CCM yampongeza Spika Ndugai kwa kutoka hadharani na kumuomba msamaha Rais Samia

Chama kimetoa kauli lini? Wasira msemaji wa chama? Tukumbushane, chama ni vikao, kauli ya chama inapaswa itokane na maamuzi ya vikao. Suala la kukemea uasi,maadili mapaya, kukisemea chama vizuri ni kazi za kila siku za wanachama, ila kupongeza, kukubali radhi, kulaani jambo inapaswa ipitie kwenye vikao stahili, je wamekutana saa ngapi?
 
Maneno yakishatamkwa hayarudishiki mdomoni
Ni kwa vile tu Tanzania imejaa wanafki, wakati anaropoka pumba zake kuna watu alikuwa anawahutubia, leo anasema clip imetengezwa, ningekuwa mimi ni mmoja ya tuliokuwa tunamsikiliza na mimi ningeitisha press conference na kumtaka Ndugai aache kudanganya umma ile clip haijachezewa ni Bonafide genuine.
 
Mzee Stephen Wassira amesema CCM imeridhishwa na kitendo cha Spika Ndugai kutoka hadharani na kuomba msamaha kwa Rais Samia na wananchi kwa ujumla kufuatia kauli aliyoitoa kuhusu Mikopo kutoeleweka sawasawa.

Mzee Wassira amesema Spika Ndugai kwa upande wake ameshafunga mjadala na CCM wamemuelewa.

Mzee Wassira yuko mubashara na Aloyce Nyanda wakijadili mambo mbalimbali ya kisiasa.

Source: The Big Agenda Star tv

Kuna Uzi wako umeusahau huku 😁😁
 
Back
Top Bottom