CCM yapongeza ziara ya rais Samia Kenya

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
324
1,000
Na Mwandishi Wetu, Dodoma

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimepongeza hatua zinazochukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha Diplomasia ya uchumi na ushirikiano wa kimataifa.

Chama kimesema hatua zinazochukuliwa na Rais Samia ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, inayoagiza kuimarisha ushirikiano na mataifa mengine na kufungua fursa kupitia diplomasia ya uchumi.

Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka alipozungumza kuhusu ziara ya siku mbili ya Rais Samia nchini Kenya ambako kwa kushirikiana na mwenyeji wake, Rais Uhuru Kenyatta, waliweka maazimio mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha uhusiano na kuchochea fursa za kibiashara kwa nchi zao.

“Sera ya mambo ya nje ya Tanzania ni kuendeleza diplomasia ya kiuchumi baada ya kupata mafanikio makubwa ya kujitangaza, kuweka bayana misimamo yake hatimaye kufahamika kimataifa kuanzia awamu ya kwanza hadi ya sita.

“Chama kinaridhishwa na juhudi za kisera zitokanazo na ufanisi upeo na maarifa aliyonayo Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan katika medani za kimataifa ukiwa ni utekelezaji wa sera ya nje na kuimarisha sera ya Diplomasia ya Uchumi,” alisema Shaka.

Alisema ziara ya Rais Samia ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika masuala ya kidipomasia.

Shaka alisema ilani hiyo katika kifungu cha 132 (a ) inaeleza; “Chama kitaielekeza Serikali kuboresha utekelezaji wa mipango ya kuimarisha diplomasia ya siasa ya kimkakati kwa ajili ya kulinda amani, uhuru, maslahi ya taifa na kuimarisha ujirani mwema na kushiriki kikamilifu kuimarisha utangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kukuza uhusiano wa kiuchumi na mataifa, jumuiya za kikanda na taasisi zingine za kimataifa.”

Kwa mujibu wa Shaka, Chama pia kimempongeza Rais Samia kwa kuendeleza msisitizo kwa kuyapa msukumo masuala ya ulinzi na usalama, mapambano dhidi Covid-19, ushirikiano wa vyombo vya ulinzi na usalama wa kikanda na kukabiliana na uhalifu.

Shaka alisema Rais Samia, licha ya kuonyesha upeo, maarifa na ufahamu mpana wa masuala ya kidiplomasia, ameweka bayana msimamo wa nchi akionyesha dhamira njema ya kutaka kuendeleza ushirikiano hususan katika nchi za Afrika Mashariki.

Akiwa Kenya, Rais Samia alifanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuzungumza na Rais Kenyatta, kuhudhuria kongamano la wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania na kuhutubia Bunge la Taifa na Seneti.

BALOZI APONGEZA

Katika hatua nyingine, Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk. John Simbachawene, ameipongeza timu ya watendaji na wataalamu kutoka nchini kwa kufanikisha ziara hiyo.

Dk. Simbachawene alitoa pongezi hizo katika Ubalozi wa Tanzania jijini Nairobi, alipokutana na timu ya watendaji na wataalamu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Viwanda na Biashara.

“Nawashukuru na kuwapongeza kwa kazi kubwa na nzuri mliyoifanya hadi kukamilika kwa ziara ya Mheshimiwa Rais, ni wazi kuwa, kufanya kazi kwa pamoja ni kitu kizuri wote tumeona hapa, asanteni sana na hongereni kwa kazi,” alisema.

Aliwataka watendaji hao kuhakikisha wanazingatia na kutekeleza yote yaliyoongelewa na kutolewa maelekezo na viongozi wakuu wa nchi hizo ili kuhakikisha vikwazo vya biashara visivyo vya kodi vinaondolewa na hivyo kukuza na kuimarisha uwekezaji na biashara kwa manufaa ya nchi zote mbili.TANZANIA...
IMG_20210506_101752.jpg
IMG_20210506_101802.jpg
 
Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
12,007
2,000
Kuabudu kunaendelezwa?

So ghe next Ccm wampongeza Sasha kwa kumzawadia Mwinyi benz huku walimu wananjaa na kucheleweshewa mishahara
 
Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
12,007
2,000
Ccm wampengeza waziri mkuu kwa kutumia ndege ya Atcl kwenda chato kumjulia hali Mama wa Maguful
 
mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
8,105
2,000
Na Mwandishi Wetu, Dodoma

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimepongeza hatua zinazochukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha Diplomasia ya uchumi na ushirikiano wa kimataifa.

Chama kimesema hatua zinazochukuliwa na Rais Samia ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, inayoagiza kuimarisha ushirikiano na mataifa mengine na kufungua fursa kupitia diplomasia ya uchumi.

Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka alipozungumza kuhusu ziara ya siku mbili ya Rais Samia nchini Kenya ambako kwa kushirikiana na mwenyeji wake, Rais Uhuru Kenyatta, waliweka maazimio mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha uhusiano na kuchochea fursa za kibiashara kwa nchi zao.

“Sera ya mambo ya nje ya Tanzania ni kuendeleza diplomasia ya kiuchumi baada ya kupata mafanikio makubwa ya kujitangaza, kuweka bayana misimamo yake hatimaye kufahamika kimataifa kuanzia awamu ya kwanza hadi ya sita.

“Chama kinaridhishwa na juhudi za kisera zitokanazo na ufanisi upeo na maarifa aliyonayo Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan katika medani za kimataifa ukiwa ni utekelezaji wa sera ya nje na kuimarisha sera ya Diplomasia ya Uchumi,” alisema Shaka.

Alisema ziara ya Rais Samia ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika masuala ya kidipomasia.

Shaka alisema ilani hiyo katika kifungu cha 132 (a ) inaeleza; “Chama kitaielekeza Serikali kuboresha utekelezaji wa mipango ya kuimarisha diplomasia ya siasa ya kimkakati kwa ajili ya kulinda amani, uhuru, maslahi ya taifa na kuimarisha ujirani mwema na kushiriki kikamilifu kuimarisha utangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kukuza uhusiano wa kiuchumi na mataifa, jumuiya za kikanda na taasisi zingine za kimataifa.”

Kwa mujibu wa Shaka, Chama pia kimempongeza Rais Samia kwa kuendeleza msisitizo kwa kuyapa msukumo masuala ya ulinzi na usalama, mapambano dhidi Covid-19, ushirikiano wa vyombo vya ulinzi na usalama wa kikanda na kukabiliana na uhalifu.

Shaka alisema Rais Samia, licha ya kuonyesha upeo, maarifa na ufahamu mpana wa masuala ya kidiplomasia, ameweka bayana msimamo wa nchi akionyesha dhamira njema ya kutaka kuendeleza ushirikiano hususan katika nchi za Afrika Mashariki.

Akiwa Kenya, Rais Samia alifanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuzungumza na Rais Kenyatta, kuhudhuria kongamano la wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania na kuhutubia Bunge la Taifa na Seneti.

BALOZI APONGEZA

Katika hatua nyingine, Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk. John Simbachawene, ameipongeza timu ya watendaji na wataalamu kutoka nchini kwa kufanikisha ziara hiyo.

Dk. Simbachawene alitoa pongezi hizo katika Ubalozi wa Tanzania jijini Nairobi, alipokutana na timu ya watendaji na wataalamu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Viwanda na Biashara.

“Nawashukuru na kuwapongeza kwa kazi kubwa na nzuri mliyoifanya hadi kukamilika kwa ziara ya Mheshimiwa Rais, ni wazi kuwa, kufanya kazi kwa pamoja ni kitu kizuri wote tumeona hapa, asanteni sana na hongereni kwa kazi,” alisema.

Aliwataka watendaji hao kuhakikisha wanazingatia na kutekeleza yote yaliyoongelewa na kutolewa maelekezo na viongozi wakuu wa nchi hizo ili kuhakikisha vikwazo vya biashara visivyo vya kodi vinaondolewa na hivyo kukuza na kuimarisha uwekezaji na biashara kwa manufaa ya nchi zote mbili.TANZANIA... View attachment 1778038 View attachment 1778039
Mimi sina tatizo na Sera zilizomo kwenye Ilani ya CCM, Uchaguzi 2020, kama zilivyo Sera za Taifa kwa ujumla. Tatizo la msingi ni Mikakati ya utekekezaji na usimamizi wake. Yaonekana tunapewa maneno mengi ya kutia matumaini lakini hadi naandika hoja yangu hii hakujawa na tafsiri kwa vitendo
 
Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
19,778
2,000
Ina maana walikuwa bado wanajiuliza wampongeze ama la, wengine tulimpongeza mara tu ilipotangazwa kuwa atakuwa na ziara.
 
dapangi

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
589
500
Na Mwandishi Wetu, Dodoma

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimepongeza hatua zinazochukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha Diplomasia ya uchumi na ushirikiano wa kimataifa.

Chama kimesema hatua zinazochukuliwa na Rais Samia ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, inayoagiza kuimarisha ushirikiano na mataifa mengine na kufungua fursa kupitia diplomasia ya uchumi.

Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka alipozungumza kuhusu ziara ya siku mbili ya Rais Samia nchini Kenya ambako kwa kushirikiana na mwenyeji wake, Rais Uhuru Kenyatta, waliweka maazimio mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha uhusiano na kuchochea fursa za kibiashara kwa nchi zao.

“Sera ya mambo ya nje ya Tanzania ni kuendeleza diplomasia ya kiuchumi baada ya kupata mafanikio makubwa ya kujitangaza, kuweka bayana misimamo yake hatimaye kufahamika kimataifa kuanzia awamu ya kwanza hadi ya sita.

“Chama kinaridhishwa na juhudi za kisera zitokanazo na ufanisi upeo na maarifa aliyonayo Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan katika medani za kimataifa ukiwa ni utekelezaji wa sera ya nje na kuimarisha sera ya Diplomasia ya Uchumi,” alisema Shaka.

Alisema ziara ya Rais Samia ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika masuala ya kidipomasia.

Shaka alisema ilani hiyo katika kifungu cha 132 (a ) inaeleza; “Chama kitaielekeza Serikali kuboresha utekelezaji wa mipango ya kuimarisha diplomasia ya siasa ya kimkakati kwa ajili ya kulinda amani, uhuru, maslahi ya taifa na kuimarisha ujirani mwema na kushiriki kikamilifu kuimarisha utangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kukuza uhusiano wa kiuchumi na mataifa, jumuiya za kikanda na taasisi zingine za kimataifa.”

Kwa mujibu wa Shaka, Chama pia kimempongeza Rais Samia kwa kuendeleza msisitizo kwa kuyapa msukumo masuala ya ulinzi na usalama, mapambano dhidi Covid-19, ushirikiano wa vyombo vya ulinzi na usalama wa kikanda na kukabiliana na uhalifu.

Shaka alisema Rais Samia, licha ya kuonyesha upeo, maarifa na ufahamu mpana wa masuala ya kidiplomasia, ameweka bayana msimamo wa nchi akionyesha dhamira njema ya kutaka kuendeleza ushirikiano hususan katika nchi za Afrika Mashariki.

Akiwa Kenya, Rais Samia alifanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuzungumza na Rais Kenyatta, kuhudhuria kongamano la wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania na kuhutubia Bunge la Taifa na Seneti.

BALOZI APONGEZA

Katika hatua nyingine, Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk. John Simbachawene, ameipongeza timu ya watendaji na wataalamu kutoka nchini kwa kufanikisha ziara hiyo.

Dk. Simbachawene alitoa pongezi hizo katika Ubalozi wa Tanzania jijini Nairobi, alipokutana na timu ya watendaji na wataalamu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Viwanda na Biashara.

“Nawashukuru na kuwapongeza kwa kazi kubwa na nzuri mliyoifanya hadi kukamilika kwa ziara ya Mheshimiwa Rais, ni wazi kuwa, kufanya kazi kwa pamoja ni kitu kizuri wote tumeona hapa, asanteni sana na hongereni kwa kazi,” alisema.

Aliwataka watendaji hao kuhakikisha wanazingatia na kutekeleza yote yaliyoongelewa na kutolewa maelekezo na viongozi wakuu wa nchi hizo ili kuhakikisha vikwazo vya biashara visivyo vya kodi vinaondolewa na hivyo kukuza na kuimarisha uwekezaji na biashara kwa manufaa ya nchi zote mbili.TANZANIA... View attachment 1778038 View attachment 1778039
Kwani aliyemtangulia alikuwa hatekelezi ilani hiyo? Kazi ipo.
 
UmkhontoweSizwe

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
4,843
2,000
Ngoja tusubiri tuone kama chadema watapinga as usual, au wataunga tela kwenye kumpongeza mama. Nadhani wako njia panda!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom