CCM yamtaka Mongella asipate kigugumizi kuwashughulikia polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yamtaka Mongella asipate kigugumizi kuwashughulikia polisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 8, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Monday, 07 March 2011 20:55 0diggsdigg

  Anthony Kayanda, Kigoma
  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) katika Wilaya ya Kigoma Mjini, kimetoa tamko kali dhidi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya hiyo, kufuatia kitendo cha baadhi ya Polisi kutuhumiwa kuhusika katika jaribio la kuteka nyara gari na kupora fedha za mishahara ya wafanyakazi wa Kampuni ya Chico, inayojenga Barabara ya Kidahwe-Ilunde, mkoani Kigoma.

  Tamko hilo lilitolewa juzi na Katibu wa CCM wa Wilaya ya Kigoma Mjini, Ally Shamte wakati wa mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika eneo la Urusi mjini hapa.Alisema CCM katika kikao chake cha Kamati ya Siasa ilimtaka Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, John Mongella, aache kigugumizi kuhusu kuwachukulia hatua kali za kisheria, askari polisi waliotajwa kuhusika katika mpango wa kuteka nyara, gari la Kampuni ya Chiko, kwa lengo la kupora fedha.

  "Chama chetu kimekuwa kikilaumiwa sana na wananchi kutokana na vitendo vya aina vinavyofanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu na kamwe hatuwezi kukubali jambo hilo na ndio maana Kamati ya Siasa katika Kikao chake,imetoa tamko la kumtaka Mkuu wa wilaya aache kigugumizi. Tunataka kuona amechukua hatua dhidi ya polisi waliotaka kupora fedha za Wachina," alisema Shamte.

  Kwa mujibu wa katibu huyo, chama chake kimechoka kuona kero za aina hiyo zikikithiri siku hadi siku wakati kuna serikali."Sheria lazima ichukue mkondo wake na kama chama, tutahakikisha kuwa ukweli unadhihirika katika tukio hilo la ujambazi," alisisitiza Shamte.

  Alihoji uhalali wa polisi kumkamata dereva wa gari lililohusika katika tukio la ujambazi huo katika Kijiji cha Kidahwe ambaye anadaiwa kulikodisha kwa Polisi mmoja aliyetajwa kwa jina la PC Christopher ambaye alidai anataka aendeshe mwenyewe kwa sababu ana kazi nalo binafsi na hivyo hahitaji dereva.

  Shamte alisema polisi mkoani Kigoma pia lazima watoe maelezo kuhusu kuugua ghafla kwa dereva wa teksi aliyekamatwa baada ya gari lake, kutumika katika tukio hilo.

  "Polisi waeleze kwa nini yule dereva teksi akamatwe akiwa mzima na baadaye kupelekwa hospitalini akiwa mahututi.Tunataka kujua ukweli wa tukio zima kwa sababu sasa imekuwa kero kwa jamii na wananchi wanaishutumu CCM kwamba ndio chanzo cha matukio haya," alisema.
  Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
   
Loading...