu Kusini.

Hayo yamesemwa leo September 6,2021 jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa CCM,Daniel Chongolo wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa mwezi wa saba Sekretariet ya Chama cha Mapinguzi ilifanya ziara katika Mikoa ya Rukwa,Songwe na Mbeya ambapo walikutana na changamoto ya wakulima kukosa soko la zao la mahindi.

Amesema mara baada ya ziara hiyo waliiagiza Serikali kununua mahindi hayo ambapo ilitoa zaidi ya shilingi bilioni 14 ambazo zilinunua zaidi ya tani 24,000.

” kwa sasa fedha hizo zimeisha na wakulima wanaendelea kuhangaika kutafuta soko la kuuzia mahindi yao”amesema.

Chongolo ameiagiza Serikali kutoa tena fedha na inunue tani 100,000 za wakulima hao kwani wanazotaarifa kuwa msimu ujao wa kilimo mvua zitakuwa chache.

“Tena kwa bei ile ile ya shilingi 500 kwa kilogramu na wafanye zoezi hilo liwe endelevu kwani mamlaka ya hali ya hewa imesema kuna changamoto katika mvua za vuli mpaka katika mvua za masika hivyo kutakuwa na changamoto ya upatikanaji wa chakula,”amesema Chongolo

Aidha Bw.Chongolo amesema katika ziara hiyo wamejifunza kwamba uchache wa vituo vya kununulia mahindi hivyo ameiagiza NFRA kuweka vituo ambavyo vitakuwa karibu na wakukulima.

“Kuna malalamiko kukatwa fedha katika shilingi 500 tunasema hapana mtu aliyepo Mufindi,Ileje,Mbozi,Nkasi tunataka bei ya mahindi iwe moja kwa wote wa karibu na mbali,”amesisitiza Chongolo.

Hata hivyo Chongolo ameziagiza Wizara za Kilimo na Fedha na Mipango kukutana ili kujadiliana jinsi ya kupunguza bei ya mbolea kutokana na kuwa juu hivyo kumuumiza mkulima.

Amesema kwa sasa bei ya mbolea aina ya Urea imepanda maradufu kutokana na changamoto ya ugonjwa wa Corona ambapo awali ilikuwa shilingi 50,000 mpaka 55,000 lakini kwa sasa ni shilingi 80,000 mpaka 85,000.

“Tunaiagiza Serikali kupitia Wizara ya Kilimo na Wizara ya Fedha na Mipango waanze mchakato wa jinsi ya kuwasaidia wakulima.Nasisitiza Wizara zikutane mapema kuwezesha kupungua kwa bei ya mbolea,”amesema Chongolo

Pia Chongolo amesema kuwa mara baada ya maagizo hayo baada ya wiki mbili wataanza ziara ya kukagua maelekezo hayo.

IMG-20210906-WA0032.jpg

IMG-20210906-WA0029.jpg

IMG-20210906-WA0030.jpg
 
Mmmmh yaani bei ya mbolea imepanda kisa CORONA? mbona bei ya sukari, Madawa ya kilimo bado the same? CCM acheni kuwaona watanzania hamnazo. Mbolea imepandishwa na kodi pamoja na serikali kuondoa misamaha kwenye bidhaa na vifaa vya kilimo.
 
Posho kubwa kubwa na matumizi ya anasa ya serikali, ndio maana mmeleta tozo kwenye simu, mafuta ya kula, gesi na car ⛽ fuel

Serikali ipunguze matumizi ya anasa
 
Ovyoo wanamdidimiza Rais, hilo ni dongo wenye macho jaribuni kuona kwa kina mtagundua, hao ni CCM wanaokwenda against serikali ,wanapitia njia za panya ili kuichafua serikali. Kikinuka waseme serikali haitusikii na hili na lile hayo ni madongo anatupiwa Dada Yule.
 
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHATOA MAELEKEZO MATATU KWA SERIKALI, AHUENI KWA WAKULIMA WA MAHINDI NCHINI.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa maelekezo matatu kwa Serikali kuhusu ununuzi wa mahindi ya wakulima, vituo vya kununulia mahindi pamoja na bei ya mbolea nchini.

Maelekezo hayo yametolewa leo tarehe 06 Septemba, 2021 na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Daniel Chongolo Makao Makuu ya Chama Dodoma.

Katibu Mkuu ametoa maelekezo hayo, baada ya Chama kusikia malalamiko ya wakulima kuhusu uhaba wa masoko ya mahindi, ambapo Chama kimeilekeza Serikali kutafuta fedha kwa ajili ya kununua mahindi katika mikoa yenye uzalishaji mkubwa.

"Baada ya maagizo ya Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa katika ziara ya mwezi Julai mwaka huu kwenye mikoa ya Rukwa, Songwe na Mbeya, kuhusu utafutaji wa masoko ya mahindi, NFRA na Bodi ya Mazao Mchanganyiko ilitenga fedha kununua mahindi, na taarifa zilizopo ununuzi unasua sua kutokakana na fedha kuisha, sasa hatuwezi kukaa namna hii wakulima wetu hawana pa kuuza mahindi yao, hivyo maagizo ya chama kwa serikali, watafute fedha popote wanapojua na suala la kununua mahindi liendelee kwenye maeneo yote ya uzalishaji." Ameelekeza Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo.

Aidha, katika Hatua nyingine, baada ya kuwepo kwa malalamiko ya wakulima kuhusu uchache wa vituo vya ununuzi wa mahindi, Chama kimeilekeza serikali kupitia Wizara ya Kilimo, kuongeza vituo vya ununuzi na gharama za usafiri wasibebeshwe wakulima kama inavyofanyika sasa kwa wakulima waliopo pembezoni mwa vituo vya ununuzi.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu ameitaka Wizara ya Kilimo na Wizara ya Fedha na Mipango kukutana haraka kwa ajili ya kuangalia namna ya kupunguza mzigo kwa wakulima baada ya ongezeka kubwa la bei ya mbolea kutoka shilingi elfu 50 kwa mfuko wa kilogram 50 na sasa kupanda mpaka shilingi elfu 80-85 katika nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania kutokana na athari za janga la Uviko 19.

#ChamaImara
#KaziIendelee

AIDHA.......

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeiagiza Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kununua tani 100,000 za mahindi katika Mikoa ya Nyanda za juu Kusini.

Hayo yamesemwa leo September 6,2021 jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa CCM,Daniel Chongolo wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa mwezi wa saba Sekretariet ya Chama cha Mapinguzi ilifanya ziara katika Mikoa ya Rukwa,Songwe na Mbeya ambapo walikutana na changamoto ya wakulima kukosa soko la zao la mahindi.

Amesema mara baada ya ziara hiyo waliiagiza Serikali kununua mahindi hayo ambapo ilitoa zaidi ya shilingi bilioni 14 ambazo zilinunua zaidi ya tani 24,000.

” kwa sasa fedha hizo zimeisha na wakulima wanaendelea kuhangaika kutafuta soko la kuuzia mahindi yao”amesema.

Chongolo ameiagiza Serikali kutoa tena fedha na inunue tani 100,000 za wakulima hao kwani wanazotaarifa kuwa msimu ujao wa kilimo mvua zitakuwa chache.

“Tena kwa bei ile ile ya shilingi 500 kwa kilogramu na wafanye zoezi hilo liwe endelevu kwani mamlaka ya hali ya hewa imesema kuna changamoto katika mvua za vuli mpaka katika mvua za masika hivyo kutakuwa na changamoto ya upatikanaji wa chakula,”amesema Chongolo

Aidha Bw.Chongolo amesema katika ziara hiyo wamejifunza kwamba uchache wa vituo vya kununulia mahindi hivyo ameiagiza NFRA kuweka vituo ambavyo vitakuwa karibu na wakukulima.

“Kuna malalamiko kukatwa fedha katika shilingi 500 tunasema hapana mtu aliyepo Mufindi,Ileje,Mbozi,Nkasi tunataka bei ya mahindi iwe moja kwa wote wa karibu na mbali,”amesisitiza Chongolo.

Hata hivyo Chongolo ameziagiza Wizara za Kilimo na Fedha na Mipango kukutana ili kujadiliana jinsi ya kupunguza bei ya mbolea kutokana na kuwa juu hivyo kumuumiza mkulima.

Amesema kwa sasa bei ya mbolea aina ya Urea imepanda maradufu kutokana na changamoto ya ugonjwa wa Corona ambapo awali ilikuwa shilingi 50,000 mpaka 55,000 lakini kwa sasa ni shilingi 80,000 mpaka 85,000.

“Tunaiagiza Serikali kupitia Wizara ya Kilimo na Wizara ya Fedha na Mipango waanze mchakato wa jinsi ya kuwasaidia wakulima.Nasisitiza Wizara zikutane mapema kuwezesha kupungua kwa bei ya mbolea,”amesema Chongolo

Pia Chongolo amesema kuwa mara baada ya maagizo hayo baada ya wiki mbili wataanza ziara ya kukagua maelekezo hayo.

View attachment 1927024
View attachment 1927025
View attachment 1927026
Korosho za mkoa mmoja tu ziliwashinda mtaweza mahindi yanayolimwa na kila mtanzania???
 
Back
Top Bottom