CCM yangu its to make or break | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yangu its to make or break

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nunu, Apr 26, 2012.

 1. n

  nunu Member

  #1
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wanajamii napenda kuwasalim kabla sijaenda kusema kwa mara ya kwanza katika blog hii.Imenichukua muda mwingi kusoma na kuelewa mwenendo wa blog na mtiririko wa hoja mbali mbali zinazoletwa humu; bila kumung'unya maneno kuna hoja nzito na pia kuna michango yenye mantiki sana na pia kuvurugana kwingi ali mradi uhuru ni wa kila mtu kuchangia unaheshimiwa. Hongera sana wawezeshaji wa mtandao huu.

  Kwa vile nachangia kwa mara ya kwanza, napenda kusema wazi mimi ni mwana CCM na ni mwanamke na kwa hakika ni katika kipindi hiki Chama chetu chaweza kujifunza ama kuvurugika vibaya(make or break). Mambo makuu na mazito yanayohitaji hatua za haraka ni: Rushwa/ufisadi na kuporomoka kwa ufanisi katika kila sector.

  1. Ni nini kigezo cha mtu kupewa msamaha wa kodi? Je hao waliopewa kama hawastahili basi wawajibishwe na walipe. Kama ni utajiri wetu wa maliasili tunufaike nao sawa na kama ni umasikini nao tugawane vema hili linawezekana. Naamini walioko kwenye madaraka na wanofisadi wanajua ugumu wa maisha ulivyo huku kwa wananchi na hivyo wanajihami kwa kufisadi na rushwa.

  Hili likomeshwe kama baadhi ya nchi jirani zinavyolitatua kwa nguvu zote.

  2. Hivi nani kasema watanzania wavivu? Hii hulka ya kutelekeza majukumu na kutowajibika inatoka wapi? Sasa ni wakati wa kufanya mageuzi kwa kuchukua maamuzi yatakayoadabisha na kutengeneza woga ndani ya watendaji. Tunamtii Mungu kwa vile tunamwogopa na kumheshimu na hivo basi lazima woga ujengwe kwa watumishi na watendaji wakuu kwa uongozi wanchi haraka iwezekanavyo. Mkuu wetu JK tenda, uwezo huo unao kabisa.

  3. Waheshimiwa wabunge (si wote) wa CCM ongezeni bidii ya kupangua hoja kwa kutumia well researched counter arguments na sio majibu au hoja za rasharasha. Wabunge wa Chadema (baadhi) wanajituma kutafuta takwimu na hoja kwa mengi wanayosema/hoji bungeni kwa kutambua kazi kubwa ya ubunge ni oversight role. Huwezi kutimiza hii bila kuwa na takwimu au hoja zilizopembuliwa vema.

  Naamini kipindi cha bajeti mtakuwa mumejiandaa vema kama wanavyojiandaa wengine. Sitafurahi kuona tena kituko kama cha Waziri na Mwenyekiti wa kamati ya Maliasili wote wa Kahama wakiminyana makonde ya ubabe wakati si CCM wilaya au mkoa hawakuweza kuona tofauti za hawa watu zikikua na hatimae kuonyeshana ubabe bungeni na sie watazamaji tukishuhudia aibu hio.

  Sitaona ajabu kama Kahama haitapata heshima ya kupata waziri kwa taswira iliyotokea kama hio kwani wilaya haikuona hili likija achilia mbali mkoa?. Kama waziri atabainika kuwa na makosa/udhaifu basi atakuwa na jeuri iliomkasirisha mwenyekiti wake ambaye naye ilimpendeza kuwajibika kwa kamati yake kama alivyofanya. Kahama imepokea kwa hisia tofauti drama hii.
   
 2. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Karibu ccm imekufa mama huo ushauri unawapa maiti ,ccm wanakila kitu kufanya tanzania iwe yenye neema lakini wameshindwa kwa sababu kuu kila aliyeko ccm NI MWIZI wanaiba hata visivyoibika ni AIBU,hakuna maono mapya ccm ,INAJIFIA TARATIBU ,2O15 kutatoke badiliko kubwa la kisiasa hapa Tz.kwani hata wale mliowadanganya na kanga wamestuka na wamechoka ngonjera zenu!
   
 3. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  umetoa ushauri mzuri ila kwasasa ndani ya CCCM hawataweza kuusikiliza hata ushauri wako
   
 4. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,769
  Likes Received: 6,098
  Trophy Points: 280
  Naam mama! Hapo kwenye red ndicho kiini hasa cha matatizo ya Tanzania chini ya utawala wa CCM hongera kwa kuliona hilo maana wenzio ndani ya chama chako ni vipofu. Katibu Mkuu aliyepita (Lt. Y. Makamba) na huyu wa sasa na hata viongozi wengine ndani ya chama lenu wana tabia ya "kuwadhihaki" sana CHADEMA na hasa Dr. Slaa kwa hilo. Utasikia wakibeza "Slaa hana jipya zaidi ya UFISADI", ndio, Dr. Slaa analenga kiini cha tatizo!

  CCM ni chama mahututi, kuwashauri sasa hivi ni kupoteza muda na nguvu zako bure. La msingi ni kuinyosha viungo kipindi hiki inapokata roho ili ienee vizuri kwenye jeneza baada ya kufa.
   
 5. beth

  beth JF-Expert Member

  #5
  Aug 14, 2016
  Joined: Aug 19, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 1,008
  Trophy Points: 180
  Shost nunu ulikuwa na maono..
  Natamani upite tena hapa uone Ngosha anavyoirudisha CCM kwenye mstari..
   
Loading...