CCM yampeleka LUKUVI MARA kuokoa Jahazi

CCM kweli ni kama vichaa .Kuna wakati walimtuma Ngeleja Tarime eti wakidai naye ana nguvu za kisiasa na mvuto wakala mweleka wakapoteana baada ya matokeo .Leo kilaza Lukuvi anaonwa ni wamaana sana ? Labda kupanga namna ya kutumia polisi nk lakini si kuzima vuhgu vugu huyo Gachuma pekee anajua .Mathayo kupigwa chini ni sawa mbona na yeye alitumia pesa na ujanja wa jamaa wa Pride Tanzania kuingia mjengoni ? Kila muosha maiti naye ataoshwa .Mathayo kaoshwa angali hai .Kwanza hana elimu ndiyo maana anatumia pesa tu kuutaka Ubunge tena wala si akili .
 
Mkutano wa maadhimisho ya miaka 35 ya CCM Musoma mjini yameshindikana na wameahirisha
 
Japo sijawahi kumsikia sana Kambarage Wasira ila Esther namuona sana katika harakati za Vijana hebu tupe U sharp wa Kambarage mkuu
SOMA HIYO BLUE NA NYEKUNDU!
Ester Bulaya hawezi kusimama na Kambarage hata kidogo!
Kambarage Wasira ni kijana sharp,na muelewa hawezi kubebwa ana uwezo wa kusimama mwenyewe hata bila baba yake.
Pia ni mahili wa kujenga HOJA kuliko Ester Bulaya, huwezi kuwalinganisha, ni sawa na Obama na Vicent Nyerere(Musoma Mjini).
Ester kwa Kambarage ANAPWAYA mara 10000.
 
Japo sijawahi kumsikia sana Kambarage Wasira ila Esther namuona sana katika harakati za Vijana hebu tupe U sharp wa Kambarage mkuu

Kambarage yuko fiti ukubali ukatae!
Ukitaka kuamini Muulize huyo Ester Bulaya atakujuza vizuri uwezo wa kijana huyo!
Ester anaonekana kwenye Luninga, Kambarage anaonekana kwa Wananchi(BUNDA).

Kambarage anaendana na vijana, anasema nao, anawashauri, anakubalika, hata wazee wanamuona kuwa nguzo Imara ya kuwatetea vijana hapo Bunda, tofauti na Ester Bulaya ambaye makazi yake yako Dar es Salaam na KASHFA nyingi tu( namtunzia heshima kama kiongozi wa umma).Ukifika Bunda leo hii ukiwanadi Ester na Kambarage usisubili matokeo, Ester atakuwa ameshindwa kabla hawajapiga kura.

Nawasilisha uhalisia.
 
hebu tuambie kuhusu mikakati ya Mathayo kugombea hapo Serengeti ni Kweli?
Na Vipi Hali ya CCM serengeti maana ndo jimbo pekee la Mara ambalo halijaonja Upinzani

Mathayo ameshakubali kwamba hawezi kumng'oa Viceny Nyerere musoma mjini na bahati mbaya sana kwake hawaivi na makongoro Nyerere(m/kiti wa ccm mkoa) lakini pia kutokana na matukio ya ndugu zake kuwapiga watu hadi kuua, watu wa musoma mjini wanachuki kubwa sana dhidi yake pamoja na kujitahidi kutumia fedha kuwarubuni.

Kwahiyo ameamua kuwekeza serengeti ambako kwa bahati mbaya mbunge wa sasa Dr, Kebwe(wakurya wanamuita mnyama, kwakuwa kwa kikurya Kebwe ni Mbweha) ameshindwa kutimiza matarajio ya wanaserengeti, na bahati mbaya m/kiti wa ccm wilaya bw.chandi ndiye alifanya umafia hadi kumuwezesha kushinda. Sasa hivi chandi kwa kushirikiana na m/kiti wa halmashauri ya wilaya bw.ng'oina wanacheza dili na fedha za halmashauri katika kujiandaa kushinda uchaguzi wa ccm ili baadae waweze kumsimamisha mathayo ambaye ana vijisenti vya kutosha.

Katika kujipanga huko amenunua ardhi kubwa sana maeneo ya park nyigoti ambako anaendesha shughuliza ufugaji wa ng'ombe wa maziwa na nyama lakini pia na shughuli za kilimo. Pamoja na hayo amefungua vituo vya mafuta mjini mugumu na hivyo muda wake mwingi anautumia kuendesha siasa zake wilkayani serengeti.

Lakini kutokana na mwamko wa wananchi wilayani serengeti, naamini chadema ikiongeza nguvu na umakini kidogo tu jimbo linatua mikononi mwao, watu wengi wamekuwa na imani na chadema hasa kwa kampeni aliyofanya mgombea ubunge mwl.Marwa Ryoba mwaka 2010. Hivyo kazi ni kwa chadema serengeti na mkoa kujipanga vizuri kulinyakua jimbo hilo.
 
CCM kweli ni kama vichaa .Kuna wakati walimtuma Ngeleja Tarime eti wakidai naye ana nguvu za kisiasa na mvuto wakala mweleka wakapoteana baada ya matokeo .Leo kilaza Lukuvi anaonwa ni wamaana sana ? Labda kupanga namna ya kutumia polisi nk lakini si kuzima vuhgu vugu huyo Gachuma pekee anajua .Mathayo kupigwa chini ni sawa mbona na yeye alitumia pesa na ujanja wa jamaa wa Pride Tanzania kuingia mjengoni ? Kila muosha maiti naye ataoshwa .Mathayo kaoshwa angali hai .Kwanza hana elimu ndiyo maana anatumia pesa tu kuutaka Ubunge tena wala si akili .

Mimi Najua Lukuvi ni fisadi wa elimu!! Sijajua kama alishaweza kununua Vyeti vyenye seal Original!! Ila kwa watu kama hawa wanaonunua Vyeti Tutegemee Maendeleo Katika Hii Nchi ni Ndoto!!
 
Makongoro Nyerere tyr amekiri kuwa million 100 tyr zimechangwa na mafisadi kuhakikisha harudi madarakani,japo amejihakikishia Ushindi,ameyasema hayo katika mahojiano maalum na gazeti la SEMA usikike
 
Tatizo la LUKUVI ni kutokutaka kukosana na mtu hata mmoja.

Inanikumbusha kisa cha jamaa aliyekuwa anakufa na mkewe akaamua kwenda kumwita Padre ili amuombee saa zake za mwisho. Padre kufika akamuuliza kama anamkana Shetani na kazi zake zote, jamaa akasema "Hapana, simkani." Mara mbili akaulizwa na jibu likawa lilelile.

Padre akamuuliza kwa nini hamkani Shetani? Jamaa akajibu "Padre, kwa mtu ambaye yuko kwenye hali kama yangu, siki KIPINDI KIZURI kujitengenezea maadui."

Lukuvi, siku itafika itabidi uamue tu kuwa unataka kumtumikia nani. Hili la hutaki kujitengenezea maadui, halitakufikisha mbali. Kikwete alijaribu sana kulifanya hili ila matokeo yake Chama kinamfima mikononi pamoja na Muungano. Ajitahidi tu walau aweke katiba mpya na Tanzania milele itamkumbuka kwa hilo.
 
Ndo kusema nae kwishnei?

Similar Discussions

Back
Top Bottom