Ccm yasimamisha mgombea ubunge wa darasa la 6c jimbo la mhambwe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm yasimamisha mgombea ubunge wa darasa la 6c jimbo la mhambwe!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Bukijo, Sep 9, 2010.

 1. B

  Bukijo Senior Member

  #1
  Sep 9, 2010
  Joined: Jul 28, 2010
  Messages: 166
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Wadau wa JF,Poleni na majukumuu ya kuleta mapinduzi ya kifikra katika jamii.
  Nimeona nami niwashilikishe hili japa bado mi mchanga katika siasa lakin kuna jambo nikifikiria linaniuma na ningependa mnijulishe kwa ufupi-
  Je,ni halali kwa mtu ambaye hana hata Certificate ya Primary kuingia Bungeni et kisa yupo CCM?.
  Jimbo la Mhambwe lililopo Kibondo/Kigoma mgombea wake wa Ubunge kupitia CCM hakufanikiwa kumaliza darasa la Saba! ameishia darasa la Sita ila kwenye kura za maoni amepita kidedea na kuwa mshindi kupitia CCM!.Wananchi wamechanganyikiwa wakihofu kuwa endapo watamchagua hatofanya lolote kwa kuwa uwezo wa kujieleza ni mdogo na pia hatokua na confidence ya kusimama Bungeni kwa kuwa yeye ni darasa la sita!
  Hii et imemsababisha Mbunge wa zamani wa Jimbo hilo-Arcado D.Ntagazwa kuwaonea huruma wakazi wa Jimbo hilo na kuamua Kugombea Ubunge kwa Tiketi ya CHADEMA,akiahidi et kuwaletea maendeleo!
  Lakini Je,Ntagazwa ambaye amekaa Bungeni kwa zaidi ya Miaka 20 akiwa CCM na hakufanya lolote katika Jimbo hilo ataleta Mapindizi yoyote kwa sababu yupo CHADEMA?.
  Wadau naombeni ushauri kuhusu Jimbo hilo hatuoni Tumchague nan kwani hakuna hata mmoja kati yao anayefaa!!
  Asanteni!
   
 2. M

  Majala Kimolo JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 344
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Dr Slaa, mgombea wake wa Urais alisema mchagulie mbunge wa chama chake, hata kama atakuwa zezeta watamchangamsha. Miaka 20 ndani ya sisi m ni sawa na kuwa uvunguni mwa mafia, huwezi kufurukuta mpaka uwe ndani ya mtandao. Poleni wana Kibondo kwa kuachwa nyuma, napajua jinsi palivyochakaa. Ila msikate tamaa, ikataeni sisi m kama ilivyowatosa kwa miaka mingi
   
 3. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Darasa la 6 hii kiboko sasa ile miswada nani atakuwa anamsaidia kutafsiria au mkalimani wake atakuwa Mwl.Makamba :becky::becky::becky:
   
 4. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwanza umejitambulisha? ok kama wananchi ndio waliompitisha lazima wanajua uwezo wake wa uwajibikaji kwao,so tuwaachie wenyewe,na je sifa za mgombea ubunge ni zipi? yawezekana na sheria inamruhusu kugombea.
   
 5. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Sifa za mgombea wa Tz ni kujuwa kusoma na kuandika!!!!!
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,434
  Likes Received: 5,691
  Trophy Points: 280

  wapi wameandika mbunge lazima awe na certificate siku nyingine uliza kabla ya kuleta hadharani ....ata jiwe wanauuwezo wa kulismamisha na kushinda ujui ccm
   
 7. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Uko sahihi kaka, hata Slaa angekuwa CCM asingefurukuta na ndio maana Zitto wanamtaka sana lakini hawampati maana anajua kwamba huko ni kwenda kifungoni, jambo ambalo analiona wazi litammaliza kisiasa katika umri anaotakiwa kupaa.
   
 8. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Ulishamsikia makamba akichangia hoja bungeni au kuongea kiingereza hata siku moja?
   
 9. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  ccm ya vimeo...vilaza..vihiyo kama katibu wao mkuu
   
 10. comp

  comp Member

  #10
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umesahau pale bungeni wabunge wote wa CCM wanavyolazimishwa wawe na msimamo mmoja wakati wapinzani wanapoanzisha topic ambazo ni against sera zao? wana vikao vyao wanakaaga siku moja kabla hot topic kuwasilishwa, mwenyekiti anakuwa waziri mkuu kama siyo katibu wao mkuu wa chama(sina hakika sana hapo) Ukiwa mbunge wa CCM unatetea interest za CHAMA siyo nchi. so siyo kitu cha ajabu kuona Ntagazwa akawa active sana ndani ya CHADEMA compared na alivyokuwa CCM. ni system na sera za chama tu mkuu, usiogope kumpa kura.
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  elimu haijawahi kuwa na umuhimu kwenye siasa za tanzania.

  ukimaliza ccm kaangalie kwa upinzani. hali hiyo hiyo.
   
 12. B

  Bukijo Senior Member

  #12
  Sep 9, 2010
  Joined: Jul 28, 2010
  Messages: 166
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Mkuu nashukuru kwa ushauri wako,make nimesoma Makala yake(Ntagazwa) kwenye gazeti nikavutiwa na msimamo wake ila wasiwasi wangu nikua huenda akawa kama kipindi yupo CCM!
   
 13. A

  ALIBAALIO Member

  #13
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sioni kama kuwa mbunge wa ccm na sasa ameamua kutoka kunaweza kumfanya asiwe mwanachama mwaminifu kwa CHADEMA.mtu anabadili dini na anakuwa muhumini mzuri zaidi ya waliozaliwa kwenye hiyo dini
   
 14. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #14
  Sep 9, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  wakazi wa kibondo mpeni ntagazwa, na hakika atakuwa mgombea mzuri, sana
   
Loading...