CCM yasambaza vipeperushi vya kifo

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
310
79
Baada ya serikali kuingilia kati na kuvishauri vyombo vya habari kuepuka habari za Wangwe zenye mwelekeo wa kuvunja utawala wa sheria na baada ya siri ya CCM kusambaza waraka wa Wangwe kugundulika. Sasa mkakati mpya umeanza wa kusambaza vipeperushi vidogo vinavyoeleza kwamba Freeman Mbowe, Dr Slaa, Zitto na Mnyika ni wauaji wakubwa CHADEMA waliomuua chacha wangwe. Tayari vipeperushi hivyo vimeshasambazwa barabarani mikoa ya Mwanza na Shinyanga, kwa mujibu wa kiongozi mmoja wa CCM ambao hakutaka kutajwa jina lake. Vipeperushi hivyo vitasambazwa pia katika mikoa mingine

PM
 
wanataka kuwagawanya Chadema, kwani ndo chama kinachowasumbua baadhi ya sehemu ukiacha visiwani ambako CUF ndo wamedominate
 
Baada ya serikali kuingilia kati na kuvishauri vyombo vya habari kuepuka habari za Wangwe zenye mwelekeo wa kuvunja utawala wa sheria na baada ya siri ya CCM kusambaza waraka wa Wangwe kugundulika. Sasa mkakati mpya umeanza wa kusambaza vipeperushi vidogo vinavyoeleza kwamba Freeman Mbowe, Dr Slaa, Zitto na Mnyika ni wauaji wakubwa CHADEMA waliomuua chacha wangwe.
Huo ndio ukweli wenyewe...!
 
kwa kweli huu ni uchonganishi wa hali ya juu kati ya wananchi na viongozi hawa wa chama cha upinzani.Nia hasa ni kuua nguvu waliyonayo CHADEMA
 
Tatizo lingine la CCM ni kutikuwa na Strategists walio up - to - date
 
Hizo ni harakati za mfa maji. Shututma za ufisadi zimewaelemea sasa ni lazima wale wote wanaong'ang'ania hoja hiyo ni lazima wamalizwe. Hiyo ndiyo sisiemu. Sasa ngoja uone wakimaliza Chadema watageukana wao kwa wao. Mama Kilango ukiona mwenzio ananyolewa wewe tia maji. Na akina Mwakyembe subirini ya kwenu yanakuja.

CHADEMA msife moyo sisi wananchi tunajua ukweli huu, ninyi ndiyo ma-championi wa vita dhidi ya ufisadi. Aluta continue, mapambano bado yanaendelea.
 
Uwezi Kuwa Na Stratege Wakati Sg Makamba Mind Yake Ipo Kama Ya Mchuuzi Tu,they Behave Now Kama Opposition
 
Tehetehe .... hii habari inafaa kuundwe forum nyingine iitwe upupu!!! alafu hii habari ipelekwe huko.
 
Hapa hakuna uchonganishi wala nini, hii ni mbinu chafu ya CCM ya kutaka kuondoa FOCUS kwenye UFISADI ili watu waanze kujadili Upuuzi wao. TUNATAKA MAFISADI WASHITAKIWE KWANZA Then tuangalia mambo mengine.
 
kicks of a dying horse,dont make me laugh what strategy do you expect from makamba who sat for his form 4 exam as a private candidate while he was dar RC? wangemwachia Msekwa labda
 
Huo ndio ukweli wenyewe...!
Yani serikali ya ccm iwe na ushahidi halafu wawaache hao wanaosema wamemwua Wangwe mtaani....Huu ni mtaji wa ccm wa kisiasa...Na kama nilivyojuwa ccm wanataka kuitumia kama karata yao...Wapinzani wangekuwa wajanja wangeungana sasa nyuma ya Mrema...Mrema Rais...Makamu Slaa...Waziri Mkuu Zitto...Makamu wa pili wa Rais Lipumba...Na huko Zenji mnaurekebisha mungano...Waziri wa mambo ya ndani Mbatia...Mengine mjazie...Hiyo ikiwa ni serikali kivuli ili kuwabipu ccm...Basi wataufyata!
TRUST ME.
 
Mategemea nini kutoka kwenye cham cha kifisadi kilichojaa mafisadi na kuongozwa n viongozi wasiyo na uwezo wowote wa kuongoza akina JK, Msekwa na Makamba.
 
Hapa hakuna uchonganishi wala nini, hii ni mbinu chafu ya CCM ya kutaka kuondoa FOCUS kwenye UFISADI ili watu waanze kujadili Upuuzi wao. TUNATAKA MAFISADI WASHITAKIWE KWANZA Then tuangalia mambo mengine.

Ni yote mawili kwa mpigo. Kwanza ni kutuhamisha katika UFISADI na pili ni kuigawa CHADEMA sasa wanaichonganisha na wapiga kura. TUNAHITAJI KUBADILI MBINU ZA KUKABILIANA NA MAFISADI kwani kwa upeo wa wananchi wetu watafanikiwa kuishusha thamani CHADEMA kwa hila zao hizi za kuihusisha na Kifo.

Naomba mwenye vipeperushi hivyo atusaidie humu JF tuvichambue tumewakaba koo hawa. Pia nimewasiliana na Mwandishi wa Mwanza aliyefichua kuhusu Waraka wa Wangwe kusambazwa na CCM naye amesema kuwa anavisaka Vipeperushi hivyo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom