CCM yatoa maelekezo kumaliza sintofahamu ununuzi wa mahindi Songea

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
735
476
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimewataka wakala wa chakula NFRA kuweka utaratibu mzuri ili kumaliza sintofahamu iliyopo juu ya ununuzi wa mahindi Manispaa ya Songea kwa kuhakikisha wananchi wote waliokwisha kuorodheshwa Mahindi yao yananunuliwa pamoja na kuongezwa kwa kituo kimoja cha ununuzi wa mahindi ili kuepuka msongamano katika kituo kinachotumika sasa na kuwaondolea wananchi usumbufu.

Hayo yalielezwa na katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka alipotembelea wakala wa Taifa wa chakula (NFRA) na kujionea zoezi la ununuzi linavyoendelea pamoja na kusikiliza wakulima waliokuwa na mahindi nje ya geti la wakala huo.

"Serikali ya CCM inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imekwishatoa shilingi bilioni 7.5 kwa ajili ya ununuzi wa tani elfu kumi na tano katika hatua za awali kwa NFRA hapa Songea Mjini na fedha hizo tayari zipo kwenye akaunti zao, chama kinaitaka NFRA kutoa kipaumbele kwa wananchi wote waliokwisha kuorodheshwa na kuongeza kituo kingine cha ununuzi wa mahindi ili kuepuka huu msongamano na kuwaondolea wananchi wa pembezoni usumbufu." Alisema Shaka.

Shaka aliwataka wananchi kuondoa wasiwasi kwani serikali imepanga mgao wa tani elfu thelathini na tano katika msimu huu kwa mkoa wa Ruvuma. Bado serikali inaendelea kutafuta masoko zaidi nje ya Nchi ili kuhakikisha mahindi yote yanapata soko. Aidha aliwaomba wananchi kuwa wakati ununuzi ukiendelea mahindi zaidi yasishushwe hadi yaliyopo yatakaponunuliwa yote ili kuepuka hasara.

Shaka alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Mheshimiwa Dkt Damas Ndumbaro kwa kuwa mtetezi wa kweli wa wananchi anaowawakilisha. Pia aliwapongeza NFRA kwa kujiongeza na kutafuta ghala la ziada litakalotumika kuhifadhi mahindi tani elfu kumi na tano zitakazonunuliwa sasa.

IMG-20210920-WA0016.jpg
 
CCM YATOA MAELEKEZO KUMALIZA SINTOFAHAMU UNUNUZI WA MAHINDI SONGEA.

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimewataka wakala wa chakula NFRA kuweka utaratibu mzuri ili kumaliza sintofahamu iliyopo juu ya ununuzi wa mahindi Manispaa ya Songea kwa kuhakikisha wananchi wote waliokwisha kuorodheshwa Mahindi yao yananunuliwa pamoja na kuongezwa kwa kituo kimoja cha ununuzi wa mahindi ili kuepuka msongamano katika kituo kinachotumika sasa na kuwaondolea wananchi usumbufu.

Hayo yalielezwa na katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka alipotembelea wakala wa Taifa wa chakula (NFRA) na kujionea zoezi la ununuzi linavyoendelea pamoja na kusikiliza wakulima waliokuwa na mahindi nje ya geti la wakala huo.

"Serikali ya CCM inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imekwishatoa shilingi bilioni 7.5 kwa ajili ya ununuzi wa tani elfu kumi na tano katika hatua za awali kwa NFRA hapa Songea Mjini na fedha hizo tayari zipo kwenye akaunti zao, chama kinaitaka NFRA kutoa kipaumbele kwa wananchi wote waliokwisha kuorodheshwa na kuongeza kituo kingine cha ununuzi wa mahindi ili kuepuka huu msongamano na kuwaondolea wananchi wa pembezoni usumbufu." Alisema Shaka

Shaka aliwataka wananchi kuondoa wasiwasi kwani serikali imepanga mgao wa tani elfu thelathini na tano katika msimu huu kwa mkoa wa Ruvuma. Bado serikali inaendelea kutafuta masoko zaidi nje ya Nchi ili kuhakikisha mahindi yote yanapata soko. Aidha aliwaomba wananchi kuwa wakati ununuzi ukiendelea mahindi zaidi yasishushwe hadi yaliyopo yatakaponunuliwa yote ili kuepuka hasara.

Shaka alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Mheshimiwa Dkt Damas Ndumbaro kwa kuwa mtetezi wa kweli wa wananchi anaowawakilisha. Pia aliwapongeza NFRA kwa kujiongeza na kutafuta ghala la ziada litakalotumika kuhifadhi mahindi tani elfu kumi na tano zitakazonunuliwa sasa.

IMG-20210920-WA0456.jpg
IMG-20210920-WA0457.jpg
IMG-20210920-WA0458.jpg
 
Ruvuma mwaka huu inakadiriwa kuzalisha tan milion 1 kati ya hizo ziada n tani la 3&4 Sasa serikal itanunua tani elfu 30 hiz tani lak 2-lak 3 atanunua Nani

Sawa na 3% ya manunuzi hiz asilimia 97% atanunu nani.

Serikal ifungue mipaka isilete siasa katka zao hili

Zoez lenyewe linamlolongo mwingi had kupata nafas ya kuuza hayo mahindi

Rushwa kujuana ndio vimetawala hapa

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Nchi inakosea vibaya mno kuacha biashara hii nyeti mikononi mwa makada wajinga wa chama hiki.
 
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHATOA MAELEKEZO KUMALIZA MGOGORO UNUNUZI WA MAHINDI SONGEA.

20 Septemba, 2021.

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimewataka wakala wa Taifa wa uhifadhi wa chakula (NFRA) kuweka utaratibu mzuri ili kumaliza sintofahamu iliyokuwepo juu ya ununuzi wa mahindi Manispaa ya Songea kwa kuhakikisha wananchi wote waliokwishakuorodheshwa Mahindi yao yananunuliwa pamoja na kuongezwa kwa kituo kimoja cha ununuzi wa mahindi ili kuepuka msongamano katika kituo kinachotumika sasa.

Hayo yalielezwa na katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka alipotembelea wakala wa Taifa wa uhifadhi wa chakula (NFRA) na kujionea zoezi la ununuzi linavyoendelea pamoja na kusikiliza wakulima waliokuwa na mahindi nje ya geti la wakala huo.

"Serikali ya CCM inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imekwishatoa shilingi bilioni 7.5 kwa ajili ya ununuzi wa tani elfu kumi na tano katika hatua za awali kwa NFRA hapa Songea Mjini na fedha hizo tayari zipo kwenye akaunti zao, chama kinaitaka NFRA kutoa kipaumbele kwa wananchi wote waliokwisha kuorodheshwa na kuongeza kituo kingine cha ununuzi wa mahindi ili kuepuka huu msongamano na kuwaondolea wananchi wa pembezoni usumbufu." Alisema Shaka

Shaka aliwataka wananchi kuondoa wasiwasi kwani serikali imepanga mgao wa tani elfu thelathini na tano katika msimu huu kwa mkoa wa Ruvuma. Bado serikali inaendelea kutafuta masoko zaidi nje ya Nchi ili kuhakikisha mahindi yote yanapata soko. Aidha aliwaomba wananchi kuwa wakati ununuzi ukiendelea mahindi zaidi yasishushwe hadi yaliyopo yatakaponunuliwa yote ili kuepuka hasara.

Shaka alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Mheshimiwa Dkt Damas Ndumbaro kwa kuwa mtetezi wa kweli wa wananchi anaowawakilisha. Pia aliwapongeza NFRA kwa kujiongeza na kutafuta ghala la ziada litakalotumika kuhifadhi mahindi tani elfu kumi na tano zitakazonunuliwa sasa.

IMG-20210920-WA0232.jpg

IMG-20210921-WA0067.jpg

IMG-20210920-WA0235.jpg
 
Waziri wa Kilimo na Serikali yote imeshindwa kushughulikia hili tatizo kubwa sana hadi ipewe maelekezo ya nini cha kufanya.

Nawasalimu kwa jina la divided republic of Tozonia nanyi mnajibu KUDEMKA kuendeleee.
 
Hiki chama cha CCM kilikuwa wapi siku zote kwenda kutatua hii shida. Wanatengeneza mgogoro kwa lengo la kwenda kwa baadaye kutoa maamuzi .
 
Back
Top Bottom