CCM yatimua makatibu wa mikoa sita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yatimua makatibu wa mikoa sita

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 30, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Wednesday, 29 June 2011 21:15 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Boniface Meena

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewaondoa makatibu wake wa mikoa zaidi ya sita nchini ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wake wa kujivua gamba ulioanzishwa mapema mwaka huu.

  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na wahariri wa magazeti ya kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), alipofanya ziara katika makao makuu ya kampuni hiyo Tabata-Relini jijini Dar es Salaam.

  MCL ndiyo inayozalisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti.Katika ziara hiyo, Nape alisema kuwa zoezi hilo la kuwaondoa makatibu litaendelea hadi ngazi ya makatibu wa wilaya ikiwa ni sehemu ya falsafa ya CCM ya kujivua gamba.

  Alisema kujivua gamba ni dhana pana ambayo msingi wake ni kufanya mabadiliko ya kiutendaji na uendeshaji wa CCM kwa ujumla wake na kwamba yapo mambo mengi ambayo yamefanywa katika kutekeleza azma hiyo.

  “Makatibu wa mikoa kama sita au saba hivi wameshaondoka na wengine wamestaafu, ni katika kujivua gamba na tutaenda kwenye wilaya pia,”alisema Nape.

  Alipoulizwa iwapo hao walioondoka katika nyadhifa zao wamestaafu au wameondolewa, Nape alijibu kwa kifupi “vyote kwa pamoja”.

  Alitaja baadhi ya mikoa ambayo makatibu wake wameondolewa kuwa ni pamoja na Shinyanga, Dodoma na Kagera.

  Utaratibu wa kumpata mgombea urais
  Alisema jambo jingine ambalo linafanyika kupitia mchakato huo ni chama hicho kuangalia upya utaratibu wa kumpata mgombea urais ambao utakuwa tofauti na uliokuwa ukitumika katika chaguzi zilizopita.

  “Kuna kamati inashughulikia hilo,” Nape alisema na kuongeza:
  "Pia tunataka tuwe na kamati kama za Bunge ili kutathimini jinsi Serikali inavyotekeleza ahadi ambazo chama kimezitoa ama kupitia wagombea au kwenye Ilani ya Uchaguzi."

  Alisema hatua hiyo itakiwezesha chama hicho kubaini udhaifu uliopo katika utekelezaji wa wajibu wake kwa umma, tofauti na sasa ambapo hakuna mfumo unaowawezesha ufuatiliaji huo.

  Nape alisema kuwa hivi sasa wanafanya mabadiliko katika mfumo wa uongozi katika makao makuu ya chama hicho na ndiyo maana hakuna mawaziri katika safu za juu za uongozi.

  "Hivi sasa hakuna mawaziri, kwani wakati ule walikuwepo mawaziri katika chama ambao ni viongozi, sasa tupo wenyewe na tunakiendesha chama,"alisema na kuongeza:"Hata mfumo wa ndani katika kitengo changu cha Itikadi na Uenezi nako tunafanya mabadiliko na taarifa zitakuwa zikitolewa in details(kwa undani) na si kwa ufupi ili wananchi wazipate."

  Kauli yake kuhusu watuhumiwa ufisadi
  Kuhusu watuhumiwa wa ufisadi na siku 90 walizopewa kujiondoa kwenye nyadhifa wanazoshikilia ndani ya chama, Nape alisema kuwa hakuna suala la siku 90 bali ni vikao vya chama vitakutana na kutoa maamuzi.

  "Siku 90 zinazozungumzwa ni tafsiri ya watu pale mwenyekiti wa chama (Jakaya Kikwete) aliposema tutakutana baada ya miezi mitatu na watu wakatafsiri hivyo, lakini vikao vya NEC ndivyo vinatoa maamuzi,"alisema Nape.

  Alisema kuwa hadi hivi sasa hajui makamu mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa alichozungumza na watuhumiwa hao wa ufisadi baada ya kukutana nao.

  "Sikuwepo kwenye kikao hivyo hadi sasa sijui walizungumza nini, na siwezi kwenda kumtaka Katibu Mkuu anieleze kilichozungumzwa kwani katika vikao vijavyo tutapata taarifa,"alisema Nape.

  CCM na vijana
  Nape ambaye alizungumzia mambo mbalimbali ya chama na Serikali alisema kuwa hali ya CCM kuwasahau vijana iliwaletea matatizo katika Uchaguzi Mkuu uliopita na ndiyo maana hivi sasa chama hicho kimeamua kujivua gamba.

  Aliwaasa vijana walioko vyuoni kwa sasa akisema kuwa siyo vizuri kwao kudhani kuwa siasa ni ajira na kwamba endapo kila mwanafunzi atafikiria hivyo, hali hiyo haitawasaidia kitu.

  Kuhusu takwimu za Serikali na ndani ya CCM, Nape alisema kuwa kuna ugonjwa mkubwa katika utoaji takwimu kwa kuwa takwimu nyingi zimekuwa ni za uongo.

  “Udanganyifu wa takwimu unakuwa kama ni tabia na ipo kwenye chama na kwa Serikali,”alisema.

  Alisema katika kila jimbo takwimu zao zinaonyesha asilimia 70 hadi 80 ya watu ni wanaCCM, lakini inashangaza kwa nini wanapata ushindi wa chini kwenye uchaguzi.

  Wananchi wana haki ya kupata habari
  Alisema kuwa atakuwa tayari kuwasaidia wanahabari kupata taarifa za serikalini ambazo zinakaliwa na maafisa habari au watu wa serikalini kwa kuwa wananchi wana haki ya kupata taarifa kuhusu Serikali yao.

  “Kama kuna taarifa mnaihitaji serikalini nitawasaidia kuipata ili watu wapate habari kwa kuwa, Serikali ni ya CCM na sisi ndiyo viongozi wa chama,”alisema Nape.

  Kuhusu kusherehekea miaka 50 ya Uhuru, Nape alisema kuwa ni vizuri wananchi na wanasiasa wakalinda historia ya taifa kwa kuwa limetoka mbali tangu Uhuru ulipotikana.

  “Ombi langu kwa wananchi ni hili, miaka 50 ya Uhuru ni safari ndefu, nataka dhana ya kwamba hakijafanyika chochote iondoke, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilianzia jengo la Ushirika na leo kipo eneo lake halafu mtu anabeza, hilo haiwezekani,”alisema.

  Alisema kuwa pamoja na vyombo vya habari kufichua maovu ndani ya nchi, lakini ni lazima vilinde historia ya nchi tangu ilipopata Uhuru.

  Akingia kifua gazeti la Mwananchi

  Akizungumzia hali ya CCM na Serikali dhidi ya gazeti hili , Nape alisema kuwa fikra ya kwamba chama chake kinaliona gazeti la Mwananchi kama lina mlengo wa chama kingine haipo na ifutike.

  “Nimekuja kwa mambo matatu, kufahamiana, kufuta dhana ya CCM kulalamikia magazeti na kutoa msimamo wa chama kuondoa dhana kwamba Mwananchi ina mlengo wa chama kimoja cha siasa,”alisema.

  Alisema kuwa ni muhumu CCM ikatambua kuwa gazeti la Mwananchi ni wadau wa mabadiliko katika jamii, hivyo mstari uliopo kati ya CCM na Mwananchi ufutwe.

  “CCM kama taasisi tunajua Mwananchi inaaminika na ina wasomaji wengi kuliko gazeti jingine nchini, pia tunajua linaaminiwa na watu na chama pia,” alisema Nape.

  Akizungumza kuhusu hilo, Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya MCL, Theophil Makunga alisema kuwa Mwananchi kama gazeti lina sera zake na moja ya sera hizo ni kutoegemea upande mmoja.

  Alisema kuwa maamuzi ya habari gani inayofaa kuchapwa kwenye magazeti ya MCL hayafanywi na mtu mmoja bali hupitia vikao vya wahariri vinavyofanyika mara mbili kwa siku.

  “Hata editorial (tahariri) haifanywi na mtu mmoja ni uamuzi wa wahariri,”alisema Makunga.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Good move Nape, keep it up. We stilll have a lot to gain from you and CCM in general.
   
 3. kibakwe

  kibakwe Senior Member

  #3
  Jun 30, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jivueni GAMBA mkianzia na yale MAGAMBA MAKUBWA,siyo vijigamba vidogo
   
 4. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  waanze kwanza kutimua kwanza mafisadi wanaokichafua chama
   
 5. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  hao mmewaonea tu danganya toto hatudanganyikiiii, tunataka muanze kujitimua juu ndo kuja chini na mwaka huu hii remort control ya chadema kazi ipo mpaka 2015 itakuwa kama KANU. After KANU CCM follows
   
 6. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Usanii mtupu, watu wamestaafu mnasema mnajivua gamba, si mseme tu mmeshindwa. Sitashangaa mkisema baada ya siku 90 tumewavua gamba hawa makatibu. Tunasubiri mvue lile gamba gumu RACHEL, we are still counting down the days.

  Halafu Nape hada idadi ya waliostaafu 'jivua gamba' huwajui?, eti sita au saba hivi. Nape tunakusoma.
   
 7. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu hiyo ndio CCM, always changa la macho.

  Makatibu wamestaafu kwa hiari, wao wanajigamba kuvua gamba ... waziri mkuu akifukuzwa kazi na bunge wao wanamwita mstaafu ... tuwaelewe vipi hawa watu?
   
 8. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Hivi nyoka anavyojivua gamba huwa ananza kichwani au mkiani?
   
 9. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Chadema inaingiaje hapa? Bwana Masawe mbona unaingiza chama chenu hapa kwenye hoja ambayo haiendani?
   
 10. Kwamex

  Kwamex JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 378
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Bora umeongea maana mpayukaji kadri anavyojitafutia umaarufu wake binafsi, ndo anavyozidi kukiteketeza chama chake....wawafuate RACHEL tuone uanaume wao.
   
 11. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,887
  Likes Received: 6,072
  Trophy Points: 280
  CCM acha utani, tunataka "MAPACHA WATATU". Msiwe waoga wa kufanya maamuzi kama mlivyoambiwa na 'gamba # 2'
   
 12. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  CCM wajanja sn mnavifukuza vidagaa vidogo huku mkiyaacha makambale yakiendelea kula yanavyotaka teh! teh! teh!
   
 13. h

  hans79 JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  pagumu kufunga paka kengere,manyowe yamechosha twataka vitendo so kaul tatanishi.
   
 14. W

  WildCard JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kwa EL sio rahisi. Alijiuzuru kwa kuwajibika tu. Hivyo ndivyo JK na CCM yake wanavyoelewa na ndivyo tutakavyoelezwa. Hawa wengine wawili inategemea kama wao wenyewe watakuwa tayari kutolewa sadaka kama EL alivyofanya kuinusuru serikali nzima isianguke. Sio Mukama wala Nape wanaojua nini kitafanyika.
   
 15. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kweli CCM, kwa usani kiboko yaani leo kaikana kauli yake baada ya kuona maji ya shingo tulimwambia hawa wezi akina Lowasa, Rostam na Chenge...
   
 16. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #16
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Isije ikawa ni danganya toto kumbe JK anapanga timu yake ya kupandikiza mgimbea urais 2015. Mnawatoa waliokuwa kundi la EL na kuweka ambao watamuunga mgombea wenu. Magamba si ni watu wa fitna miaka yote, hakuna uamuzi unaofanyika Magamba ukawa objective, they are always subjective kumnufaisha fulani. Hapa wanajipanga kwa 2015 hawana lolote. Mwenye Chama alishakufa (Nyerere) waliobaki wote wasanii wanaangalia future na maslahi yao. Nape mwenyewe yuko kibiashara tu hapo.
   
 17. l

  luhwege Member

  #17
  Jun 30, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 90
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Nijuavyo nyoka kujivua gamba huwa linakuja lingine na huwa na sumu kali na usiombe ukakuta ndiyo anamalizia kujivua huwa ni mkali kupita kiasi sasa CCM kwa mtaji huo ni hatari kwao mimi naona ndiyo mwisho wao wasome nyakati
   
 18. l

  luhwege Member

  #18
  Jun 30, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 90
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Nijuavyo nyoka kujivua gamba huwa linakuja lingine na huwa na sumu kali na usiombe ukakuta  ndiyo anamalizia kujivua huwa ni mkali kupita kiasi sasa CCM kwa mtaji huo ni hatari kwao mimi naona ndiyo mwisho wao wasome nyakati
   
 19. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #19
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Waacheni wafu wawazike wafu wenzao...
   
 20. HOMOSAPIEN

  HOMOSAPIEN JF-Expert Member

  #20
  Jun 30, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 719
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Ni kina nani hao tuwekeeni majina tuwajue,na yule wa Arusha yumo?
   
Loading...