CCM Dar yamtaka Dr. Magufuli aombe radhi

Hapo Magufuli kalikoroga mwenyewe inabidi alinywe! Kupenda sifa na dharau ndio hulka yake, sasa kakutana na watoto wa mjini! Hayo matamko si bure yawezekana kuna wakubwa wapo nyuma! Yeye hana budi tu kusema samahani halafu mambo yaishe. Otherwise,hii kitu itamsumbua tu na hakika inamsumbua!
 
Mawaziri wasiwe wabunge au wanasiasa.
Kwani ukiwa haumudu nauli si unatembea?... sasa utatembeaje juu ya maji?.... piga mbizi.
 
kivuko si sawa na daraja

kivuko kinahitaji
1.ukarabati wa kila wakati
2.mafuta kwa ajili ya kukiendesha
3.mishahara kwa watakao kihudumia

lakini daraja halina mahitaji hayo,unadhani bila pesa kivuko kitaendeshwa vipi?

mashangingi yao yanaendeshwa vp?
 
kivuko si sawa na daraja

kivuko kinahitaji
1.ukarabati wa kila wakati
2.mafuta kwa ajili ya kukiendesha
3.mishahara kwa watakao kihudumia

lakini daraja halina mahitaji hayo,unadhani bila pesa kivuko kitaendeshwa vipi?
Mbona nchi nyengine kama Kenya watu wanapanda bure,na si kivuko kama cha Kigamboni bali mavyombo kweli na yanafanya kazi kweli masaa yote mpaka saa 9 usiku.Yeye Magufuli akienda nje si anaona mwenyewe.
 
Mbona nchi nyengine kama Kenya watu wanapanda bure,na si kivuko kama cha Kigamboni bali mavyombo kweli na yanafanya kazi kweli masaa yote mpaka saa 9 usiku.Yeye Magufuli akienda nje si anaona mwenyewe.
Marekani wanalipa.
Halafu halmashauri ya jiji inaweza kununua kivuko na kusafirisha watu bure.... sema ndiyo hivyo tena hata sehemu za watoto kucheza zimegeuzwa sehemu za maduka.
Serikali zetu za mitaa ni upotevu wa posho na mishahara. Huwezi kuilaumu wizara kama haina fedha, labda tu ungeuliza jiji la Dar huwa linakusanya mapato ya kiasi gani?.. Halafu fananisha na Mombasa.
 
Magufuli amejichafua bure wakati daraja la Kigamboni kwa upande wa kurasini liko njiani kujengwa.Kwani likimalizika lile kutakuwa na haja tena ya kuvuka na Pantoni?.
 
"With friends like these who needs enemies?. CCM wanajimaliza wenyewe na adui yao mkubwa ni wao wenyewe wala sio upinzani.

Guninita amefanya nini la maana kwenye hili jiji la Dar? Mafuriko yametokea Dar, Magufuli bila kujali ni x'mas alikuwa barabarani akisimamia ukarabati wa madaraja, Guninita na wenzake walikuwa wapi? Kwa nini Guninita hakumtaka Waziri wa Ulinzi awaombe radhi wakazi wa Dar kutokana na milipuko ya mabomu licha za waziri ahadi kwamba hayatarudia? Watu wamepoteza maisha, kwanini Guninita hakujitokeza kwenye vyombo vya habari na kudai msahama wa waziri wa ulinzi?

Nahiisi wabunge wa Dar wamoena ngoma nzito wakaamua kujificha kwenye hii ngozi ya 'ccm-mkoa wa Dar' ili wamkomoe Magufuli. Juzi Magufuli amesema anataka kivuko kijitegemee lakini pia anataka kutumia kiasi cha fedha kitakachopatikana ili kujenga vifuko vingine ili kupunguza tatizo la usafiri Dar. Sasa Guninita analeta porojo gani hapa? Hili tatizo limekuzwa na hawa hawa wabunge wa ccm -Dar. Na ni aibu kubwa kuona hawa mufilisi wakiendeleza ngonjera kwenye vyombo vya habari kwa mambo yaliyo wazi kabisa. Mbali na Magufuli ccm wana waziri gani mwingine mchapa kazi? Wassira? Kawambwa? Ngeleja?

Magufuli usirudi nyuma wafanye wanalotaka lakini usirudi nyuma kabisa kabisa. Na kwa Guninita na wenzake, wahanga wa mafuriko bado hawana mahali pa kukaa, huko wanakopelekwa hakuna chochote ni viwanja vitupu sijui watalala wapi hadi watakapojenga nyumba! Je, mnaoliona hilo au kila kukicha mnawaza namna ya kushambuliana?

Mmeshindwa kusimamia maamuzi yenu ya siku tisini sasa mnataka pa kutokea!

mala nyingi sana nimefuatilia mwenendo wa ccm juu ya magufuli,kinachoonekana ni kutaka kumrudisha nyuma magufuli na aonekane kuwa si lolote ktk ccm ya leo,kama unakumbuka ktk ile bomoabomoa wakuu wote wa serikali walimjia juu magufuli na kumtaka asitishe zoezi hilo tena hadharani wala hakukuwa na vikao vya ndani kuongea nae,

kwa hiyo hapa nachokiona mimi ni ile hali ya uchapakazi wake inayowafanya baadhi ya wanaccm kuona kuwa magufuli anmepiga hatua kubwa zaidi ktk usimamiaji wa kazi na hata watu wanakubaliana nae kwa hiyo upatikanapo mwanya wa kumbomoa basi wanaccm wenyewe hufanya hivyo tena hadharani ili kutimiza malengo yao

Mh Magufuli tupo nyuma yako,mala nyingi chema hakipendwi hata iweje,kwa hiyo usikatishwe tamaa na chama chako piga kazi mkuu
 
Watanzania fungeni mikanda, hata kma mtakula nyasi lazima ndege ya raisi inunuliwe, watanzania mna wivu wa kijinga, mna wivu wa kike, mtoto wa selemala atakuwa selemala, pigeni mbizi, wakuja, kiherehere chao kupata mimba...n.k. HIVI KATI YA WALIOTOA HIZO KAULI HAPO JUU YUPI ANASTAHILI KUOMBA RADHI?
 
