Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,370
- 39,186
CCM yacharuka
na Esther Mbussi (Tanzania Daima)
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimetoa makucha yake kwa kutoa adhabu kali ya kuwasimamisha uongozi na uanachama viongozi wawili waliokiuka maadili katika kutumikia chama chao na wananchi waliowachagua.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Katibu wa CCM mkoani Dar es Salaam, Kilumbe Ngenda, aliwataja viongozi waliokumbwa na adhabu hiyo ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Mohamed Yakub, ambaye amepewa adhabu ya onyo kali kutokana na ukiukwaji huo wa maadili na kumzuia kuwania tena nafasi hiyo. Yakub pia ni diwani wa Kata ya Mchafukoge.
Mwingine aliyekumbwa na makucha hayo ya CCM ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mnazi Mmoja, Khamis Kizenga, ambaye amevuliwa uanachama wa CCM.
Ngenda alisema uamuzi wa kutoa adhabu hizo kwa viongozi hao, umetolewa katika vikao viwili tofauti kwa mujibu wa Kanuni za Maadili toleo la 2002 na Katiba ya CCM.
Alisema adhabu ya karipio aliyopewa Yakub, imetokana na kikao cha Kamati ya Siasa ya mkoa kuridhika kuwa alitenda kosa la kushiriki katika operesheni haramu ya kuvunja nyumba za wananchi wa Tabata Dampo, kinyume cha wajibu wake kama diwani na Naibu Meya na kuitia hasara serikali ya sh bilioni 1.8.
"Pamoja na hasara hiyo kwa serikali, pia wamewapa usumbufu wananchi walioathirika na kadhia hiyo na kuleta aibu kwa chama chetu na serikali tunayoiongoza, kwa kuwa chama chetu kinaheshimu sana haki za binadamu na kusisitiza uendeshaji wa kazi na utawala kwa kuzingatia misingi ya utawala bora, hivyo kamati ya siasa ya mkoa katika kikao chake cha Julai 17, imeamua kuchukua hatua hii ili iwe fundisho kwa wengine," alisema Ngenda.
Alisema katika tukio la ubomoaji wa nyumba hizo, Yakub ameitia aibu serikali kwa kujitokeza wazi wazi kushuhudia utekelezaji wa bomoabomoa hiyo, huku akijibebesha mzigo huo wa utekelezaji.
Pamoja na adhabu ya karipio, alisema pia Halmashauri Kuu imemweka chini ya uangalizi wa kipindi cha miezi 18, ambapo hataruhusiwa kushiriki au kupewa madaraka mengine yoyote, ukiacha nafasi ya udiwani aliyonayo.
"Katika hatua hiyo, Halmashauri Kuu ya mkoa, imeteua madiwani watatu wa Wilaya ya Ilala ili kugombea nafasi ya Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala katika kamati ya madiwani wa CCM wa manispaa hiyo, kwani Yakub amemaliza muda wake na haruhusiwi kugombea tena nafasi hiyo hadi kipindi chake cha chini ya uangalizi kitakapoisha," alisema.
Ngenda aliwataja walioteuliwa kugombea nafasi hiyo na kata wanazowakilisha kwenye mabano kuwa ni Johannes Osanga Kaseno (Kitunda), Saidi Abdallah Kitambulio (Kiwalani), William Daniel (Pugu), Cecilia Macha (Charambe) na Victor Mwakasindile (Makangarawe).
Wilaya ya Kinondoni ni Julian Bujugo (Magomeni), Ibrahim Kisoki (Goba) na Omari Kimbau (Kijitonyama), na katika nafasi ya Naibu Meya wa jiji, Ahmed Mwilima amekuwa mgombea pekee aliyejitokeza kuomba nafasi hiyo.
Kwa upande wa Khamis Kizenga, katibu huyo wa CCM wa mkoa alisema, Halmashauri Kuu ya CCM, imemvua uanachama katika kikao chake kilichokutana juzi kutokana na vitendo vyake vya kukosa uaminifu, maadili ya uongozi na matumizi mabaya ya madaraka aliyokuwa nayo.
Kizenga ambaye anatuhumiwa kwa tabia yake ya kuwatukana viongozi wenzake na wananchi hadharani, kutishia kuua kiasi cha kufikia hatua ya kushtakiwa kwenye vyombo vya dola, pia amekuwa akighushi mihitasari ya vikao vya mtaa wake na kupeleka katika mamlaka za juu na kufunga moja ya barabara kwa kuweka kontena lake, kinyume cha taratibu za mipango miji.
"Pamoja na kushauriwa katika vikao mbali mbali vya chama ngazi ya tawi na wilaya kuzingatia miiko ya uongozi bila kubadilika, kikao cha Halmashauri Kuu mkoa kimeona kuwa ameshindwa kutimiza matarajio ya wananchi waliomchagua zaidi ya kuzalisha migogoro. Kwa kufanya hivyo Kizenga amekiuka miiko ya uongozi kama ilivyoainishwa kwenye Katiba ya CCM, ibara ya 18 (1) na ahadi za mwanachama fungu la (2), (3), (7) na (9)," alifafanua Ngenda.
Alisema kutokana na sababu hizo NEC mkoa, imetumia madaraka yake iliyopewa kumwachisha uanachama bila kumuonea kwa mujibu wa Katiba ya CCM Ibara ya 94 (14).
My Take:
Chama chochote kinapoona kuna tatizo katika uongozi wake hakina budi kuchukua hatua mara moja ikiwemo kumsimimasha mtu uongozi na kumnyima madaraka (Naibu Meya) au kumfuta Uanachama (Kizenga). Hata hivyo ukiangalia utaona kuwa Kizenga amepewa adhabu nzito sana na chama chake kulinganisha na makosa anayotuhumiwa nayo.
Zaidi ya yote kwa viongozi wote wawili sijui wana nafasi gani ya kukata rufa kupinga maamuzi ya chama chao.
Kwa upande wa Naibu Meya, ni wazi kuwa amepewa adhabu ndogo zaidi kulinganisha na kosa lake ambalo limeisababishia serikali hasara ya Shs. Bilioni moja. Kwa mtindo huu kweli chini ya CCM tutafika?
Kinachonisumbua mimi ni kuwa katika nchi yenye kuheshimu sheria inakuwaje mtu aliyesababisha serikali (siyo chama) hasara ya Bilioni 1.8 anaendelea na madaraka wakati wale jamaa wa Wazazi waling'olewa uongozi kwa kusababisha hasara ya tumilioni tuchache twa CCM? Je fedha ya CCM inauma zaidi?