CCM yasimamisha uchapishaji wa gazeti la Uhuru kwa siku 7 na kuwasimamisha Watendaji Wakuu watatu

Si sahihi Katibu Mkuu wa CCM kusema amelifungia gazeti bali aseme ameagiza usitishwaji wa uchapishaji/uzalishaji wa gazeti hilo.
Yupo Waziri mwenye dhamana na magazeti ndiye angetoa tamko kama gazeti hilo limekiuka misingi ya kusajiliwa kwake!
Hivi CCM kuna wanasheria gani ?! Mbona mnashindwa kuwashauri viongozi katika kutimiza majukumu yao!
Tatizo la kupeana nafasi ndani ya Chama bila kujali uwezo, CCM imejaza Wanasheria vil.aza sana!
 
Me sijaelewa kabisa,hilo gazeti ni la chama au??

M,ccm anapataje nguvu ya kulifungia hilo gazeti,nipeni elim ndugu zangu.

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Katibu mkuu wa CCM mh. Daniel Chongolo amelifungia gazeti hilo la uhuru. Pia wafanyakazi wengine na wahariri wa gazeti hilo wamesimamishwa.
Gazeti hilo limefungwa kutoka na upotoshaji ulio fanywa.
Pia Ikumbukwe Gazeti hilo ni mali ya CCM

FB_IMG_16286913241432301.jpg

FB_IMG_16286913241432301.jpg
 
Kwani uongo? Mama atoshi.
Kama 25 atasimama mtapata kura 1.
Sasa kama jiwe na ubabe wake bila kuiba asingepita,watz wa leo sio wa jana.
 
DANIEL CHONGOLO AMBAE NI KATIBU MKUU CCM TAIFA AMELIFUNGIA SIKU SABA GAZETI LA UHURU KWA KUCHAPISHA HABARI ISEMAYO KUWA RAIS SAMIA HASSANI SULUHU HANA MPANGO WA KUGOMBEA 2025.

GAZETI LA UHURU LIMEFUNGUWA SIKU SABA

Uhuru wa vyombo vya habari saizi uko huru.

----
Chama cha Mapinduzi kimesimamisha uchapishaji wa gazeti la Uhuru kwa muda wa siku saba huku kikiwasimamisha kazi watendaji wakuu watatu wa gazeti hilo kwa madai ya upotoshaji wa kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Mapema leo chama hicho kilitoa taarifa kikieleza kusikitishwa na kitendo kilichofanywa na gazeti hilo cha kupotosha kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan iliyotokana na mahojiano ya kiongozi huyo na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), ambapo chama kiliahidi kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wote waliohusika katika uandaaji wa habari hiyo.

Gazeti hilo la CCM, toleo la leo Agosti 11, limeandika habari yenye kichwa kisemacho “Sina wazo kuwania urais 2025-Samia”, ambayo imepewa uzito mkubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari baadaye leo Jumatano Agosti 11, 2021, Katibu Mkuu wa chama hicho, Daniel Chingolo amesema uamuzi wa kuwasimamisha kazi viongozi hao umetolewa na bodi ambayo imeenda mbali na kuunda kamati ya kuchunguza sababu za jambo hilo kutokea.

“Ukifuatilia mahojiano aliyofanya Rais Samia Suluhu Hassan hakuna mahali alipozungumza maneno yaliyoandikwa kwenye kichwa cha habari cha gazeti la Uhuru la leo, amelishwa maneno na uungwana ni vitendo tunamuomba radhi Rais.

Viongozi waliosimamishwa kazi ni Mkurugenzi Mtendaji wa gazeti hilo, Ernest Sunguya ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mhariri Mtendaji, Athumani Mbutuka na msimamizi wa gazeti hilo, Rashid Zahoro.

“Tumeamua mambo kadhaa, bodi ilikutana na kuleta taarifa ya hitimisho la kikao chao, ninaipongeza kwa uamuzi walioufanya na mimi kama Katibu Mkuu nimesimamisha kuanzia leo uchapishaji wa gazeti la Uhuru kwa siku saba, hayo ni mamlaka yangu,” amesema Chongolo.

Chanzo: Mwananchi

Menyewe kwa menyewe wallahi.

Kwani waziri mwenye dhamana kasema je?
 
Mbona kichwa cha habari kiko kibiashara kuuza gazeti tu. Ukisoma content unakuta hakuna tofauti mama alivyosema. Alisema ni mapema kua amefanya uamuzi kama atagombea urais. Hawa kina chongolo naona wanafanya papara jazba na kujipendekeza tu. Yafaa wawe makini sana jinsi ya kuongoza chama.
 
DANIEL CHONGOLO AMBAE NI KATIBU MKUU CCM TAIFA AMELIFUNGIA SIKU SABA GAZETI LA UHURU KWA KUCHAPISHA HABARI ISEMAYO KUWA RAIS SAMIA HASSANI SULUHU HANA MPANGO WA KUGOMBEA 2025.

GAZETI LA UHURU LIMEFUNGUWA SIKU SABA

Uhuru wa vyombo vya habari saizi uko huru.

----
Chama cha Mapinduzi kimesimamisha uchapishaji wa gazeti la Uhuru kwa muda wa siku saba huku kikiwasimamisha kazi watendaji wakuu watatu wa gazeti hilo kwa madai ya upotoshaji wa kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Mapema leo chama hicho kilitoa taarifa kikieleza kusikitishwa na kitendo kilichofanywa na gazeti hilo cha kupotosha kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan iliyotokana na mahojiano ya kiongozi huyo na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), ambapo chama kiliahidi kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wote waliohusika katika uandaaji wa habari hiyo.

Gazeti hilo la CCM, toleo la leo Agosti 11, limeandika habari yenye kichwa kisemacho “Sina wazo kuwania urais 2025-Samia”, ambayo imepewa uzito mkubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari baadaye leo Jumatano Agosti 11, 2021, Katibu Mkuu wa chama hicho, Daniel Chingolo amesema uamuzi wa kuwasimamisha kazi viongozi hao umetolewa na bodi ambayo imeenda mbali na kuunda kamati ya kuchunguza sababu za jambo hilo kutokea.

“Ukifuatilia mahojiano aliyofanya Rais Samia Suluhu Hassan hakuna mahali alipozungumza maneno yaliyoandikwa kwenye kichwa cha habari cha gazeti la Uhuru la leo, amelishwa maneno na uungwana ni vitendo tunamuomba radhi Rais.

Viongozi waliosimamishwa kazi ni Mkurugenzi Mtendaji wa gazeti hilo, Ernest Sunguya ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mhariri Mtendaji, Athumani Mbutuka na msimamizi wa gazeti hilo, Rashid Zahoro.

“Tumeamua mambo kadhaa, bodi ilikutana na kuleta taarifa ya hitimisho la kikao chao, ninaipongeza kwa uamuzi walioufanya na mimi kama Katibu Mkuu nimesimamisha kuanzia leo uchapishaji wa gazeti la Uhuru kwa siku saba, hayo ni mamlaka yangu,” amesema Chongolo.

Chanzo: Mwananchi
Mazingaombwe yameanza tena. Very technical to identify behind this🤸🤸🤸
 
Back
Top Bottom