Dr Magufuli anatakiwa kuomba radhi watanzania kwa mambo mengi mfano uuzaji wa nyumba za serikali
 
Guninita ni makapi ya siasa za fitina na majungu. Kisomo chake ni darasa la 7 na hajawahi kushtuka hata kufanya distance learning au MEMKWA maarufu kama QT. Na huo uenyekiti wa mkoa alipewa tu kama.fadhila na akina EL kwa kuwa alikuwa ameshafulia vibaya
 
Kwanza ifahamike, kivuko si jambo la biashara, ni moja kati ya majukumu na wajibu wa serikali kuhakikisha kwamba raia wanafika sehemu moja kutoka ingine, na kivuko ni sawa na daraja. Kama serikali imeshindwa kujenga daraja kati ya magogoni na kigamboni, si haki kwao kutoza wananchi wanaovuka hapo, na ikiwa hivyo ndivyo basi hata yale madaraja makubwa wawe wanatoza nauli

Nami nimekuwa na mtazamo kama wako. Kivuko ni kiunganishi kutoka upande mmoja hadi mwingine kama ilivyo barabara. Serikali ina wajibu wa kuhakikisha raia wake wanaweza kwenda upande mwingine bila gharama ya ziada (kumbuka mwananchi wake alitanguliza kodi). Huwa hatupendi kulinganisha nchi a nchi lakini Mombasa kuna kivuko kikubwa sana kinachounga new and old town ambacho hakitozi nauli kwa wavukaji. Labda tu tuseme wakazi wa kigamboni wamestuka kugomea ongezeko la nauli kwa sasa lakini cha msingi walitakiwa kugomea kulipa kabisa tokea mwanzo!
Upande wa radhi sitegemei Magufuli aombe coz ndio kauli zao tunazozisikia kila siku!
 
Nakuunga mkono asilimia mia 200. Siasa na kazi wapi na wapi!!! Big up Magufuli!!!
Hakuna haja ya kuomba radhi, Panton limeua watu wengi tangu enzi ya kina Mustafa Nyang'anyi na watu hawakuombwa radhi, ni mara ngapi yalikufa mapantoni ya Kigamboni watu wakakosa huduma leo watu wa Dsm hawataki kufikiri, likifa na hilo hao wabunge watachangia?
Kwa hilo bora magufuli ajiuzulu nauli hakuna kushuka na CCM haihusiki (Itenganisha Siasa na kazi) na usalama wa watu au majini watakapozama
 
Hakuna haja ya kuomba radhi, Panton limeua watu wengi tangu enzi ya kina Mustafa Nyang'anyi na watu hawakuombwa radhi, ni mara ngapi yalikufa mapantoni ya Kigamboni watu wakakosa huduma leo watu wa Dsm hawataki kufikiri, likifa na hilo hao wabunge watachangia?
Kwa hilo bora magufuli ajiuzulu nauli hakuna kushuka na CCM haihusiki (Itenganisha Siasa na kazi) na usalama wa watu au majini watakapozama

well said Ukwaju! we are tired and sick of these hopeless and rhetoric good for nothing politicians! Ni kweli Maghufuli bora awaachie wao wafanye hiyo kazi kama wanaona ni rahisi tuone kama wataweza!
 
Hakuna haja ya kuomba radhi, Panton limeua watu wengi tangu enzi ya kina Mustafa Nyang'anyi na watu hawakuombwa radhi, ni mara ngapi yalikufa mapantoni ya Kigamboni watu wakakosa huduma leo watu wa Dsm hawataki kufikiri, likifa na hilo hao wabunge watachangia?
Kwa hilo bora magufuli ajiuzulu nauli hakuna kushuka na CCM haihusiki (Itenganisha Siasa na kazi) na usalama wa watu au majini watakapozama
Nakuunga mkono. Hawa wanasiasa wanafiki sana. Magufuli hakuna kuomba radhi
 
kivuko si sawa na daraja

kivuko kinahitaji
1.ukarabati wa kila wakati
2.mafuta kwa ajili ya kukiendesha
3.mishahara kwa watakao kihudumia

lakini daraja halina mahitaji hayo,unadhani bila pesa kivuko kitaendeshwa vipi?

we ni eng wa kitu gani jamaa yangu!?
Unafikiri madaraja hayawi mantained?
Sio kazi ya raia kugharamikia kivuko, ile ni huduma ambayo wananchi wanatakiwa kuchangia tu. Ni jukumu la serikali kuhakikisha watu wanavuka pale, kwa panton, daraja au kupiga mbizi.

Ngoja wanyooshane kwanza....halafu wataitwa kwenye kamati kuu na kupigwa mkwala, na watanyamaza wote kama kawaida yao. Na wananchi wataendelea kuteseka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom