CCM yaogopa kuwakabidhi barua mafisadi warushiana mpira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yaogopa kuwakabidhi barua mafisadi warushiana mpira

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by carefree, Apr 23, 2011.

 1. c

  carefree JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  [​IMG] Kila mmoja akwepa ni lini zitaandikwa
  [​IMG] Wengine wawa mbogo, kuulizwa hayo  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama


  Wingu la ufisadi bado linazidi kuwaumiza vichwa viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), baada ya vigogo wa ngazi za juu wa chama hicho kuogopa kuweka wazi iwapo watuhumiwa wa ufisadi ndani ya chama hicho wameshakabidhiwa barua za kuwataka wajiondoe wenyewe.
  Kila kiongozi aliyetafutwa jana kuzungumza iwapo tayari chama kimewaandikia barua za kuwataka wajiondoe kwenye chama hicho, aling’aka na kuelekeza aulizwe mwenzake.
  Wa kwanza alikuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ambaye alisema suala hilo halishughulikiwi na idara yake hivyo alielekeza aulizwe Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Mukama.
  Alisema kila idara inajukumu lake na kwamba ofisi yake ni ya kuzungumzia masuala ya chama, lakini si mambo yanayohusu masuala ya utendaji.
  “Kila idara inawajibu wake, hilo haliko kwenye idara yangu, mimi ni msemaji wa chama nitafuatilia kujua kama zimeshaandikwa na kuwasilishwa kwa wahusika ila anayeweza kulisemea ni Katibu Mkuu,” alisema na kuongeza:
  “Jumatano watu wote wakiwa ofisini nitakuwa katika nafasi nzuri ya kulizungumzia hilo, nitafuatilia kujua kama zimeshaandikwa na kukabidhiwa kwa wahusika au la, lakini kwa sasa sijui lolote kuhusu hizo barua,” alisema Nnauye ambaye kabla ya kushika wadhifa huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi.
  Alipotafutwa Naibu Katibu Mkuu Bara, John Chiligati, alisema anayeweza kulisema suala hilo ni msemaji wa chama, Nnauye kwa kuwa si kila mtu anaweza kuzungumzia masuala ya chama.
  “Chama kinamzungumzaji wake ambaye ni Nape, mtafute Nape maana kila mtu akianza kuzungumza mambo ya chama itakuwa vurugu, ukimpata yeye atakueleza vizuri,” alisema.
  Alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Mukama, alikuwa mkali na kuelekeza kuwa aneyefaa kuulizwa ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Pius Msekwa.
  “Hayo unayoniuliza sikuwahi kuagiza yafanyike na wala si wajibu wangu, mtafute Makamu Mwenyekiti ndiye atakueleza, kwanza kwa sasa niko kijijini kwangu kuna mambo mengine nafanya,” alisema Mukama na kukata simu.
  Alipotafutwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Pius Msekwa aligeuka mbogo na kuhoji mwandishi anatafuta habari hizo kwa ajili ya kuzipeleka wapi.
  Baada ya kuulizwa iwapo chama hicho kimeshawaandikia barua watuhumiwa wa ufisadi, Msekwa alikuwa mkali na kumweleza mwandishi kuwa masuala hayo ni ya ndani ya chama na hayamhusu.
  “Hizi habari unatafuta za nini wakati hazikuhusu, unajua kuna habari za kuandika na zingine si za kuandika, hizi ni za kwetu ndani ya chama na hazikuhusu unataka za nini kwaheri,” alisema Msekwa na kukata simu.
  Wiki iliyopita, Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilimuagiza Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Mukama, kuwaandikia barua viongozi wanaotakiwa kujiuzulu kuwafahamisha kwamba, kama hawatafanya hivyo kikao kijacho cha NEC kitawafuta uongozi.
  Watuhumiwa hao wa rushwa na ufisadi wakiwemo wajumbe wa NEC taifa, wamepewa muda wa miezi mitatu sawa na siku 90 wapime uzito wa tuhuma zinazowakabili, wajiuzulu wenyewe.
  Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa, alieleza msimamo huo mjini Dodoma wakati wa mkutano wa kuwatambulisha wajumbe wa sekretarieti mpya akiwemo Katibu Mkuu, Wilson Mukama.
  Hatua hii ni mchakato wa CCM kujivua gamba. Tayari wajumbe wa Sekretarieti na Kamati Kuu walikwisha kujiuzulu na kutoa fursa ya kuteuliwa wengine. Maamuzi yaliyofanyika Dodoma wiki mbili zilizopita.
  Mytake
  HAwakuwa na sababu ya kutoa tamko ambalo hawawezi kulitekeleza kwani mimi nilidhani maamuzi yanayohusisha kikao cha ngazi za juu ya chama huwa yanaingia kwenye utekelezaji moja kwa moja sasa hapa kinachoonekana ni propaganda kwa kwenda mbele haiwezekani wazunguke mikoani kuitangaza maazimio ambayo hawajayatekeleza hii inakushushia hadhi kijana kama Nape kuwa nyuma ya mauzauza kama haya
   
 2. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Duhh..huu usanii kama bado haujaangamiza, soon utaangamiza taifa hili
   
 3. U

  Uswe JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  RACHEL si mchezo wewe!
   
 4. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,876
  Likes Received: 11,988
  Trophy Points: 280
  CCM hawana ubavu wowote wa kuwanyooshea kidole RACHEL maana RACHEL ndiyo CCM na CCM ndiye RACHEL wote wanaopiga kelele kuanzia mkuu wao kina Nape kina Mukama kina Msekwa wanalishwa na wameajiriwa na akina RACHEL mwambie Msekwa abishe kama kibarua chake hakitakwisha leo.
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mi nilisema hawa hawawezi kumfany akitu LOWASSA maana ni heavy weight kweli kweli....Jk mwenyewe anamgwaya itakua hivo vikunguni vya akina Nape
   
 6. mjunguonline

  mjunguonline Member

  #6
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM ni full usanii,hawa jamaa wana Masters ya Usanii kutoka "KAOLE SANAA GROUP",ila mwaka 2015 watakwisha...
   
 7. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,131
  Likes Received: 3,320
  Trophy Points: 280
  Sasa kilicho wafanya walopoke ni nini sasa?
   
 8. K

  Kiwete JF-Expert Member

  #8
  Apr 24, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 281
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 45
  Hivi Msekwa alishaacha uenyekiti wa board ya VODACOM TZ
   
 9. z

  zamlock JF-Expert Member

  #9
  Apr 24, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  unajua Mungu anapotaka kufanya jambo juu ya kitu fulani ni mengi huwa yanajitokeza kwa watu wenye akili timamu kuonekana awana akili hyo ni njia ambayo Mungu anaitumia kukiangamiza kabisa hii chama cha magamba na nina wambieni hichi chama kitafutika kwenye akili za watanzania
   
 10. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #10
  Apr 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Ccm sasa imefikia mwishi wake,nakumbuku kauli ya mbunge mmoja wakati wa uchaguzi, aliulizwa swali na mwandishi mmoja kama anajua Chama chake (Ccm) kimepanga kumundoa kwenye wadhifa fulani ndani ya Bunge,yeye akasema hivi "Mungu akitaka kummaliza mtu humpofusha asione litalo mkuta mbele". Hayo ndiyo yanyotokea kwa sasa ndani ya Ccm,wamejimaliza wenyewe wasitafute wa kumlaumu.
   
 11. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #11
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Lakini tuseme tu ukweli, pamoja na Lowasa kuchafuka huwezi mliganisha na Kikwete kwenye maongozi، halafu Lowasa ana pesa siku nyingi tu toka enzi ya Mwalimu, je Kikwete na Riziwan wake wamepata wapi haya mabilion ndani ya miaka 5 tu? Jamani haya mambo tuangalie! Huyu Jk ndiye noma kabisa.
   
 12. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #12
  Apr 24, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nape: muulize Katibu mkuu
  Chiligati: Muulize msemaji wa chama nape
  Mukama: achana na mimi muulize msekwa
  Msekwa: toka zako hapa "ukitaka nenda kwa JK"
  JK: mashairi ya sijui.
   
 13. Dadii

  Dadii Senior Member

  #13
  Apr 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 142
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mapacha watatu ni nomaaaa,,,,,,we subiri tu albamu yao itoke,,,, first single tu.....magamba wote hoi.
   
 14. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #14
  Apr 24, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  MZEE imekula kwako mkulu, ulifikiri hiyo singo ingechezeka kwa muda mrefu lakini ajabu yake sasa inazaa part two yake ambayo itawamaliza wenyewe kuliko mlivyotarajia maana kunaibuka swala la kuwatema wasiotemeka na ikibidi kuwatema mtaanza kwa kujitema wenyewe, mie simo mziki ndio umeshaanza hakuna wa kuuzima au ku-pause
   
 15. I

  Ilonza Senior Member

  #15
  Apr 25, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sikio la kufa harisikii dawa.Ebu tusubiri hawa viziwi kama watatibiwa au masikio yao yata endelea kupooza mpaka 2015
   
 16. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #16
  Apr 25, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hawa ccm kama walivyosema wanajanvi wengine hawana ubavu wa kuwafukuza Hao mapacha watatu toka chamani kwao ; hilo lilikuwa changa la macho kwa WAdanganyika ili kudivert attention yao toka mambo muhimu yanayowakabili kama vile ugumu wa maisha na mambo yanayohusu utungaji wa katiba mpya! Mwisho wa yote hii secretariat wanayosema ni ya kujivua magamba itafukuzwa mmoja baada ya mwingine. Let us wait time will tell.
   
Loading...