CCM yamvua kiongozi Uanachama, yampa karipio kali Naibu Meya

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,463
39,929
CCM yacharuka

na Esther Mbussi (Tanzania Daima)


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimetoa makucha yake kwa kutoa adhabu kali ya kuwasimamisha uongozi na uanachama viongozi wawili waliokiuka maadili katika kutumikia chama chao na wananchi waliowachagua.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Katibu wa CCM mkoani Dar es Salaam, Kilumbe Ngenda, aliwataja viongozi waliokumbwa na adhabu hiyo ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Mohamed Yakub, ambaye amepewa adhabu ya onyo kali kutokana na ukiukwaji huo wa maadili na kumzuia kuwania tena nafasi hiyo. Yakub pia ni diwani wa Kata ya Mchafukoge.

Mwingine aliyekumbwa na makucha hayo ya CCM ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mnazi Mmoja, Khamis Kizenga, ambaye amevuliwa uanachama wa CCM.

Ngenda alisema uamuzi wa kutoa adhabu hizo kwa viongozi hao, umetolewa katika vikao viwili tofauti kwa mujibu wa Kanuni za Maadili toleo la 2002 na Katiba ya CCM.

Alisema adhabu ya karipio aliyopewa Yakub, imetokana na kikao cha Kamati ya Siasa ya mkoa kuridhika kuwa alitenda kosa la kushiriki katika operesheni haramu ya kuvunja nyumba za wananchi wa Tabata Dampo, kinyume cha wajibu wake kama diwani na Naibu Meya na kuitia hasara serikali ya sh bilioni 1.8.

"Pamoja na hasara hiyo kwa serikali, pia wamewapa usumbufu wananchi walioathirika na kadhia hiyo na kuleta aibu kwa chama chetu na serikali tunayoiongoza, kwa kuwa chama chetu kinaheshimu sana haki za binadamu na kusisitiza uendeshaji wa kazi na utawala kwa kuzingatia misingi ya utawala bora, hivyo kamati ya siasa ya mkoa katika kikao chake cha Julai 17, imeamua kuchukua hatua hii ili iwe fundisho kwa wengine," alisema Ngenda.

Alisema katika tukio la ubomoaji wa nyumba hizo, Yakub ameitia aibu serikali kwa kujitokeza wazi wazi kushuhudia utekelezaji wa bomoabomoa hiyo, huku akijibebesha mzigo huo wa utekelezaji.

Pamoja na adhabu ya karipio, alisema pia Halmashauri Kuu imemweka chini ya uangalizi wa kipindi cha miezi 18, ambapo hataruhusiwa kushiriki au kupewa madaraka mengine yoyote, ukiacha nafasi ya udiwani aliyonayo.

"Katika hatua hiyo, Halmashauri Kuu ya mkoa, imeteua madiwani watatu wa Wilaya ya Ilala ili kugombea nafasi ya Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala katika kamati ya madiwani wa CCM wa manispaa hiyo, kwani Yakub amemaliza muda wake na haruhusiwi kugombea tena nafasi hiyo hadi kipindi chake cha chini ya uangalizi kitakapoisha," alisema.

Ngenda aliwataja walioteuliwa kugombea nafasi hiyo na kata wanazowakilisha kwenye mabano kuwa ni Johannes Osanga Kaseno (Kitunda), Saidi Abdallah Kitambulio (Kiwalani), William Daniel (Pugu), Cecilia Macha (Charambe) na Victor Mwakasindile (Makangarawe).

Wilaya ya Kinondoni ni Julian Bujugo (Magomeni), Ibrahim Kisoki (Goba) na Omari Kimbau (Kijitonyama), na katika nafasi ya Naibu Meya wa jiji, Ahmed Mwilima amekuwa mgombea pekee aliyejitokeza kuomba nafasi hiyo.

Kwa upande wa Khamis Kizenga, katibu huyo wa CCM wa mkoa alisema, Halmashauri Kuu ya CCM, imemvua uanachama katika kikao chake kilichokutana juzi kutokana na vitendo vyake vya kukosa uaminifu, maadili ya uongozi na matumizi mabaya ya madaraka aliyokuwa nayo.

Kizenga ambaye anatuhumiwa kwa tabia yake ya kuwatukana viongozi wenzake na wananchi hadharani, kutishia kuua kiasi cha kufikia hatua ya kushtakiwa kwenye vyombo vya dola, pia amekuwa akighushi mihitasari ya vikao vya mtaa wake na kupeleka katika mamlaka za juu na kufunga moja ya barabara kwa kuweka kontena lake, kinyume cha taratibu za mipango miji.

"Pamoja na kushauriwa katika vikao mbali mbali vya chama ngazi ya tawi na wilaya kuzingatia miiko ya uongozi bila kubadilika, kikao cha Halmashauri Kuu mkoa kimeona kuwa ameshindwa kutimiza matarajio ya wananchi waliomchagua zaidi ya kuzalisha migogoro. Kwa kufanya hivyo Kizenga amekiuka miiko ya uongozi kama ilivyoainishwa kwenye Katiba ya CCM, ibara ya 18 (1) na ahadi za mwanachama fungu la (2), (3), (7) na (9)," alifafanua Ngenda.

Alisema kutokana na sababu hizo NEC mkoa, imetumia madaraka yake iliyopewa kumwachisha uanachama bila kumuonea kwa mujibu wa Katiba ya CCM Ibara ya 94 (14).

My Take:
Chama chochote kinapoona kuna tatizo katika uongozi wake hakina budi kuchukua hatua mara moja ikiwemo kumsimimasha mtu uongozi na kumnyima madaraka (Naibu Meya) au kumfuta Uanachama (Kizenga). Hata hivyo ukiangalia utaona kuwa Kizenga amepewa adhabu nzito sana na chama chake kulinganisha na makosa anayotuhumiwa nayo.

Zaidi ya yote kwa viongozi wote wawili sijui wana nafasi gani ya kukata rufa kupinga maamuzi ya chama chao.

Kwa upande wa Naibu Meya, ni wazi kuwa amepewa adhabu ndogo zaidi kulinganisha na kosa lake ambalo limeisababishia serikali hasara ya Shs. Bilioni moja. Kwa mtindo huu kweli chini ya CCM tutafika?

Kinachonisumbua mimi ni kuwa katika nchi yenye kuheshimu sheria inakuwaje mtu aliyesababisha serikali (siyo chama) hasara ya Bilioni 1.8 anaendelea na madaraka wakati wale jamaa wa Wazazi waling'olewa uongozi kwa kusababisha hasara ya tumilioni tuchache twa CCM? Je fedha ya CCM inauma zaidi?
 
Kama hawana taarifa hapo ni huyo Omari Kimbau anatafutiwa nafasi!
Huyo ni mtoto wa Kanali Kimbau na wao kama kina Kinje tu nasikia Dar ni yao!
Sasa kama ufisadi hautashughulikiwa mimi nafikiri hata wao wasije kushangaa kukageuka na kuwa shubiri.
Kwani kwa mwenendo ulivyo...Bado inaonyesha ccm nao wanajipanga kwa ajili ya kuendelea kulinda ufisadi.
Huyu Kimbau kuna mtu ana data zake?
Maana naona ni uongozi hapo sasa...Sijuwi ni umeya ama nini.
Huku nasikia na Zainabu Kawawa na kina Nape nao wamo!
Sasa kama ufisadi haujashughulikiwa hao ndio watakaopelekea matatizo kwani hao ndio usalama wa Taifa na BOT na kila kitu.
 
Tatizo sio kufika tu. Naona kwa sasa CCM wamepoteza hata mwelekeo wa wapi tunaelekea. Sijui tutajuaje tumefika kama tunakokwenda hatujui. Kinachosikitisha zaidi hapa ni viongozi wa chini wanaofanya makosa madogo wanapata adhabu kubwa kweli kweli (kufutwa uanachama), wakati viongozi wakubwa wanaofanya makosa makubwa (asara ya 1.8 bilioni) au kubwa zaidi za Richmond, EPA, n.k. wnanendelea kupewa nafasi ya kutuumiza zaidi. Hapa hakuna kufika wala nini, ni kuzunguka tuuu
 
Siasa hapa nikulindana na kujilinda, sijaona jipya hata chembe. Inasikitisha sana.

Mw Nyerere alidesign system nzuri sana that why leo hii kila mtu mwalimu na fikra zake, implementors wamekuwa na mawazo ya Mwalimu na ya watu wao wanaowapa kula na waliowasaidia. wanajichanganya hawa watawala na hawajui washike wapi na sijui hata zile maths techniques za projection and whatever hawajazisoma kujua tunaenda wapi? Nini kazi ya usalama wa taifa? kuangalia akaunti za watu zisitolewe hadharani? hivi mnajua somo lililopatikana baada ya mkuu wa kitongoji kula dola 800 akafungwa miaka 10 wakati waleeeeee wanapeta? hamjui kama watu wanavamia vituo vya polisi, hamjui kama waalimu sasa wanachapwa viboko wanafunzi wao? achilia mbali migomo ya hapa na pale. haya yote mnafikiri wengine wanajifunza nini?

Hatua za haraka kuanzia system design, implementation and physical condition has to be reviewed and treat everybody fairly.

asante
 
Kwa upande wa Naibu Meya, ni wazi kuwa amepewa adhabu ndogo zaidi kulinganisha na kosa lake ambalo limeisababishia serikali hasara ya Shs. Bilioni moja. Kwa mtindo huu kweli chini ya CCM tutafika?

Mwanakijiji niko gizani kidogo, is it true ni kwa sababu ya kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni moja, au kuna sababu nyingine na hiyo inatumiwa kama excuse? Maana ukweli ambao wote tunaufahamu ni kuwa kwenye Chama ukiwa mwizi hasa mwizi mkubwa utalindwa, ukiwa mzembe hasa mzembe mkubwa unahamishwa post na sio kuondolewa au kusumamishwa uanachama. Kuna mifano 100 ambayo tunaweza kuitoa kuhusu haya, kuna EPA, Import support, Richmond etc etc . Huyu jamaa kutakuwa na sababu nyingine ambayo bado haijulikani.
 
Huu unatakiwa kuwa mfano kwa wengine, kama kuna kiongozi ana matatizo dawa ni kuyaweka wazi na kuchukua hatua, lakini sio kuzunguka zunguka weee mwisho hakuna, wakati tatizo halitatuliwi viongozi wanarushiana maneno yasiyokuwa na maana umauzi mzito hautolewi that is nonesense,

Kiongozi ana kosa weka makosa yake hadharani, toa adhabu end of the story, sio never ending story maneno hayaishi, mpaka huelewi anyesema ukweli ni nani na anayesema uongo ni nani.
 
CCM isiishie kuwaadhibu wadogo

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), juzi kilionyesha kuwa kinaweza kuwachukulia hatua viongozi wake wanaokiuka miiko ya maadili ya uongozi, baada ya kutoa adhabu ya kuwasimamisha uongozi na uanachama viongozi wawili, kwa madai ya kukiuka maadili katika kukitumikia chama hicho na wananchi waliowachagua.

Taarifa ya adhabu kwa viongozi hao, ilitolewa na Katibu wa CCM mkoani Dar es Salaam, Kilumbe Ngenda. Aliwataja waliokumbwa na adhabu hiyo kuwa ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Mohamed Yakub, na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mnazi Mmoja, Manzese, Khamis Kizenga.

Yakub amepata adhabu ya onyo kali baada ya kubainika kuwa alishiriki katika operesheni ya kuvunja nyumba za wakazi wa Tabata Dampo, Dar es Salaam, kinyume cha wajibu wake kama diwani na naibu meya na hivyo kuitia hasara serikali ya sh bilioni 1.8 ya kuwalipa fidia wakazi hao. Yakub pia ni Diwani wa Kata ya Mchafukoge.

Pamoja na uzito wa kosa hilo, Yakub amepewa adhabu ya onyo kali kutokana na ukiukwaji huo wa maadili. Pia amezuiliwa kuwania tena nafasi hiyo.

Mbali ya adhabu ya karipio, meya huyo pia amewekwa chini ya uangalizi wa kipindi cha miezi 18 na hataruhusiwa kushiriki au kupewa madaraka mengine yoyote, ukiacha nafasi ya udiwani aliyonayo sasa.

Wakati Yakub akipata adhabu ya onyo kali, Kizenga alijikuta akivuliwa uanachama wa CCM kwa madai ya kukosa uaminifu, maadili ya uongozi na matumizi mabaya ya madaraka aliyokuwa nayo.

Inasemekana kuwa Kizenga alikuwa na tabia ya kuwatukana viongozi wenzake na wananchi hadharani, kutishia kuua kiasi cha kufikia hatua ya kushitakiwa kwenye vyombo vya dola. Hali kadhalika amekuwa akighushi mihutasari ya vikao vya mtaa wake na kupeleka katika mamlaka za juu na kufunga moja ya barabara kwa kuweka kontena lake kinyume cha taratibu za mipango miji.

Tunaunga mkono hatua zote za CCM za kuwachukulia hatua viongozi hao, ili iwe fundisho kwa wengine ndani ya chama hicho tawala wenye na tabia ya kujifanya miungo watu katika maeneo wanayoongoza, huku wengine wakijihusisha na vitendo vya ufisadi unaoliangamiza taifa.

Lakini adhabu walizopewa viongozi hao hasa ile ya Naibu Meya Yakub ni ndogo sana ikilinganishwa na uzito wa kosa lake. Kitendo alichokifanya Yakub cha kujitokeza waziwazi kushuhudia utekelezaji wa bomoabomoa ya Tabata Dampo, huku akijibebesha mzigo huo wa utekelezaji, si tu kwamba imewapa usumbufu wananchi walioathirika na kadhia hiyo, bali pia imekitia aibu chama hicho na serikali inayoiongoza.

Lakini adhabu za aina hiyo - licha ya udogo wake - zisiishie kutolewa kwa watumishi wadogo kama hawa. Hivi karibuni taifa limeshuhudia baadhi ya viongozi wakubwa wa CCM waliokuwa na nyadhifa serikalini wakikumbwa na kashfa za ufisadi hadi kujiuzulu nafasi hizo.

Wapo viongozi waliolisababishia taifa hasara ya mabilioni ya shilingi kutokana na kuingia mikataba tata ambayo hadi leo inaliangamiza taifa, lakini wapo, chama kina waona na hakiwachukulii hatua.

Tabia ya kuonyesha makucha na hata kuchukua hatua kwa watendaji wadogo na kuwaacha wakubwa, haikijengi chama hicho zaidi ya kujiweka katika mazingira magumu ya kuendelea kuliongoza taifa hili kwa kufuata misingi ya utawala bora katika miaka ijayo.

Source-Tanzania Daima Julai 22, 2008
 
Omari Kimbau ni mtoto wa mjini..tatizo lake elimu yake ni ndogo na anaiogopa Siasa. Hiyo ndio sababu alikuwa nyuma ya Ippy Malecela (RIP) na Kinje. Yeye mwenyewe akisimama siasa haiwezi lakini naona watu wanamtengenezea njia. Hiyo nafasi ya kugombea Unaibu Meya atakuwa ametupiwa kwa sababu ana Jina la "KIMBAU". Ukiondoa jina yeye mwenyewe kwenye siasa ni zero kabisa. Hata hivyo nina mashaka iwapo hiyo kazi ataiweza, ni kijana mayai sana kuwa naibu meya wa jiji la Dsm. Anyway, kuna namna nyingi hawa wanaotaka kumuweka wanaweza kumlinda ili aonekane anawajibika ipasavyo.

Kinje atakuwa anafurahia maana Kimbau akichaguliwa atakuwa na mtu wake wa karibu sana kwenye maamuzi yote ya Jiji...sitashangaa iwapo tukisikia amepata kibali cha kufungua ukumbi wa Disco Ikulu.!!! Time will tell
 
Wanataka wanaCCM wa ngazi za chini walalamike kuwa wao ndio wanachukuliwa hatua ili uongozi uweze kuwachukulia hatua mafisadi?
 
Omari Kimbau ni mtoto wa mjini..tatizo lake elimu yake ni ndogo na anaiogopa Siasa. Hiyo ndio sababu alikuwa nyuma ya Ippy Malecela (RIP) na Kinje. Yeye mwenyewe akisimama siasa haiwezi lakini naona watu wanamtengenezea njia. Hiyo nafasi ya kugombea Unaibu Meya atakuwa ametupiwa kwa sababu ana Jina la "KIMBAU". Ukiondoa jina yeye mwenyewe kwenye siasa ni zero kabisa. Hata hivyo nina mashaka iwapo hiyo kazi ataiweza, ni kijana mayai sana kuwa naibu meya wa jiji la Dsm. Anyway, kuna namna nyingi hawa wanaotaka kumuweka wanaweza kumlinda ili aonekane anawajibika ipasavyo.

Kinje atakuwa anafurahia maana Kimbau akichaguliwa atakuwa na mtu wake wa karibu sana kwenye maamuzi yote ya Jiji...sitashangaa iwapo tukisikia amepata kibali cha kufungua ukumbi wa Disco Ikulu.!!! Time will tell

Kimbau na Kinje na wengineo nadio mabosi wa Dar.
Na ccm imeamuwa kuwafanya hao ndio wanausalama wa mali za wananchi.
Sasa ndio maana nauliza...Kwasababu keshaamuwa kuingia kwenye siasa kama wenzake...Kuna mtu mwenye data zake?
Maana umakamu Meya si kitu kidogo na sasa nasikia watoto wa vigogo wanatekwa nyara huko bongo.
Maelezo yako hapo juu inaelekea una tunyeti flani flani...Sasa kama anaingia kwenye siasa ni bora umwage mambo hapa jf.
 
Humu jf kuna mafisadi wengi sana tu na watu wa kila aina WENGINE SAFI.
Na ndio maana halisi ya jamii yetu.
Hii naona hata haiguswi...Tungependa kujulishwa mara baada ya taarifa ya nini kinachoendelea kwani zamu ya watoto wa vigogo imeisha na sasa ni watanzania wote na yeyote yule almuradi hana haja ya kuwa na jina la kigogo!
Mabadiliko ni LAZIMA!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom