CCM yashusha maelekezo mazito bandari ya Mtwara

Political Jurist

Senior Member
Sep 6, 2021
120
104
CCM YASHUSHA MAELEKEZO MAZITO BANDARI YA MTWARA

Ijumaa Sept 17, 2021.

"Pamoja na uwekezaji huu mkubwa wa takribani bilioni 158.8 za kuboresha bandari hii ya Mtwara ni ajabu haitoi huduma kama ilivyokusudiwa" shaka Mwenezi Taifa

"Sababu ikiwa ni urasimu na hata hujuma zinazofanywa na baadhi ya watendaji wa kiserikali kwa kushirikiana na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu" Shaka Mwenezi Taifa

"CCM hatutakubali kuona utekelezaji wa ilani yetu ya uchaguzi unakwamishwa kwani kufanya hivyo ni kumkwamisha Mhe Rais Samia Suluhu Hassan na kuchelewesha maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla" Shaka Mwenezi Taifa

"Tunataka bandari hii ianze kutoa huduma haraka ili kuzalisha ajira, kuchochea uchumi wa Mtwara na nchi pia" Shaka Mwenezi Taifa

"Mamlaka ya bandari iweke mkakati thabiti wa kuitangaza bandari hii ili wafanyabiashara na wawekezaji mbalimbali waijue na waitumie kuingiza na kusafirisha mizigo yao kupitia hapa" Shaka Mwenezi Taifa.

"Haiwezekani Rais Samia amemtuma Waziri Mkuu Majaliwa lakini baadhi ya watendaji wasiwaminifu wamepuuza maagizo hayo" Shaka Mwenezi Taifa

"CCM haitamvumilia yoyote mwenye nia ovu ya kukwamisha jitihada za Rais Samia katika kuwaletea maendeleo watanzania atakwama yeye" Ndg Shaka Mwenezi Taifa

IMG-20210917-WA0375.jpg
 
Back
Top Bottom