Ccm yamtosa 6

Alaigwanani

Member
Nov 9, 2010
15
0
Sitta, Chenge watupwa Send to a friend Thursday, 11 November 2010 00:16 0diggsdigg

kiliositta.jpg
Mr Samwel Sitta akiwa ameshika kichwa

Habel Chidawali, DodomaKAMATI Kuu ya CCM imewapitisha Anna Abdallah, Anna Makinda na Kate Kamba kuingia katika kinyanganyiro cha uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupita chama hicho.Hata hivyo majina hayo yatapelekwa kwenye Halmashauri Kuu ya CCM kwa ajili ya kumpata mgombea mmoja atakayechuana na wagombea wengine watakaojitokeza kuwani uspika.
Matokeo hayo yamewatupa nje wagombea wanaume walioomba nafasi hiyo kupitia CCM wakiwemo mahasimu wawili Samuel Sitta aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa na Andrew Chenge. Wanachama 13 wa CCM waliomba kuteuliwa kuwania nafasi hiyo nyeti katika Bunge ambacho ni chombo cha juu cha kutunga sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba alisema wamechukua uamuzi huo wakizingatia kuwa umefikia wakati wanawake waongoze vyombo vya dola.

"Watanzania wote wanafahamu utendaji wa Spika aliyepita hatuna tatizo naye, lakini chama chetu kupitia Kamati Kuu kimeona kuwa umefika wakati wa wanawake kupewa muhimili japo mmoja wa dola," alisema Makamba.

Kupitishwa kwa akina mama hao ambao wanaonekana kuwa na uzoefu wa aina tofauti katika siasa ndani na nje ya CCM, kunakipa chama hicho changamoto kubwa katika kuongoza Bunge la 10 ambalo lina wabunge wengi wa upinzani na wenye uwezo mkubwa tofauti na ilivyokuwa katika mabunge yaliyopita.

Mara baada ya kutolewa taarifa hizo umati watu waliouwa wamefika katika mkutano huo uliofanyika katika jengo Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma walinyong'onyea, huku baadhi yao wakisema mapendekezo ya kamati kuu ni tofauti ya matarajio yao.

Chini ya Sitta, Bunge lililopita liliweza kuonyesha dhahiri uwezo wake kwa kuzingatia Sheria na kutoa maamuzi yalioongeza demokrasia bungeni.

Awali mahasimu wawili waliokuwa wakiwania kiti cha uspika, Chenge na Sitta walionekana kuficha uhasama wao kwa kukumbatiana mbele ya wajumbe wa Kamati Kuu walipokuwa ukumbini.

Kikao cha Kamati Kuu kilichokutana kwa ajili ya kuteua majiba ya wanaowania uspika kupitia CCM kilianza saa 9:25 za jioni na kilihudhuriwa na wajumbe 35 kati ya wajumbe 39 waliotakiwa kushirikia katika kikao.

Chenge aliyekuwa amekaa na Makinda kwenye ukumbi wa mkutano alikuwa wa kwanza kumuita Sitta alipoingia ukumbini.

Sitta alipoingia ukumbini aliwasalimia wajumbe wa mkutano huo kwa kuwapungia mkono, lakini Chenge alimuita kumtaka wasalimiane kwa karibu naye bila ya kusitaalikwenda katika kiti wakasalimiana na kukumbatiana.

“Haya ni mambo ya kawaida naona waandishi wa habari wanataka kuchukua na picha wakidhani kuwa ni jambo kubwa. Ndani ya CCM hivi ni vitu vya kawaida tu,” alisema Sitta.

Kikwete aliwaambia wajumbe wa kamati hiyo kuwa kikao kilikuwa ni halali kwani kilihudhuriwa na wajumbe wengi na kuwataja walishindwa kuhudhuria kuwa ni Benjamin Mkapa, Dk Salmin Amour pamoja na Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambaye hata hivyo, cheo hicho hakipo kwa sasa.

Kabla ya mkutano huo kuanza katibu wa CCM, Yusufu Makamba alimuita Naibu Katibu Mkuu, Kapteni George Mkuchika na kuteta naye kabla ya kumuita Katibu wa Itikadi na Uenezi, Kapteni John Chiligati amba walisimama kwa dakika kadhaa kisha wakaingia kwenye chumba alichokuwepo mwenyekiti Jakaya Kikwete.

Kikwete aliingia katika kikao hicho akiongozana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa, Makamu Mwenyekiti (Zanzibar), Aman Karume, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassani Mwinyi na Waziri MKuu Mstaafu, John Malecela.

Baada ya kikao kufunguliwa hicho Mwenyekiti wa CCM aliwaambia wajumbe kuwa cheo kilichokuwa cha Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hakipo tena hivyo nafasi hiyo itachukuliwa na makamu wa pili wa rais.

“Hapa katiba haisemi hivyo, lakini huu ndio ukweli kuwa cheo cha Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hakipo tena, hivyo naamini kuwa nafasi hiyo inatakiwa kuchukuliwa na Makamu wa Pili wa Rais ingawa,” alisema Kikwete.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom